MAONI KUHUSU KATIBA MPYA
Kwanini mambo yote yawe ya Muungano
Kufuatia mgogoro uliopo baina ya pande mbili za kisiasa kushindwa kufikia muafaka juu ya muundo wa serikali ningependa kusema tatizo la nchi yetu lipo ndani zaidi ya swala la idadi ya serikali zetu iwe 1, 2 au 3 kwa sababu serikali huundwa kwa minajiri ya kugawana mamlaka ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Na ifahamike tu kwamba hakuna muundo maalum wa serikali ziwe ngapi ktk mfumo wa washirika ktk utawala wowote iwe ule wa Muungano (union), Shirikisho (federation), Jumuiya (Confederation/Community) kwa sababu ushirika haujengwi kwa idadi ya serikali bali hali halisi ya matakwa ya wananchi ktk ushirika wao kwa masharti na malengo walotaka kuyafikia ndio hujengwa serikali zake ili kuwafikia wananchi haraka na wepesi zaidi.
Mgogoro wa kisiasa
Sintojikita ktk mgogoro wa kisiasa ulofuatia bunge maalum la katiba kuvunjika kwa sababu huo ni mjadala mrefu sana pengine tutaugusia pale inapopaswa isipokuwa nitakwenda moja kwa moja katika kutoa maoni yangu kuhusiana na mapungufu ya kiutawala ndani ya katiba iliyopo ambayo wananchi walikusudia kufanywa na sio mgogoro juu ya Muungano wetu ama serikali ngapi zinafaa kwa sababu kati ya wananchi walochangia sana mjadala huu wa katiba na kuufuatilia kwa ukaribu sana toka mwaka 2002 hapa JF mimi nilikuwa mmoja wapo.
Kwa mtazamo wangu, baada ya kutazama kwa kina malalamiko ya pande zote mbili ambazo zingependa sana kuishi pamoja kwa amini na utulivu lakini wameshindwa kufikia muafaka wowote juu ya Mustakabali wa taifa hili ndani ya UTAIFA huu imetokana na wote kushindwa kuingia ndani zaidi kutazama kiini cha matakwa ya wananchi bali wametumia siasa zaidi kupanua wigo la hoja za Muungano wenyewe jambo ambalo wangeweza kuwakilisha hoja hiyo katika vikao vya bunge na kadhalika pasipo kuathiri uandishi wa katiba tuitakayo. Hivyo nimekuja na mapendekezo ambayo nina hakika yatagusa hisia za wananchi wa sehemu zote za JMT ikiwa ni kuanza na muundo wa UTAWALA na mamlaka yake.
Ni imani yangu kwamba kutokana na hoja za pande mbili zote ambazo zimejikita zaidi ktk Muungano na serikali ukiwasoma kwa undani utagundua kwamba wanahitilafiana zaidi ktk kugawana MAMLAKA ya utekelezaji wa shughuli za serikali hivyo matatizo hayapo ktk aidha kwenye Muungano wenyewe ama idadi ya serikali. Lakini hata utawala huu umejaribu sana kuongeza hesabu za mikoa, wilaya na hata majimbo lakini kwa vile mabadiliko hayo hayatoi mamlaka kamili kwa vyombo vya serikali hizo ili kutekeleza majukumu yao na kuwajibishwa na wananchi, mabadiliko hayo hayakuleta mafanikio zaidi ama kupunguza kero za wananchi.
Hivyo katiba yetu bado inapwaya sana ktk kutoa mamlaka kwa wananchi na serikali, serikali na halmashauri zake kwa sababu bado mfumo mzima wa utawala wa nchi hii upo bado ktk mageuzi (transition) ya Kisiasa na kiuchumi na ilitakiwa hatua kwa hatua kuweza kufikia mageuzi kamili ikiwa KATIBA ya nchi yetu hii itabadilishwa na kutoa mamlaka hayo kwa vyombo vinavyostahili kuleta mabadiliko yanayokusudiwa. Sheria mama ndiyo dira na mwongozo wa mabadiliko yote na sii kutegemea muundo wa washirika ama idadi ya serikali ndizo hupelekea kupata maendeleo.
Hivyo kwa kuwa naamini kwamba mgogoro mkubwa wananchi wa pande zote mbili unahusiana na maslahi ya nchi hizo inaonyesha wazi kwamba katiba iliyopo ina mapungufu ambayo hayakomei ktk washirika wa muungano wa nchi hizi mbili bali mgogoro huo unashuka hadi ktk tawala za mikoa, wilaya na miji yake kwa madai ya kutopewa huduma bora kulingana na mahitaji yao. Mapungufu haya ya muda mrefu yamezua kero nyingi sana toka Halmashauri za mitaa, miji, wilaya, mikoa, serikali 2 hadi imefikia watu kutokuwa na imani na viongozi ama serikali zao kwa sababu ya muundo mzima wa Utawala wa nchi yetu ulijengwa ktk misingi ya Kijamaa.
Chama tawala kilikuwa na mamlaka yote ya kiutawala toka uchaguzi wa wajumbe wa nyumba kumi, viongozi wa halmashauri, wabunge, mawaziri, baraza kuu la Mawaziri (executive council), mahakimu, uteuzi wa viongozi wote wa taasisi serikali, mashirika ya umma, vyoombo vya serikali, vyama vya ushirika, uteuzi wa watendaji wakuu wa ngazi zote za serikali, nafasi za kazi kwa waajiriwa na kadhalika. Chama tawala pia kilikuwa ndicho chombo pekee kilichomiliki njia kuu za uchumi ambazo ni pamoja na Ardhi, maji, madini, misitu, mafuta, nguvu za umeme, usafiri, njia za habari, bishara za nje, mabenki, bima, viwanda vya chuma, silaha, simenti, mbolea, viwanda, ugawaji na mambo mengi makubwa ambayo kwa wakati ule ndio ilikuwa msingi mkubwa wa ujenzi wa UTAIFA wetu.
Haya yote ni mambo yalokuwa ktk siasa ya Ujamaa na Kujitegemea chini nya chama kimoja na haya hayawezi kuondoka kwa kubadilisha ushirika wetu iwe kwa kuvunja muungano ama kujadili idadi ya serikali zetu, ititiri wa vyama vya siasa na mahitaji yao bali yanahitaji mabadiliko makubwa ya katiba yetu ili Mamlaka hayo yote yapelekwe katika sehemu zinazohusika ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli zote za serikali, taasisi na na vyombo vya kijamii ambavyo ndivyo pekee leo hii vinavyotakiwa kuwajibika ktk kushiriki katika kutoa huduma, haki na usawa wa jamii hii. Hatuwezi kuendelea na mfumo ule ule tukitegema kubadilika kwa serikali ndio muarobaini wa mapungufu makubwa ya kikatiba uwajibikaji na mamlaka ya vyombo vya utekelezaji.
Ni Imani yangu kwamba Watanzania wengi wameitaka katiba mpya ambayo italenga kuondoa mapungufu ya katiba yetu ya mwaka 1977. Wananchi wanaitaka katiba ambayo inayojitosheleza ktk maswala yote UTAWALA, KISIASA, KIJAMII na KIUCHUMI kulingana na mazingira ya dunia tuishiyo, hivyo basi
Napendekeza MUUNGANO na sio SHIRIKISHO uendelee kuwepo isipokuwa ktk sehemu ya kwanza ibara ya 4 (3) ya katiba ya JMT ya mwaka 1977 pamoja na rasimu ya katiba ya tume ya Warioba ziyaweke MAMBO YOTE YAWE YA MUUNGANO isipokuwa Ushuru wa bidhaa na mapato yasokuwa ya kodi kama liseni na sheria. Kwa kufanya hivo Serikali zetu, Manispaa, Mashirika ya Umma, na vyombo vya serikali kama TISS, NEC, na kadhalika yote yapewe mamlaka kamili ya kupanga Utekelezaji wa shughuli zao kama itakavyo ainishwa pasipo kuvunja masharti ya katiba na hivyo kuwajibika moja kwa moja na sheria mama ilotungwa kwa manufaa ya wananchi ili kukuza amani na utulivu.
Mambo yote yakiwa ya Muungano yataweza vipi kuondoa mapungufu na kufuta kero za wananchi? Hili nitalizungumzia baada ya kujibu hoja za wanabodi ambao watakuwa na haja ya kulizungumzia hili.
Nawasilisha
Invisible, Mzee Mwanakijiji, Kibunango, Pasco, Mdondoaji, lynxeffect22, JokaKuu Mag3 Mchambuzi Nguruvi3 Barubaru, Waberoya, AshaDii, Zakumi, Mama Mdogo, Ngongo, Nyamizi, Mimibaba, Katavi, bona, Janjaweed, zumbemkuu, TUJITEGEMEE, Mwelewa, MTAZAMO, amkawewe, gfsonwin, Englishlady, Sikonge, Mgaya D.W

Last edited by a moderator: