Katiba mpya: Mbunge/ diwani degree: Rais degree na uadilifu usiotiliwa mashaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya: Mbunge/ diwani degree: Rais degree na uadilifu usiotiliwa mashaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Aug 9, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Bunge letu linaonyesha linawatu ambao hawajui kwa nini ni wabunge na halmashauri zetu zinaendeshwa kama gulio. Elimu ni muhimu sana pamoja na kwamba na mambo mengine yanahusika katika uongozi kama hekima, busara, uwezo wa kufikiri, utashi, ubunifu nk ila kwa sasa elimu inatuangusha sana.

  Wabunge wetu wengi wananunulika kirahisi ama na vyama vyao au mafisadi au mijadala kwa sababu hata uwezo wa kusoma hotuba, bajeti za wizara, sheria za bunge na kuzipamabanua hawawezi. Wengine hawawezi hata kuainisha ukweli, majungu, siasa, na habari za kutengeneza. Wabunge wengi hawajui mahusiano ya nyaraka za serika na kazi ya bunge, hawawezi hata kufanya kautafiti kadogo tu. hali hii vile vile iko kwenye halmashauri zetu nyingi.

  Hatuwezi kuendelea tusipobadili huu utaratibu wa kiongozi anatakiwa kujua kusoma na kuandika tu. Katiba iseme wazi lazima awe na degree walau moja tu kutoka chuo kinachotambuliwa na kilichosajiliwa.

  Kwa sasa Tanzania inazaidi ya vyuo vikuu 30 na kuwa na uwezo wa kila kijiji kuwa na msomi wa degree walau moja, wakati umefika kuendana na wakati na kasi ya maendeleo ya dunia.

  Raisi Lazima awe na degree moja na lazima awe na record ya uwajibikaji, asiwekuwa na kashfa ya aina yeyote ya matumizi mabaya ya ofisi yeyote ile iwe ya umma au binafsi. Lazima apimwe uwezo wake wa utendaji kazi na awe mwadilifu na mwenye uwezo wa kukemea uovu bila shaka.

  Katiba iweke wazi, Raisi akishindwa kuwajibisha wahalifu na wala rushwa wanaotuhumiwa bila mashaka yeyote yale kwa rushwa, uzembe, uhujumu na kutokuheshimu wananchi Raisi atolewe madarakani kwa kura zakutokuwa na imani naye.

  Mahakama ziwe huru na kila jaji apitishwe na bunge na awajibike bungeni sio kwa Raisi. Usalama wa taifa uwajibike kwa bunge

  Takukuru ifutwe iunganishwe na CID kuwe na vitengo mbali mbali kama rushwa, uhalifu, cyber crime, na uhalifu wowote wa ndani ya nchi kwa mtu yeyote na hiki kitengo kisiwe chini ya polisi kiwe ni kitengo kinachojitegemea.

  Polisi ivunjwe na iwe ina endeshwa kimkoa na jinsi ya kupata polisi kila mkoa uwe na utaratibu wake, mkuu wa mkoa awe ndiye mwenye jukumu la kulinda na kuteuwa mkuu wa polisi na kuhakikisha ulinzi wa mkoa wake.

  Mkuu wa mkoa apigiwe kura na wananchi wote na asiwe wa kuteuliwa. Kuondoa vyeo vyote vya kuteuliwa mkoani na madaraka mengi yabakiye mkoani.

  Tuwe na wizara sizozidi kumi na mbili tu na za kudumu.

  Mungu utusaidie tufike tuendako salama

  Chief Mkwawa wa kalanga
   
 2. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mkuu ni kweli kabisa! kuna wabunge wengi wamekuwa na mawazo ambayo mpaka yananitia mashaka kama kweli wana uwezo wa hata kuzisimamia kamati za maharusi! this is an appalling situation!
   
 3. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kama ni SLAA hagombei, hana degree.
   
Loading...