Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,184
- 671
waungwana baada ya muamko wa kutaka katiba mpya mm nilikua na mapendekezo haya yafuatayo katika ucahguzi wa kumchagua Rais wa Jamhuri yetu ya muungano.
kwanza ningependa kuona kuwa Rais wa Jamhuri yetu anatoka upande mmoja wa muungano mara moja na inayofuata atoke upande mwengine (nnakusudia nchi zilizounda muungano sio tuache tu mtu yeyote kutoka upande wowote awanie hii huenda ikazaa malalamiko ambayo kwa chini chini yapo kuwa upande mmoja wa muungano unatawaliwa na upande mmoja unatawala).
Pointi ya pili ni kuhusu kura ambazo zinamuweka Rais madarakani, ningependekeza Rais wa Jamhuri wa muungano lazima ashinde kwa zaidi asilimia hamsini kwa kura za Kila upande wa jamhuri na sio kuzihesabu kura zote na kushinda zaidi ya hamsini asilimia
nnakusudia kusema kwa vile zanzibar kuna wapiga kura wachache huenda ikatokea Rais wa jamhuri akawa hatakiwi upande mmoja wa muungano lakini upande wa pili wakamchagua na ukienda kwenye majumuisho akashinda kwa zaidi ya asilimia hamsini na kuwa Rais, kitu ambacho kinaleta malalamiko kuwa Rais huyo hawezi kuwa wa muungano bali rais wa upande mmoja tu wa muungano
nnapenda kuwasilisha mapendekezo yangu haya kwenu waungwana tuyajadili