Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,698
- 4,693
Muundo wa serikali yetu, rais analazimika kuteua mawaziri kutoka ktk wabunge. Akikosa mtu anayefaa, rais amepewa nafasi za kuteua wabunge. Utaratibu huo unampa rais nafasi ya kuteua mbunge ili amtumie ktk nafasi ya uwaziri. Ubunge wa kuteua umekuwa ni kama sadaka na zawadi tu.
Katika uteuzi wa mawaziri unaoendelea nchini Kenya, moja ya kigezo kinachoangaliwa na Bunge ili kumpitisha waziri ni taaluma imnayoendana na Wizara. Hii sasa kwa Kenya wanatupiga! Wabunge wote wa Kenya wana digrii. Mawaziri lazima wawe na taaluma husika.
Kwa TZ hali ni mbaya. Unakuta Wizara ina waziri na Katibu mkuu ambao wote hawana elimu ya taaluma husika. Kwa nguvu ya madaraka yao, wakurugenzi, makamishna na wasidizi wao wanajikuta kwenye hali ngumu ya utendaji. Kila siku ni kuhangaika kuona kama waziri au Katibu mkuu anashauliwa au ni Yule anayejidai ni boss tu!
Wizara hazina matokeo yoyote mazuri. Utendaji unapimwa kwa kelele za mawaziri kukemea watu hovyo tu! Kwa kuwa busara za marais hazitumiki, sasa tunataka katiba mpya!.