Katiba Mpya, JK kuandika Historia !!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya, JK kuandika Historia !!!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Goodrich, Mar 2, 2012.

 1. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Endapo Mh. Rais Jakaya Kikwete atafanikisha mchakato wa kuandaa Katiba Mpya, na ikapatikana Katiba nzuri na muafaka wakati huu wa kipindi chake, basi atakuwa amejiwekea hazina (Legacy) itakayokumbukwa vizazi kwa vizazi. Pata picha mwaka 2085 wajukuu wakiongozwa na katiba nzuri tuliyoandaa, pengine itawafanya kuwa taifa lenye nguvu.
  Nadhani sifa za katiba nzuri, Mh Rais azijue ni pamoja na:

  1. Kukubalika na wananchi bila kuacha manunguniko ya msingi. i.e kuzingatia mapendekezo ya msingi
  2. Kupingwa na watu wanaonufaika na mifumo dhaifu. i.e Katiba nzuri lazima itapingwa na watu wanaonufaika na mifumo mibovu/dhaifu.
  3. Kutenganisha kabisa mihimili mitatu, yaani Bunge, Mahakama na Serikali. i.e Muhimili mmoja usiwe juu ya mwingine, wala kuteua kiongozi wa muhimili mwingine.

  Mimi naamini kwa nia aliyoonyesha Rais wetu, kwa hili anaweza. Nadhani kwa sasa haangalii watu wanaomzunguka ambao wengi wao wananufaika na hii mifumo dhaifu. Nadhani Rais wetu kwa suala la Katiba anaangalia miaka 100 mbele.

  Kwa hili, Hongera JK !
   
 2. G

  Gamba la Chuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,247
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa. JK anajitahidi sana. Ila tatizo ni hao magamba wanaomzunguka. Wameshampotosha katika mambo mengi. Lakini akiwa na msimamo kwa hili anaweza kujiwekea historia !
   
 3. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  La muhimu kabisa ni Kutenganisha kabisa mihimili mitatu, yaani Bunge, Mahakama na Serikali. i.e Muhimili mmoja usiwe juu ya mwingine, wala kuteua kiongozi wa muhimili mwingine.
  Kila muhimili uwe na mfumo wake wa kujiendesha wenyewe.
   
 4. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280

  Kama kiongozi wa nchi inatakiwa awe na misimamo yake yenye manufaa kwa taifa !!!
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani historia itakuwa imewekwa na CDM kwa kumshinikiza JK na serikali yake kuandika katiba mpya. Kama huu ungekuwa ni utashi wa Jk na chama chake wasingeacha kuliweka suala hili katika ilani yao ya uchaguzi. Ni vema tukaepuka kumpa sifa mtu ambaye ame-copy na ku-paste.
   
 6. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280

  Natofautiana na JK katika mengi. Lakini kwa hili endapo atafanikisha mchakato huu, ni wazi kuwa atakuwa na legacy to be proud of
   
 7. m

  mishalejuu Senior Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mihimili independent mitatu? najua wengi mnayatoa haya myanenayo kanisani katika ile doc yenye mapendekezo ya kanisa. kama rais inatakiwa awe na veto kwa mambo muhimu ili kuweza uwa na governence power. hakuna reference ya nchi iliyokuwa na style hiyo ya mihimili halafu ikatawalika. NO. tunaelekea kubaya
   
 8. G

  Gamba la Chuma JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2014
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,247
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nchi haipaswi kutawalika bali kuongozwa kwa misingi wanayotaka wananchi.
   
Loading...