Katiba Mpya: Kuna umuhimu wa kutofunganisha uwaziri na ubunge?

everybody

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
337
103
Kwa hali ilivyo sasa hivi uteuzi wa uwaziri unafunganishwa na ubunge kwa maana kwamba ili uwe waziri ni lazima uwe mbunge ( i stand to be corrected). Ila kwa mawazo yangu, hii inazuia watu walio watendaji wazuri wasiingie kuwa mawaziri simply because hawana uwezo wa kuwashawishi wananchi kuwachagua kua wabunge au hawataki kuwa wabunge.

Kwa hali ilivyo sasa hivi, mawaziri wengi wameonekana kuwa na utendaji mbovu wakati kuna watu wenye uwezo tu ambao wangeweza kusimama kuwa mawaziri lakini sio wabunge. Je hamuoni kwamba kuna umuhimu hili swala likafikiriwa katika utengenezaji wa katiba mpya ili wasio wabunge waweze kuchaguliwa kuwa mawaziri?

Nini maoni yenu wa JF?
 
Nikweli naunga mkono hoja kwani inapunguza ufanisi wa Bunge kama sasa kuna wabunge karibu 50 walio kwenye baraza la mawaziri, manaibu, mwanasheria mkuu na wateule wa rais. Inafaa kutenganisha mihimili mitatu kwa dhati, Bunge liwe huru na executive iwe huru, kwani hii ndiyo inayosababisha hata wabunge wa ccm kudhania kuwa wao ni sehemu ya serikali wakati wao ni Bunge
 
Huu mjadala wa katiba mpya lini na wakati bunge linakatika tar26?mkuu sina shaka na hoja yako,nakuunga mikono na vidole vyote 100%
 
hoja yako ni njema mkuu, lakini tulenge katika kupunguza idadi yao pia, kwani tumeshajionea kuwa wingi si utendaji bali mzigo!
 
Kaka, zipo sababu nyingi za kuwa na mawaziri ambao sio wabunge mimi ntachangia hii moja mawaziri walio wabuge hawahofii sana kuukosa uwaziri kwani akiukosa bado ataendelea kuwa mbunge hivyo wanakuwa ni watendaji legelege, hivyo mimi naona kunahaja yakuwa na mawaziri ambao sio wabunge.
 
Nakusupport kwenye hili na pia niongezee tu kwamba kuwa mbungu na kuwa waziri kwa wakati huo huo inaweza kutengeneza upendelea kwa jimbo ambalo waziri anatoka au inaweza kudhoofisha utendaji wa jimbo ambalo waziri anatoka
 
watanzania kwakuwa kote tumeshindwa,sasa kilio,kelele na kila sauti iwe ni katiba mpya tu! Tena tunaitaka 2013! Na kauli mbiu yetu vijana kuanzia sasa iwe No longolongo katiba mpya tu tena sasa!
 
Ni muhimu sana kwenye katiba mpya tukatenganisha kwa vitendo mihimili mikuu ya dola. Baraza la mawaziri lisitokane na wabunge hii inaua kabisa uhuru wa mihili hii miwili. Pia kuwepo na idadi ya wizara. Hakuna ulazima wa kuwa na wizara zaidi ya 15. Hakuna.

Kuna Wizara kadhaa ambazo kabisa zingetakiwa ziwe idara tu na sio fully fledged Ministry. Kama Wizara ya Wizara na hata ile ya Lukuvi. Wanafanya nini hawa? Au kwa mfano Wizara ya Uwekezaji, inafanya nini tofauti na Wizara ya Viwanda na Biashara kama sio kukorogana kimajukumu?
 
mbunge abaki kuwa mbunge.
waziri na katibu waajiriwe na pasiwe na naibu waziri.
na akifanya kazi ni atimuliwe na mwenye uwezo nayo aombe kazi.
 
hiyo ni lazima hakuna haja ya mjadala, lakini sifa zao zijulikane
mmoja hawe mtu asiye na mtuhuma na raisi hasiwe na mamlaka ya kuwafukuza kazi ila bunge
 
Kwa hali ilivyo sasa hivi uteuzi wa uwaziri unafunganishwa na ubunge kwa maana kwamba ili uwe waziri ni lazima uwe mbunge ( i stand to be corrected).
You stand to be corrected?

Mtu anadai Katiba mpya halafu hajui kama hicho anachokidai kina exist au haki exist katika Katiba ya sasa.

Inawezekana tunahitaji zaidi uelewe wa Katiba iliyopo kabla ya Katiba ijayo.
 
Itakuwa vema kama mawaziri wasiwe wabunge vilevile na wabunge wasiwe kwenye board za mashirika ya umma.
Wabunge wetu wengi wanaendesha wizara kisiasa na wanawaziaga hela za kampeni na miradi ya jimboni kwao ili wachaguliwe tena. Sasa hii utakuta waziri anapendelea jimbo lake baada ya nchi nzima.
 
You stand to be corrected?

Mtu anadai Katiba mpya halafu hajui kama hicho anachokidai kina exist au haki exist katika Katiba ya sasa.
Inawezekana tunahitaji zaidi uelewe wa Katiba iliyopo kabla ya Katiba ijayo.

Mkuu ni lazima uelewe kwamba tafsiri yako ya kipengele cha sheria ni tofauti na tafsiri ya mtu mwingine. Hata unapotafsiri mstari kwenye Bible au Quran mwingine anaweza kutafsiri tofauti na unavyosema wewe. So mtu akisema "i stand to be corrected" ina maana mtu mwenye mtazamo tofauti aseme.
 
Waheshimiwa tatizo hili la Jairo ni kwamba tutafute ufumbuzi wa kudumu kwa kuundw kwa KATIBA MPYA na madaraka makubwa kupindukia Rais zipunguzwe mara moja; kwani nini ikulu ifike mahala inatutapikia ovyo kiasi hikii????????????????

Back
Top Bottom