Katiba mpya kutumika uchaguzi 2015, Pia serikali ya Tanganyika kufufuka

the ultimatum

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
401
250
Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya, imeelekeza kipindi cha mpito ambacho pamoja na mambo mengine, kitaandaa mazingira ya Katiba hiyo kutumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

“Kufanya maandalizi na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014 na kufanya maandalizi ya mambo yote muhimu kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 2014,” inasema sehemu ya rasimu hiyo.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia imependekeza kipindi cha mpito cha miaka minne kuanzia tarehe ya kuanza kutumika kwa Katiba Mpya ili sheria zilizopo ziweze kubadilishwa.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alisema jana kwamba katika kipindi hicho cha mpito utakuwa ni muda wa kutungwa kwa Katiba ya Tanganyika. Warioba alisema pia katika kipindi hicho, utakuwa ni muda wa mgawanyo wa rasilimali baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za nchi washirika.

“Katika kipindi hicho pia utakuwa ni muda wa kufanya maandalizi na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 2014,” alisema.

Warioba alisema katika kipindi hicho, Katiba ya Zanzibar itafanyiwa marekebisho ili kuwiana na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2014.

Maoni ya Muungano kutengeneza Katiba ya Tanganyika

Sehemu ya Rasimu ya Katiba ya Muungano, imependekeza kuwa maoni yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, yanaweza kutumika kutengeneza Katiba ya Tanganyika.

SOURCE: MWANANCHI LA LEO TAREHE 31/12/2013
 
Bukwabi

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
3,288
2,000

polepole tutafika kwenye nchi ya maziwa na asali.
 
Sambah

Member
Nov 4, 2008
45
70
Naomba kuuliza nimejaribu kuperuz kwa speed ya mwanga sijaweza kupata mwanga wa kutosha . ina maana kutakuwa na marais watatu??
  1. Rais wa tanganyika
  2. Rais wa zanzibar
  3. Rais wa muungano.
Sasa mbona sijaona kipengele kinachozungumzia uchaguzi wa rais wa tanganyika????isipokuwa alie Rais na wenzake yaani mawaziri manaibu na wale walioainishwa ukomo wa uongozi ni hadi uchaguzi wa 2015. kisha kitakwepo kipindi cha mpito hadi 2018 itakapo kamilika katiba ya tanganyika , vipikwa kipindi chote hicho tanganyika itatumia katiba ya muungano . Haidhuru Ikulu ya rais wa jamhuri itakuwa nchi gani ??? NITAULIZA TENA BAADAE NAENDELEA KUPERUZ KIDOGO
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom