Katiba Mpya kuondoa tatizo la umeme Tanzania ni kwa kuwawajibisha mawaziri kama January Makamba

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
1,900
2,000
Kama taifa letu litapata Katiba mpya basi tatizo la umeme hapa nchini Tanzania litakwisha kabisa. Maana kama tutakuwa na mawaziri mizigo na wazembe wenye harufu za ufisadi basi itakuwa ni suala kuwaondoa kwa nguvu ya umma tu.

Rasimu ya Warioba ilipendekeza Mawaziri wasiwe wanateuliwa kati ya wabunge, bali wawe na mikataba na wakishindwa basi wananchi wanawaondolewa kwa kutotekeleza mikataba ya ajira zao.

Makamba amefeli ndani ya siku 60 lakini CCM inamchekea tu.

Tulisahau mgao wa umeme kabisa.
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,445
2,000
Kufeli kwake sio tija yeye yuko hapo kukamilisha mchezo wa kufosi hati ya dharura ya kukodisha kampuni au mitambo ya uzalishaji ili capacity charges zilipwe na sura yake isio na haya hata kidogo 😅

Magufuli aliwajua sana watu wa hovyo na kutowapa madaraka! Yani huyu jamaa atahakikisha mtake msitake mnalipa capacity charges baada ya kupromote ukame feki😅

Ameshatupiga na kitu kizito kichwani baada ya kufosi kukodisha software ya billion 70 kila mwaka.
 
ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
2,563
2,000
Kufeli kwake sio tija yeye yuko hapo kukamilisha mchezo wa kufosi hati ya dharura ya kukodisha kampuni au mitambo ya uzalishaji ili capacity charges zilipwe na sura yake isio na haya hata kidogo 😅...
Kwasasa wana jeuri sana, ila katiba mpya itapatikana ndani ya miaka minne.

Sababu kubwa hawana uwezo wa kuwasaidia Watanzania Wengi 95% ni wenyewe na maslahi binafsi.

Vyuma vikikaza zaidi kwa sera zao, wengi watazinduka.
 
koro-boy

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
904
1,000
Kama taifa letu litapata Katiba mpya basi tatizo la umeme hapa nchini Tanzania litakwisha kabisa. Maana kama tutakuwa na mawaziri mizigo na wazembe wenye harufu za ufisadi basi itakuwa ni suala kuwaondoa kwa nguvu ya umma tu.

Rasimu ya Warioba ilipendekeza Mawaziri wasiwe wanateuliwa kati ya wabunge, bali wawe na mikataba na wakishindwa basi wananchi wanawaondolewa kwa kutotekeleza mikataba ya ajira zao.

Makamba amefeli ndani ya siku 60 lakini CCM inamchekea tu.

Tulisahau mgao wa umeme kabisa.
Hakuna Katiba itakayoruhusu kuondoa Mawaziri kwa nguvu ya umma hakuna. Maelezo yako yanachembe chembe za udikteta, Katiba pia haitataka viongozi madikteta.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom