Katiba mpya Kenya sasa kizungumkuti: Ushoga ni rukhsa.............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya Kenya sasa kizungumkuti: Ushoga ni rukhsa..............

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Rutashubanyuma, Oct 23, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Rasimu za katiba ya kenya zilizokuwa zikijulikana kama "Boma" na "Wako" ya mwaka 2005 zilikuwa wazi ya kuwa ushoga hapana lakini hii katiba mpya hiyo Ibara iliondolewa na hivyo kuhalalisha ushoga............

  Kwenye rasimu ya "Boma" Ibara ya 41(3) na kwenye "Wako" Ibara ya 42(3) ushoga ulikuwa wazi kabisa umepigwa marufuku.

  Baada ya katiba mpya kuondolewa Ibara inayokataza ushoga zipo ibara nyingine kwenye katiba hiyo ambazo zinalinda ushoga bila kuutaja moja kwa moja............Ibara 27(4) inakataza ubaguzi wa aina wowote ule hata ule wa "sex" na wala siyo jinsia tu kwa maana ya "gender" Hii imetafsiriwa na magwiji wa sheria huko Kenya ya kuwa "sex" inajumuisha ushoga........

  Ibara 20(3) ya katiba mpya inatoa mamlaka kwa mahakama kutoa matamko ya kulinda haki za wanyonge ambao wamekuwa wakidhulumia haki zao. Hivyo kama kuna utata wowote ule mashoga Kenya wanaweza kwenda mahakamani ili kuziweka bayana haki ambazo walipewa na katiba mpya. Kwao itakuwa ni rahisi sana kuzitetea kwa sababu watakachokifanya ni kuiomba mahakama kutoa tamko kuwa haki za mashoga zinalindwa na katiba na kama waasisi wa katiba mpya wangelikuwa hawataki kuzilinda wangelifanya hivyo na kwa uwazi kabisa kama ilivyokuwa kwenye rasimu za "Boma" na "Wako"..........Hii ni hoja ya shoka na siyo rahisi kuitengua........

  Mara mahakama itakapotoa tamko tajwa basi kuwanyanyapaa au kuwabughudhi mashoga waweza kujikuta unafikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 20(3) na matamko hayo ya kimahakama kuwa na nguvu sawasawa na sheria zozote zilizotungwa na Bunge lao........


  Ibara 19(3) imeweka wazi ya kuwa haki za uraia zilizomo kwenye katiba pia inajumuisha haki nyinginezo zozote zile ambazo hazikutajwa bayana kwenye katiba hiyo na kutoa mwanya mwingine wa kisheria kwa mashoga kupasua anga bila zengwe lolote lile.......

  Wapo ambao watasema hivi ni kwa nini basi waasisi wa katiba mpya walizilinda haki za mashoga kimya kimya na kwa nini hawakuweka ulinzi huo wazi kabisa kuondoa utata unaoweza kujitokeza kisheria?

  Maoni yangu ni kuwa kutokana na mashinikizo ya waumini wa madhehebu mbalimbali kuwa na mapingamizi makali dhidi ya ushoga waliona hili suala walichimbie ulaini wa kimya kimya tu..................lakini ndani ya katiba ya Kenya lolote ambalo katiba haijalikataza laweza kuundiwa sheria na kuwa rukhsa kishera.......Go Kenyan gays and lesbians an be our drag queens and kings.........Best wishes in you newfound freedoms but I do not know whether you deserve them.............
   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ushoga au Usenge?. Naona tunapotosha hapa. Kitendo cha Mwanaume kuingiliwa na mwanamme mwenzake kwenye njia kubwa ya choo kwa hiari yake kinaitwa USENGE na sio USHOGA. Ushoga ni urafiki wa kawaida kati na akina mama/dada.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Oct 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama kuna mtu ana soft copy ya Katiba ya Kenya naomba atuwekee hapa tuijadili!
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Oct 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Siku hizi usenge na ushoga ni kitu kile kile, usipotoshe!
   
 5. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushoga ni wanawake wanavyojiita marafiki na kama mtu anavyoweza kujiita mshikaji na rafiki yake wa kiume yaani wote wakiwa wanume wanaitwa washkaji wakiwa wanawawke wanajiita mashoga. Kukitokea watu wanapigana miti basi wataitwa ******* not other wise hicho ndicho kiswahili nilichofundishwa na mwalimu wangu wa lugha ya kiswahili aliyemaliza pale mlimani mwaka 1989. Labda yeye kiswahili hicho kilikuwa hakijahakikiwa na TUKI au?
   
 6. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Rutaaaaaaaaaaaaaa nakuona kaka............
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Soft copy haipatikani? Maana sipendi kujadili bila kuwa na uhakika kama mtoa hoja haja-misquote au haja-misinterpret!
   
Loading...