Katiba Mpya - Muarubaini wa Kero za Muungano

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130


[h=3][/h]


Na Juma Mohammed, MAELEZO


Wajumbe wa Baraza Wawakilishi Zanzibar wamesema muarubaini wa kero za Muungano ni kuwa na katiba mpya itakayoweka bayana mambo yatakayosimamiwa na kila upande kwa uwazi zaidi.


Akiwasilisha maoni ya Kamati ya kudumu ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa kwa makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Mwakilishi wa Kwahani(CCM) Ali Salum Haji alisema ikiwa kutakuwa na katiba itakayobainisha na kuzitambua haki za kila upande wa Muungano anaamini hakuna nchi itakayomlaumu mwenzie.



Mheshimiwa Spika, kwa hiyo muarubaini wa matatizo au Kero za Muungano wetu ni kuwa na katiba ambayo itakayobainisha na kuzitambua haki za kila upande wa Muungano huu na kutofautisha zipi zitashughulikiwa na kila Nchi katika Muungano huu na zipi zitashughulikiwa na chombo cha Muungano hapo tunaamini hakuna Nchi itakayo mlaumu mwenzie kama aidha ni mzigo au anaonewa na mwenziwe” Alisema Mwakilishi huyo.




Mwakilishi huyo aliyewasilisha maoni hayo kwa niaba ya Mwenyekiti wake, alisema hivi sasa hali haiku hivyo kwani mamlaka moja imebeba mambo yak wake na ya Muungano ambapo mwengine anahisi kuwa kuna haki zake za msingi ananyimwa.




“Waheshimiwa Wajumbe sio kama ilivyo hivi sasa kuwa kuna Mamlaka moja imebeba mambo ya kwake na ya Muungano ambapo mwingine anahisi kuwa kuna haki zake za msingi ananyimwa na mwenzake, na hii ndio inayopelekea kuwepo kwa manung’uniko ya kila siku kwa upande mmoja ambapo yamefikia kupachikwa jina na kuitwa kero za Muungano” Alisema Mwakilishi Ali.


Mwakilishi huyo alisema katiba ya Jamhuri ya Muungano, Wizara za Muungano ni chache, lakini kiuhalisia Mawaziri wote waliopo Tanzania Bara wanafanya kazi zao kama ni Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.


“Sasa, je! tujiulize, hii ndiyo sahihi? lakini ukiangalia katika katiba ya Jamhuri ya Muungano, kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Baraza letu la Wawakilishi kwa mujibu wa kifungu cha 64 cha katiba ya Muungano, mamlaka yetu yanaishia hapa hapa Zanzibar tu basi, tafsiri hiyo inabaki kuwa ni sahihi na tumekubali” Aliliambia Baraza Mwakilishi huyo.


Aidha, Kamati hiyo imesema kama wananchi na viongozi wanahisi mambo yalivyo kwa wakati huu sio sahihi basi ni lazima warekebishe katiba na kwa kuwa hivi sasa wananchi wako huru kuzungumza wanachokitaka, lakini kwa kufuata utaratibu na Sheria za Nchi zilizopo hakuna wakati mwengine isipokuwa ni wakati huu.






“Mheshimiwa Spika, kamati yangu inaamini hayo yote yanawezekana ndani ya Muungano wetu bila ya hata kutengana, kwani huu ni Muungano wetu sote na sitegemei kama atatokea kiongozi atakaetaka kumdhulumu mwenziwe, kikubwa hapo kila mmoja ajenge hoja, itakayomridhisha mwenziwe” Alisema Mwakilishi huyo.


Aidha, Kamati hiyo imewaomba wananchi wa Zanzibar kujiandaa vema kwa kujenga hoja za msingi katika mchakato wa kutoa maoni katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


“Nawaomba sana wananchi wetu wa Zanzibar wajenge hoja zao kwa kurekebisha vifungu vilivyomo kwenye Katiba na kama kuna tofauti ya mawazo basi ni vyema watu wasipikiane majungu, sijui huyu Uamsho, huyu anabururwa na CUF, huyu anabururwa na CCM, haya yote hayatusaidii kwa hivi sasa na hili ndio tatizo letu Wazanzibari, kazi yetu ni kulalamika tu sio kujenga hoja zitakazoisaidia Nchi” Alisema Mwakilishi Ali.


Aliongeza kwamba ni vizuri kwa wananchi kuzisoma katika zote mbili ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nay a Zanzibar.


“Lakini na wao wajenge hoja zao ili kuonyesha namna wanavyohisi wao, kwa hiyo ni vyema kuisoma Katiba kama ilivyoandikwa na kwa sisi Zanzibar ni lazima kuzisoma katiba zetu zote mbili na baadae kuweza kujenga hoja zetu vinginevyo tutapotea” Aliongeza.




Imewekwa na MAPARA at 7:03 PM Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
 
Tatizo hapa sio Muungano ,tatizo ni mfumo mpovu wa huu Muungano wenyewe kila upande unahisi unazulumiwa katika mfumo huu wa Muungano.

Mimi nahisi muarubaini wa Muungano nikuufumua upya huu Muungano wenyewe kwa kurudisha Serekali ya Tanganyika na mamlaka zake zote na Serekali ya Zanzibar na mamlaka zake zote, halafu ndio waulizwe watu wa pande zote mbili husika Jee ni mambo gani nagani wayafanye yawe ya Muungano ili kila upande ijuwe haya ndio ya Muungano?.

Lakini hivi sasa hakuna Muungano kuna vurugu mechi tu na utata wa Muungano, na utata huu umechangiwa zaidi na ccm na halmachauri kuu yake kujifanya wao ndio Muungano na ndio wenye mamuzi yote ya Muungano, hili ndio lililo fanya zaidi kuchangia utata na kuonekana Muungano huu ni wakisiasa zaidi kuliko wa kimahusiano ya nchi na nchi.

Ccm wanajaribu kutafuta vishingizio vingi tafauti tafauti ili tu kuwalahai wananchi wakati watu wote wako wakeup. kuna hoja husema eti Muungano unalindwa kwa sababu ya Wazanzibar waliojimarisha Bara, hii ni hoja zaifu na nivisingizio vya viongozi kuchechea chuki zidi ya Watanzania wa Bara na Wazanzibar hoja hii ife ni kuchechea chuki.

Kuna mifano mingi tu hai na isio na ubaguzi wa watu fulani, nikama Wachina ,Wasouthafrica Wahindi,Warundi,Wazambia na wenginewo hawa wote sio jumuia ya Muungano wa Tanzania lakini wanaichi Tanzania na kufuata sheria zote za nchi kwa hio na hata uvunjike Muungano basi as longger Wazanzibar waloko Tanganyika na Watanganyika waloko Zanzibar watafuata sheria za nchi na taratibu zake basi mimi naona hakuna tabu kwa vile wako wasio Watanzania lakini wanafuata sheria za nchi?.

Lakini kusema kisingizio kuwa Muungano una lindwa kwaajili ya wao hio sio kweli, Muungano wa sasa umebezi sana kisiasa kuliko kijamii za pande mbili za Muungano, ndio ukaona una matatizo mengi ya kiutendaji kwajili ya kisiasa.
 
icho ndio kitu cha msingi na wala sio kusubiri waznz watoe maoni yao kwenye katiba mpya, kama ni vilio, michango, hoja ziko wazi ni uvivu tu wa baraza la wawakilishi kuamua kupiga kura ya maoni hivi sasa. hizi hoja za waznz walioko bara watapata tabu ni kivuli cha viongozi kuogopa kukosa ulaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom