Katiba mpya katiba mpya. Je inatakiwa iweje?

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Wanajamvi na wataaalamu
.
Wanasiasa, wanasheria na watu wengi hivi sasa kilio chetu ni katiba mpya. Wengi tuna refelct mapungufu ya NEC kama pungufu mojawapo la katiba ya sasa.Naomba kuelimishwa juu ya mambo mengine

Naomba tujadili kwa details ni mambo gani mengine tunaona katiba mpya itacover ambayo katika kaiba tuliyonayo sasa kuna mapungufu

Nawasilisha
 
Wanajamvi na wataaalamu
.
Wanasiasa, wanasheria na watu wengi hivi sasa kilio chetu ni katiba mpya. Wengi tuna refelct mapungufu ya NEC kama pungufu mojawapo la katiba ya sasa.Naomba kuelimishwa juu ya mambo mengine

Naomba tujadili kwa details ni mambo gani mengine tunaona katiba mpya itacover ambayo katika kaiba tuliyonayo sasa kuna mapungufu

Nawasilisha

Mtazamaji,
Ukipata nafasi soma ilani za uchaguzi 2010 za vyama vya upinzani mf. CHADEMA na NCCR-Mageuzi. Utaona mapungufu ya katiba ya sasa kwa mujibu wa vyama hivyo, na ni mambo gani wanapendekeza katiba mpya iwe nayo. kama hutaweza kupata ilani hizo, niambie nitatafuta copies (za kurasa husika) na kuzipachika hapa. Kwa sasa nakala zangu haziko karibu.
Ila miongoni mwa mapungufu ya katiba ya sasa, ni kwamba haina kifungu kinachotamka utaifa wetu (haitutaji sisi watanzania), inalilazimisha taifa zima kufuata itikadi ya ccm (ujamaa na kujitegemea), haikutungwa na chombo kinachotakiwa kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya sheria (yaani bunge/baraza la katiba)
 
Mtazamaji,
Ukipata nafasi soma ilani za uchaguzi 2010 za vyama vya upinzani mf. CHADEMA na NCCR-Mageuzi. Utaona mapungufu ya katiba ya sasa kwa mujibu wa vyama hivyo, na ni mambo gani wanapendekeza katiba mpya iwe nayo. kama hutaweza kupata ilani hizo, niambie nitatafuta copies (za kurasa husika) na kuzipachika hapa. Kwa sasa nakala zangu haziko karibu.
Ila miongoni mwa mapungufu ya katiba ya sasa, ni kwamba haina kifungu kinachotamka utaifa wetu (haitutaji sisi watanzania), inalilazimisha taifa zima kufuata itikadi ya ccm (ujamaa na kujitegemea), haikutungwa na chombo kinachotakiwa kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya sheria (yaani bunge/baraza la katiba)

Waridi thank you.
lakini unaweza kunipa japo hints za hayo mapendekezo ni vipengele gani zaidi vinavyotakiwa kuwa Hja za kujadiliwa

So far vyama vya siasa vimeongelea uteuzi na undeshaji wa vyombo mbali mbali Kama NEC,Polisi etc kuwa vinapendelea serikalaki inayokuwepo madarakani. Mfano
- Uteuzi wa wa watendaji wa vyombo kama Polisi NEC, Majaji etc
- Madaraka ya rais

Je hakuna zaidi ya mabadiliko haya yanayotakiwa. ?
 
Kutoka Ilani ya NCCR-Mageuzi 2010, uk. 8-11
4.0 AJENDA ZETU KATIKA UCHAGUZI WA 2010

4.1 AJENDA ZA KIUTAWALA

4.1.1 KATIBA MPYA
Katiba ya nchi ndiyo sheria kuu ya nchi. Sera za Serikali na Sheria za nchi lazima zitokane na kufungamana na katiba ya nchi. Kama taifa lina katiba mbaya isiyolinda haki za wananchi, basi sheria na mfumo wa utoaji wa haki utakuwa mbaya na usiotenda haki. Kama katiba ya nchi na sheria zake havilindi haki, basi watendaji wa vyombo vya dola hawatatenda haki kwa kuwa haki haipo kisheria.

Pia, Taifa ambalo katiba yake ni mali ya viongozi, kwa maana kwamba imetungwa na viongozi kwa ajili ya kujiweka madarakani na kulinda masilahi yao, halina demokrasia ya kweli. Katiba ya Tanzania ni ya aina hiyo, Ni katiba iliyotungwa na viongozi kupitia Bunge Jamhuri. Sote tutatambua kuwa kwa mujibu wa taaluma ya katiba, Bunge ni chombo cha kutunga sheria za kawaida za nchi lakini si chombo cha kutunga katiba. Katiba ya nchi hutungwa na Baraza la Taifa la Kutunga katiba.

Chama cha NCCR – Mageuzi kinatambua ukweli kwamba baraza la Taifa la Kutunga Katiba ndicho chombo halali cha kutunga katiba ya nchi. Chama chetu kinatambua pia kuwa tangu Taifa letu kuundwa, hatujawa na chombo hiki kwa mujibu wa katiba na sheria zetu za nchi.

Baraza la Taifa la Kutunga Katiba hujumuisha wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, na wawakilishi wa sekta muhimu, vyama vya siasa, taasisi za kijamii, mashirika ya dini, vyama vya wafanyakazi, wakulima, taasisi mbalimbali za serikali na kadhalika.

Chama cha NCCR-mageuzi kitahakikisha kuwa Baraza la Taifa la Kutunga Katiba litaundwa na litatekeleza mchakato wa kutungwa katiba mpya. Kwa mujibu wa mageuzi haya, lengo letu ni kuwa na katiba mpya ya nchi itakayofanya mambo yafuatavyo:

i) Itaainisha misingi na maadili ya utaifa kutokana na muafaka wa kitaifa, misingi ambayo itadumisha haki, maelewano, amani na umoja.
ii) Itaweka mfumo mpya wa uchaguzi utakaowawezesha wananchi kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi huru na wa haki. Mfumo huo utaanzisha uwakilishi wa uwiano sambamba na uwakilishi wa majimbo ulioko hivi sasa.
iii)Itaamuru kuwepo na tume huru ya uchaguzi na itaweka masharti ya uundwaji wake;
iv) Italiamuru Bunge la Jamhuri kutunga sheria mpya ya uchaguzi inayoweka mazingira huru na sawa kwa wote kushiriki na kushindana katika uwanja ulio sawa.
v) Itaweka misingi ya mgawano wa mamlaka katika mihimili ya dola itakayoondoa utaratibu wa hivi sasa wa mihimili hii kuingiliana katika utendaji wa wajukumu yake na itaondoa utaratibu usiofaa wa kuwapa watumishi wa mihimili hii kofia zaidi ya moja, matharani mbunge kuwa pia waziri au mkuu wa mkoa, jaji kuwa mwenyekiti wa Tume ya serikali, na kadhalika.
vi) Itaweka usawa wa kijinsia katika kutekeleza mfumo mpya wa uchaguzi.
vii) Itatangaza rasmi utaifa wa Watanzania, kuweka vigezo vya uraia na kutaja wazi haki ya kila raia kupewa kitambulisho cha uraia.
viii) Itaanzisha mahakama ya kudumu ya katiba itakayopokea na kusikiliza masharti ya kikatiba, raia binafsi au taasisi.
ix) Italipa bunge nguvu ya kuwa chombo cha kutetea maslahi ya wananchi na kuwa na uamuzi wa mwisho katika utungaji wa sheria, uridhiaji ya mikataba na kuwa na mamlaka ya kupitisha au kukataa uteuzi wa viongozi muhimu wa dola.
x) Itaainisha wizara na idadi ya kudumu ya wizara za Jamhuri ya Muungano.
xi) Itapunguza baadhi ya madaraka ya rais kwa kuyaweka kwenye vyombo vingine vya maamuzi.
xii) Italinda haki ya raia wa Jamhuri ya Muungano kumiliki ardhi na kulipwa fidia ya haki inayoendana na bei za soko ardhi inapochukuliwa na serikali kwa miradi ya umma.
xiii) Itaweka muundo wa muungano wenye dola la shirikisho baina ya Tanganyika na Zanzibar.
xiv) Itaainisha haki za binadamu kwa viwango vinavyokubalika kimataifa ikizingatia utu wa mwafrika na utamaduni wake.
xv) Itaruhusu wagombea huru wa nafasi za uongozi (udiwani, ubunge, na urais).
xvi) Itatambua sekta ya habari kama muhimili muhimu wa demokrasia yetu na kuliamuru Bunge litunge sheria ya kulinda uhuru wa vyombo vya habari na haki ya raia kupata, kutumia na kutuma habari;
xvii) Itaimarisha uhuru wa mahakama na kuamuru Bunge litunge sheria itakayorahisisha utoaji na upatikanaji wa haki kwenye vyombo vya maamuzi nchini;
xviii) Itahakikisha kuwa ardhi na maliasili vinaendelezwa, vinamilikiwa na vinawanufaisha Watanzania.
 
Ilani ya CHADEMA 2010 uk.56-59
6.4 CHADEMA itafanya nini katika kujenga uongozi bora na kuimarisha utawala wa sheria?
6.4.1 Ili kuimarisha kujenga uongozi na kuimarisha utawala bora na utawala sheria, Serikali ya CHADEMA itachukua hatua zifuatazo:

i) CHADEMA inatambua kwamba nguvu ya utawala bora ni KATIBA ya nchi iliyojengwa katika misingi ya kulinda demokrasia, kulinda haki za wananchi na kutoa fursa kwa wananchi hao kuwawajibisha viongozi wao. Katiba yetu ya sasa haikujengwa katika misingi hii. Kwa sababu hii, hatua ya kwanza itakayochukuliwa na CHADEMA ndani ya siku 90 tangu kuchaguliwa kwake ni kuanzisha mara moja mchakato wa kubadilisha katiba ili hatimaye tupate katiba ambayo imejengwa katika misingi ya kidemokrasia na haki za binadamu. Lengo ni kuhakikisha kuwa inapofika uchaguzi mkuu mpya wa 2015, Tanzania inafanya uchaguzi huo chini ya Katiba mpya ambayo, pamoja na mambo mengine,

itakaweka mgawanyo thabiti wa madaraka baina ya Bunge, Serikali na Mahakama.


ii) Ili kupunguza gharama za utawala na kutoa madaraka na mamlaka katika ngazi za chini, Serikali ya CHADEMA itapunguza ukubwa wa serikali kuu na kuimarisha madaraka katika ngazi za halmashauri ya Wilaya. Wizara za Serikali zitatamkwa kwenye Katiba ya nchi ili kuondoa mwanya wa Rais kubadilisha wizara kila anapojisikia kufanya hivyo. Tutafuta vyeo vya wakuu wa wilaya na kuimarisha mamlaka katika ngazi ya Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji. Tutaanzisha mchakato wa kupeleka madaraka makubwa ya kiutendaji na kiutawala mikoani ili kuchochea maendeleo.

iii) Ili kukabiliana na wimbi la ufisadi miongoni mwa viongozi wa kisiasa na watumishi wa umma, Serikali ya CHADEMA itafanyia mabadiliko ya haraka sheria ya Maadili ya Umma ili hatimaye watumishi wote wa Umma wakumbushwe kuwa wako katika utumishi wa umma. Katika sheria hii adhabu kali zitawekwa ili kuhakikisha kuwa watumishi wa umma hawatumii vyeo na nafasi zao vibaya ili kujinufaisha wao au watu wa karibu yao. Sheria hii itakuwa tayari kwenye Bunge la Kwanza litakalokuwa chini ya CHADEMA.

iv) Ili kuimarisha utendaji wa Tasasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Serikali ya CHADEMA itaiondoa taasisi kutoka ofisi ya Rais na kuifanya huru chini ya Katiba. Pamoja na kwamba Rais atamteua Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, uteuzi wake hautakamiliki hadi utakapojadiliwa na kuthibitishwa na Bunge. Aidha ukomo wa utumishi wa Mkurugenzi wa TAKUKURU utakuwa kwa mujibu wa Katiba, na sio matakwa na utashi wa Rais. Kwa maneno mengine Mkurugenzi wa TAKUKURU hatoweza kuondolewa na Rais isipokuwa kwa utaratibu uliowekwa wazi kisheria.
v) Viongozi wate wa kisiasa na watumishi wa umma ambao walishabainishwa kujihusisha na ufisadi na ubadhirifu (rejea orodha ya mafisadi) ya umma lakini Serikali ya CCM imeshindwa kuwafikisha mahakamani kwa kuwa ni washiriki, watafikishwa mahakamani ndani ya siku 180 chini ya Sheria ya Kuzuia Mitandao ya Uhalifu na Uhujumu Uchumi ya 1984 pamoja na Sheria nyingine zozote ambazo zitaonekana zimevunjwa. Wale watakaothibitika mahakamani kuhusika na vitendo vya ufisadi, pamoja na kuadhibiwa na mahakama, mali zao zitataifishwa na kurudishwa serikalini. Katika hili viongozi waliopita (wakiwemo Marais) ambao wataonekana kuhusika na vitendo vyovyote vya ufisadi au uvunjaji wa sheria watavuliwa kinga zao na Bunge ili hatimaye waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao yatakayoletwa na Taifa lao. Hakutakuwa na kiongozi ambaye hatoweza kufikishwa mahakamani kama amefanya vitendo vya uhalifu akiwa madarakani.

vi) Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kifisadi miongoni mwa viongozi wa kisiasa na watumishi wa umma hapa nchini, na kwa kuzingatia uwezo mdogo wa mahakama zetu katika kushughukikia kesi zinazohusu ufisadi, Serikali ya CHADEMA itafanya uteuzi wa kutosha wa Majaji wa Mahakama Kuu ili baadhi yao wakae kama Mahakama ya Hujuma ya Uchumi kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Mitandao ya Uhalifu na Uhujumu Uchumi ya 1984. Lengo ni kuhakikisha kuwa kesi zote kubwa za ufisadi zinashughulikiwa kwa haraka bila kuingilia utendaji wa mahakama katika kesi zinazohusu makosa mengine.

vii) Ili kujenga moyo wa kuheshimu maadili katika ajira na kazi mbalimbali vyuo vikuu nchini vitatakiwa katika masomo yake ya msingi kuwepo na masomo ya mambo ya maadili na miiko (morality and ethics). Katika ngazi za chini za elimu masomo yenye kuchochea uzalendo yatatolewa kama sehemu ya elimu ya Uraia.

viii) Kwa kuwa vijana ndio kundi kubwa hapa nchini, na kwa kuwa uhai wa muda mrefu wa taifa letu upo mikononi mwa vijana, Serikali ya CHADEMA itawezesha vijana kuunda Baraza la Vijana (BAVITA) ambalo limekwamishwa na Serikali ya CCM kwa muda mrefu. Baraza hili litakuwa na jukumu la kuwaunganisha vijana wote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa au dini zao. Baraza hili pia litawezeshwa ili ndio liwe tanuru la kupika viongozi wa nchi. Jukumu la Baraza hilo litakuwa pia kama chombo cha mijadala na mafunzo mbalimbali ya vijana nchini na kusimamia ujirani mwema, umoja na ushirikiano katika utendaji wa mambo mbalimbali.

ix) Ili kuwawezesha wanawake kuunganisha nguvu zao bila kujali itikadi zao za kisiasa, Serikali ya CHADEMA itaruhusu na kufanikisha kuanzishwa kwa Baraza la Wanawake Tanzania. Baraza hili litakuwa chombo huru cha kutetea maslahi ya wanawake wote na wasichana nchini.
 
Waridi thanks tena. So nimeona NCCR wamejitahidi kuonyesha issue ambazo zinatakiwa kuwa hoja kwenye mijadala ya katiba mpya. Nazo ni

  1. Mfumo mpya wa uchaguzi
  2. Mgawano ma mamlaka na madaraka kwenye mihimili mitatu ya dola
  3. Usawa wa kijinsia
  4. Uraia wa Haki na wajibu wa mtazania.
  5. Nguvu ya bunge
  6. Muundo wa serikali
Muundo mfumo na uteuzi wa viongozi na wajumbe wa tume ya uchaguzi hili sidhani kama linamjadala lbda kwa chama kilichpo madrakani kinaweza kujifanya haioni tatizo . Hapa kuna tatizo

Madaraka ,wajibu na mipaka kati ya mahakama bunge na serikali nayo ni hoja nzito. Hata protocal ya madaraka within chombo kimoja inachanganya. Mfano ndani ya bunge katibu wa bunge ana madaraka kiasi gani. Kuna mada nimeona imeadikw hapa ikohoji nafasi ya Waziri mkuu wa tanzania katika muungano.

NCCR wamejaribu kutaja usawa wa kijinsia . Wasi wasi wangu hapa ni tikiruhusu kuongelea usawa wa kijinsia basi itabidi turuhusu kuongelea usawa wa kidini kikabila , ki age group, na hata dissabilities. Nadhani Katiba isitize kutobagua na tuusinge wenye mtego wa katiba kutaja kundi fulani la jamiii.

Ngoja niishie hapa. kwanza. Je nyie wajumbe mnataka kuona mabadiliko ya vitu specifically gani kwenye katiba.
 
Katiba mpya ni haki ya waTZ. It is time now that we need a new and wholistic constitution. The one party constitution must be burnt to ashes!
Ahahaaa! Mnyalu
 
itakuwaje nchi ya vyama vingi iongozwe na katiba ya chama kimoja kweli hapo yatakosa mapungufu
 
Back
Top Bottom