Tukubali kuziweka siasa pembeni. Kama ilivyo kwa mwenda kuoga, tukubali kuyavulia maji nguo, tuukabili ukweli usiosemeka:
1. Ridhaa ya kuongoza nchi hupatikana kutoka kwa wananchi.
2. Haiwezekani popote kuwa ridhaa hiyo ikatolewa kwa mtu ambaye agenda zake hakuna kuheshimu usawa, uhuru wala haki.
3. Wapo walioingia madarakani pasipokuwa na ridhaa za wananchi wao. Wakitumia mitutu ya bunduki, wizi, ghiliba na hata hadaa.
Kutegemeana na walivyoingia madarakani nchi moja hufanana na nyingine au hata kutofautiana wazi wazi.
A: Tanzania, Burundi, Rwanda, Uganda, Zimbabwe zina kufanana kwingi kwenye nyanja nyingi za kiutawala. Kwenye nchi hizi mihimili ya utawala haiko huru na kote upo mmoja uliojichimbia zaidi.
Matokeo yake, harakati za wazi za watu wasiojulikana, tuhuma za ugaidi kwa wapinzani, malalamiko ya kuminywa demokrasia, na vyote vya namna hiyo, huko ndiyo kwao.
Katika nchi hizi watu kupotea, kutekwa na kuuwawa vidole vikielekezewa dola ndiyo maisha yenyewe.
Kama tunavyo waulizia kina Moses Lijenje, kwenye nchi za kwenye kundi hili nako ni hivyo hivyo.
Waliingia bila ridhaa ya wananchi hawataondoka kwa maamuzi ya wananchi.
Alisema Museveni kwa nyundo kama quarter pin ya baiskeli aliingia na ndivyo atakavyotoka.
B:. Kenya, Malawi, Zambia, Afrika Kusini; mihimili yaani serikali, bunge na mahakama iko huru na kila mmoja unatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa katiba.
Haipo mivutano ya dola na wapinzani. Hazipo harakati za wasiojulikana na maisha yanasonga kwa amani pasipo na matumizi ya nguvu kuwanyamazisha wenye mawazo tofauti kisiasa.
Hawa waliingia kwa ridhaa za wananchi, watatoka kwa maamuzi wananchi.
Hatustahili kuwa katika kundi lenye viongozi wasiokuwa chaguo letu.
Hatustahili kuwa kwenye kundi ambalo leo wako kwenye kujipangia nafasi za uongozi 2025 bila ridhaa zetu.
Tunauhuru wa kuchagua hali hii kuendelea au kukataa.
Uamuzi ni wetu.