Katiba mpya: Mbona kila kitu kiko wazi wanachong'ang'ania serikali ya ccm ni kipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya: Mbona kila kitu kiko wazi wanachong'ang'ania serikali ya ccm ni kipi?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mtu wa Mungu, Apr 7, 2011.

 1. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna somo kubwa kwa watanzania kwa muswada uliopelekwa bungeni kuhusu hoja ya kuandika katiba mpya!!!!!

  Kwanza Kongamano la UDASA siku ya Jumamosi tarehe 2, Machi 2011, liliacha waTz midomo wazi, wakishindwa kuelewa dhamiri ya yale yaliyoandikwa ndani ya muswada huo!!!!!!!. Ilionekana kutoingia akilini mwa walioelewa mapema kwa serikali yenye nia njema na mustakabali wa uhai na heshima ya wananchi na nchi kuweza kuandika muswada kama ule!!!!!!!!.Ni dharau kwa waTz;

  Kwa sababu gani? Kwa mTz wa kawaida maswali mawili yanabaki bila majibu:-
  1: Kimsingi wananchi ndiyo wadau na wamiliki wa katiba kama mwongozo wa jinsi wanavyotaka wajitawale-yaani waajiri wa vyama vyote vya siasa nchini; chama tawala na serikali yake ni waajiriwa waliopata ajira baada ya mchujo kwa njia ya kura huru; wakati vyama vya upinzani vikiwa vimebakia katika orodha ya kusubiri-waiting list;
  2: Kwa mswada uliopelekwa bungeni sisiemu na serikali yake ambao ni waajiriwa ndiyo wamepora nafasi ya wananchi kwa kuchukua na kusimamia mchakato mzima wa maandalizi ya katiba-mwongozo wa jinsi ya kutawala nchi !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Kwa ambao ni wadadisi wa mambo ya siasa na uchungu na nchi hii, wanaona kabisa kwamba bila shaka kuna jambo??????; Iweje itoe tafsiri kwamba CCM na serikali yake wanaelekea kuelewa fika agenda ya siri iliyomo ndani ya muswada huo; ambao kwa uwazi unaonekana kabisa hauna dhamiri njema na utashi wa kisiasa kwa tafsiri ya mTz mwenye akili timamu, zaidi ya provocation of maandamano ili watumie nguvu ya dola kuzima maasi??????;
  Kwa maoni ya kawaida CCM na serikali yake wamelenga kwamba muswada huo usipopita, basi watakuwa wamepata sababu ya kuendeleza delaying tactics hata mpaka mwaka 2020!!!!!!!!!!!!;
  Lakini ukweli ni kwamba CCM na serikali yake wanajenga mazingira ya machafuko nchini ili hatimaye rais wao atangaze hali ya hatari, na kuanza utawala wa kiimla na kidikteta!!!!!!;
  Kwa kuwa CCM na serikali yake hutawala kiujanja ujanja, si ajabu mradi wa Loliondo ulilenaga kuwapumbaza waTz -wakidhani kwamba hili ni taifa la mazezeta kwa vikombe vya babu wa Loliondo ili watawalike kirahisi;
  Hata namna mchakato wa kiini macho cha kile kinachoitwa kupata maoni Dar na Dodoma kwa mtu ye yote mwenye akili timamu anaona kabisa kwamba ni danganya toto!!!!!!
  CCM wamedhamiria kupeleka nchi puta katika hili, na kama atatokea mtu ama chama kupinga kwa njia ya maandamano, angalia yaliyotokea Dar na Dodoma;
  Jamani kwa yale yaliyotokea kwenye kongamano la UDASA na leo kuthibitishwa na yale yaliyotokea Dar na Dododma waTz wamechoka kutawaliwa na CCM na serkali yake kama vile wananchi wa nchi za kiarabu walivyochoka kutawaliwa na watawala wale wale kwa miaka nenda rudi, na sasa wameamua kwa dhati kuwa ni aluta continua mpaka kieleweke tu ndiyo solution!!!!!!!!!!!!!!!

   
 2. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hivi ni sahihi huo mjadala kujadiliwa Dodoma na Dar es Salaam tu? kwani sehemu zingine siyo sehemu za Tanzania? Je,wanadhani maoni ya watu wa Dar na Dodoma ndiyo representative ya maoni ya watu wa wote wa nchi hii? Jamani mbona watu wanaohubiri amani ndiyo wanaoleta mazingira yanayoweza kupelekea kuleta uvunjifu wa amani? Ikitokea hivyo god forbid nani wa kulaumiwa?? Nashindwa kuelewa utawala wa Kiimla wa CCM unachokifanya!

  Siyo kila jambo mnalifanyia siasa,suala la katiba na mchakato wake si suala la kulifanyia siasa. Tuweke mchakato mzuri unaokubalika na watanzania wengi siyo kundi dogo la watu wanaodhania watawala milele. Ni vyema mkaelewa kwamba wakati mtakapokuwa nje ya utawala mtagundua kwamba mlifanya kosa kufanya mambo kipuuzi kama mnavyotaka kufanya.

  Mnashabikia mambo ya kijinga sasa lakini baadaye mtajutia ujinga wenu.
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Kweli sasa Watanzania wamevaa ujasiri wa ama kufa ama kupona ...ukiona wananchi walichofanya tegeta ndo upime uone kama bado kuna uvumilvu,utulivu na hyo amani ...umma umeamua kuonyesha kwamba sasa HUMILIATION,EXPLOITATION,INJUSTICE,DEHUMANIZATION etc. are NO longer torelable ANY MORE

  THE SAGA CONTINUES ......,BUT THE SAGA HAS JUST BEGAN
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
   
 5. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi kumbe hata polisi nao wameanza kuchoka: jana huko Tegeta polisi walipoitwa kuja kuokoa mauaji walijibu kwamba acha wauane kwanza, watakaopona watawapa taarifa ya kuandika kwenye ripoti!!!!!!!
  Kikwete na serikali yake wakiwategemea polisi hawa, ambao kwa upande mwingine watakuwa pia wanahofia familia zao na ndugu zao kuuawa wakijaribu kufanya yale ya Arusha kwa nguvu kubwa ya umma ambayo inaandaliwa kukabiliana na vuguvugu la katiba mpya, watakuwa wanajidanganya. Zidumu Pipooooooooooos Pawa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...