KATIBA MPYA: Meya na Mwenyekiti wa Halmashauri Wachaguliwe na Wananchi

Kishili

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
295
225
Naomba kuwashawishi wanajanvi kujitokeza kwa wingi na kutoa maoni kwenye tume ya maoni ya katiba mpya na kupendekeza kuwa ili kuziimarisha Serikali za mitaa ambazo ndizo hasa ziko karibu zaidi na wananchi, Mameya wa miji manispaa na majiji au wenyeviti wa halmashauri za wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi na siyo madiwani kwa sababu zifuatazo;

1. Ni makosa mno kimifumo ya kiungozi Meya au Mwenyekiti wa halmashauri kuchaguliwa miongoni mwa madiwani kwani diwani ni kiongozi aliyejipima kisaikolojia, akili na nguvu kuwa anaweza kuongoza kata yenye vjiji vitatu hadi vitano sasa huyu anakuja kukabidhiwa jukumu la kuongoza wilaya yote yenye vijiji karibu mia au zaidi yenye jimbo moja au matatu wakiwemo na wabunge wenye uwezo kuliko yeye! Wengi wao hulemewa lakini hawajivui kwa vile madaraka hayo huendana na marupurupu.

2. Kumchagua Diwani kuwa meya au mwenyekiti wa halmashauri ni kuendeleza utaratibu ambao unakataliwa wa wabunge kuwa mawaziri hivyo kuendeleza upendeleo wa maeneo yao(kata) na kufifisha uwakilishi wa wananchi kwenye halmashauri.

3. Meya au Mwenyekiti wa halmashauri kuchaguliwa na wananchi kutaongeza hadhi ya nafasi hizo hivyo zitakuwa zinawaniwa na watu wenye uwezo wa kiuongozi na kielimu kukidhi nafasi hizo kuliko ilivyo sasa ambapo viongozi hao huendeshwa na matakwa ya watendaji tu.

4. Meya au Mwenyekiti wa halmashauri kuchaguliwa moja kwa moja kutazifanya halmashauri kuwa imara zenye nguvu zaidi hivyo kupunguza unyanyasaji na uingiliaji wa ovyo wa serikali kuu na kuongeza uwezo wa halmashauri kusimamia watendaji hivyo kupunguza ufisadi kwenye halmashauri na wananchi kupata maendeleo zaidi.

Kwa hayo na mtakayoongeza itakuwa ni muhimu sana iwapo katika katiba mpya Meya na Mwenyekiti i wakachaguliwa na wananchi wa halmashauri husika katika uchaguzi mkuu
Naomba kuwasilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom