SoC01 Katiba Mpya: Mchakato muhimu 'uliotekwa nyara' na wanasiasa

Stories of Change - 2021 Competition
May 7, 2021
29
64
Wanasiasa wote Duniani muda wote hufikiria madaraka,kwenye madaraka hawana mchezo wanaweza kufanya lolote ili kupata madaraka au kukumbatia madaraka yao.Ni siasa za kuchumia tumbo,wanataka au wanakumbatia madaraka ili yawanufaishe wao,kaya zao au ndugu zao na si vinginenyo.

Wote wanasiasa wa upinzani na watawala hawafanyi siasa nje ya kufikiria madaraka na ndiyo maana wameuteka mjadala wa katiba mpya.Chama cha mapinduzi wanahofia mabadiliko ya katiba yataleta tume huru ya uchaguzi ambayo inaweza kuwahhng'oa madarakani na upinzani unaamini tume huru ya uchaguzi ndiyo suluhisho la wao kuingia madarakani .

Lakini kuna mambo mengi ya muhimu nje ya madaraka ya wanasiasa ambayo yangeingizwa kwenye katiba mpya yangekuwa na manufaa kwa taifa bila kujali vyama vya siasa na madaraka ya wanasiasa.Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na;

Uraia pacha
Duniani kuna nchi zaidi ya 60 ambazo zimeruhusu uraia pacha na kati ya hizo kuna nchi tajiri zaidi Duniani kama Marekani,Uingereza,Canada,Italia,Ujerumani,Hispania na Ufaransa zilizoruhusu uraia pacha na Afrika nchi kama Algeria,Nigeria,Afrika kusini na Angola zimeruhusu uraia pacha.Faida ya uraia pacha ni nyingi kwanza tutaweza kuwarejesha waliokuwa Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine ambao wanaweza kuja kuwekeza na kufanya biashara na hivyo kuchangia katika uchumi wa nchi yetu.Pia wangeweza kuja kuleta utaalam na ujuzi walionao.

Yussuf Poulsen ni mcheza kandanda ambaye anachezea timu ya RB Leipzig ya Ujerumani mwaka huu pia alikuwa mmoja wa wachezaji wa Denmark waliocheza michuano ya mataifa ya Ulaya.Baba yake Yussuf ni Mtanzania aliyetokea Tanga na mama yake ni raia wa Denmark.

Malaika Mihambo yeye ametwaa medali ya dhahabu katika mchezo wa kuruka mbali katika michezo ya Olympic inayofanyika Japan akiiwakilisha Ujerumani.Mama yake ni Mjerumani na baba yake ni Mtanzania.Watu kama hawa wapo wengi ambao Tanzania ingeweza kunufaika nao na si lazima kuwapa uraia ili wachezee Tanzania lakini tungeweza kunufaika nao kwa namna nyingi kama kuwa mabalozi wa utalii,mabalozi wa uwekezaji,wangeweza kuja kuwekeza kwenye michezo na uchumi pia wangeweza kuja kufundisha michezo vijana wa Kitanzania.

Uchaguzi mdogo
Kuanzia oktoba 2020 mpaka julai 2021 Tanzania imefanya uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo matatu ambayo ni Konde baada ya kufariki Khatib Haji,Muhambwe baada ya kufariki Atashasta Nditiye na Buhigwe baada ya Dk.Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais. Na hivi karibuni kutakuwa na uchaguzi mdogo katika majimbo ya Konde baada ya kujiuzulu Sheha Mpemba Faki ambaye amejiuzulu kabla ya kuapishwa na Ushetu baada ya kufariki kwa Elias Kwandika.

Uchaguzi mdogo unaligharimu sana Taifa bila sababu za msingi , fikiria jimbo la Konde linafanya uchaguzi mara tatu ndani ya mwaka mmoja na hii mara ya tatu ni kutokana na Watawala kuchezea uchaguzi ,hawafikirii fedha inayotokana na kodi za Watanzania kupotea.
Fedha hizi za kufanya uchaguzi mdogo zingeweza kwenda kuboresha huduma za afya,kujenga madarasa,kujenga miundombinu ya maji na kufanya mambo mengine ya muhimu na tungeweza kuziepuka uchaguzi hizi kwa kubadili katiba na kuchagua chama badala ya mtu.Chama kinachoshinda ubunge au udiwani ikitokea diwani au mbunge wake kafariki au kajiuzulu chama husika kiteue mwanachama wake awe mbunge au diwani wa eneo hilo bila kuitisha uchaguzi.

Mfumo huu si mpya nchi nyingi Duniani zinautumia pia hata hapa Tanzania unatumika kwenye viti maalum vya ubunge na udiwani pamoja na Urais na ndiyo maana alipofariki Dk.Magufuli hatukufanya uchaguzi na ikitokea Rais Samia akajiuzulu Urais hakutakuwa na uchaguzi bali Dk.Mpango atakuwa Rais bila kufanya uchaguzi.

Kama nafasi kubwa ya Urais inawezekana kutokufanya uchaguzi inashindikana nini kwenye ubunge na udiwani?nchi yetu bado ni masikini sana tutumie fedha za walipa kodi kwa manufaa ya Watanzania wote ili ziweze kunufaisha kizazi cha sasa na kijacho.
 
Nchi tajiri zinaona fursa ya uraia pacha lakini nchi masikini zinaupinga.Marekani inafaidika sana na raia kutoka nchini nyingine, kwenye Olympic imepeleka Wanamichezo wengi wenye asili ya Afrika.
 
Back
Top Bottom