Katiba Mpya lazima kwa mustakabali wa amani na maendeleo yetu

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Katiba ni mwongozo au msahafu wa nchi uliotungwa na wananchi, ambayo ni sheria mama yenye msingi madhubuti wa kutoa mamlaka za kisheria zinazo akisi matakwa ya wananchi.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977 asili yake ni matakwa ya watu wachache wakiamini katika kuwakilisha maoni ya wengi bila ushirikishwaji wa wananchi ndiyo maana kuna wakati inatoa mianya ya kutoa na kunyang'anya Haki.

Zipo sababu ambazo watawala hawaamini kuwa katiba mpya ni suluhisho,kwa kuwa wanaamini kwa Katiba hii inayo mpa mamlaka rais wa nchi kuwa mwenye miliki na nchi hii,ina wapa nguvu ya kimamlaka kuendelea kutawala kwa misingi wanayo taka wao.

Hapo ndipo unapotokea ulazima wa hitaji la katiba ya wananchi, itokanayo na matakwa ya wananchi wenyewe, yenye uwezo wa kutoa haki bila upendeleo na yenye meno kwa maana ya kuwajibisha pale haki inapokanyagwa.

Ndiyo maana tusitegemee kwa katiba hii watawala wapo tayari kuiacha kwa mbadala wa katiba nyingine.

Kwa katiba hii inayo mfanya rais kuwa juu ya sheria imetengeneza matabaka ya haki ya kuhoji uhalali wa chaguzi zetu nchini.

Katiba yetu inampa kinga rais kwa matokeo ya uchaguzi uliomweka madarakani kutohojiwa mahakamani, lakini imetoa mwanya huo kwa wabunge na madiwani kuhojiwa mahakamani kupitia uchaguzi huo huo, hali inayo mfanya mtawala kujenga kibri cha kimamlaka.

Katiba hii imempa kinga rais kutoshitakiwa mahakamani kwa makosa aliyo yatenda akiwa madarakani, lakini imeweka wigo mwembamba kwa bunge kumuondoa madarakani pale bunge linapo kosa imani naye, kwa kuweka mlolongo mrefu unao leta mzunguko usio na tija kwa nchi inayo jinadi inafuata misingi ya utawala bora.

Ibara ya 37 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano imetoa masharti ambayo yana kinzana na uhalisia, kwa maana ya jaji mkuu aliyeteuliwa na rais na kuapishwa na rais ndiye mwenye kufikishiwa tuhuma ,na ndiye mwenye kuteuwa kamati ya kuzichunguza tuhuma na kuzipeleka kwa spika ambaye naye ni kada aliyeteuliwa na kamati kuu ya chama chini ya rais ambaye ni mwenyekiti wa chama.

Huu ni utata ikiwa kesi ya mbuzi apelekewe fisi, haki itakuwa kizungumkuti.

Tuna tambua urais ni taasisi lakini kwa ibara 37 ina ondoa haki ya kushauriwa kitu kinachofanya rais kujiona Mungu, na ukimpata asiye na hekima atawaburuza kwa matakwa yake atakavyo.

Sura ya kwanza ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 1. Inasema Tanzania nchi moja yenye Jamhuri ya Muungano.

Lakini Zanzibar kwa sasa nayo ni nchi yenye mamlaka kamili inayotambua kuwa kuna nchi mbili zenye serikali mbili ndani ya Jamhuri ya Muungano kinyume na tamko la katiba ibara ya 2 inayotambua Tanzania visiwani ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano.

Lakini pia ibara ya 102(1) inasema; kutakuwa na serikali ya Zanzibar, itakayo julikana kama "serikali ya Mapinduzi Zanzibar " ambayo itakuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kwa mujibu wa masharti ya katiba hii.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano haitambui Zanzibar kama nchi, inaitambua kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano.

Hii inaibua utata mkubwa pale Zanzibar inapojitambua kama nchi yenye Mamlaka kamili, ukizingatia Tanganyika imejificha kwenye koti la Muungano.

Huu ni utata unao paswa kutatuliwa kwa matakwa ya pande zote mbili juu ya Tanganyika na Zanzibar.

Lakini pamoja na taharuki lukuki, mantiki ya hoja yangu ni ukimya wa katiba pale katiba inapovunjwa na kuifanya uvunjaji wa katiba ni fumbo la imani.

Hapo ndipo tunapoona nyufa za Muungano zipofichwa kwenye koti la uchama, hali inayosababisha kuporwa haki nyakati za uchaguzi katika kudhibiti taharuki zitakazo ibuliwa na chama kingine kitakacho ongoza dola kwa upande wa Visiwani.

Kujinasibu Muungano uko salama wakati nyufa zake ziko wazi ni kujikaanga kwa mafuta yetu wenyewe.

Ndiyo maana katiba mpya ni hitaji sahihi kwa wakati sahihi si suala la hisani kwa watawala.

Leo ukimfungia mtu ndani kwa lengo la kumdhibiti asijuwe kilichoko nje, maanake ni kumuongezea hamasa ya kutaka kujua kwanini anazuiwa kuona kilichoko nje, ndo maana kamati ya Jaji Warioba iliona umuhimu wa mjadala mpana wa katiba hususani mmambo ya Muungano.

Tukiacha kwa kauli za kejeli kwa kudhania kuzuia katiba ni mbinu imara ya kuwadhibiti watanzania wenye mtazamo mbadala kuongoza dola hakika tutakuwa tumejipalia makaa ya moto.

Hatuna budi kama nchi kuitaka serikali kuacha kibri cha kimamlaka,kwa kuzuia mchakato wa katiba ulio gharimu fedha za walipa kodi kupewa kipau mbele uendelee ili wananchi waamue wenyewe mustakabali wa nchi yao.

Kuzuia madai ya katiba ni sawa na kuzuia shimo la panya kwa kipande cha mkate.

#wewantspeace
#wewantsnewconstitutional

#makalioyasufuriahayaogopimoto
 
Naona taratibu mnaanza kukubali matakwa ya wanannchi.

Mtachelewesha tu muda lakini Katiba ni muhimu.
Yapo Mambo mengi ambayo yanachochea uhitaji wa katiba mpya iliyo shirikishi,tuna weza kuwa king'ang'anizi wakakubali wakatuletea rasimu yao kumalizia mchakato ule,tusikibali sisi tunataka maoni yetu yaheshimiwe kwa rasimu ya Warioba.
 
Yapo Mambo mengi ambayo yanachochea uhitaji wa katiba mpya iliyo shirikishi,tuna weza kuwa king'ang'anizi wakakubali wakatuletea rasimu yao kumalizia mchakato ule,tusikibali sisi tunataka maoni yetu yaheshimiwe kwa rasimu ya Warioba.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom