Katiba Mpya: JK anaogopa yai la Muungano kumpasukia mikononi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya: JK anaogopa yai la Muungano kumpasukia mikononi??

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mr. Zero, Mar 18, 2011.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Ni takiribani miezi minne tangu Rais atuahidi katiba mpya. Kwa jinsi kimya kilivyo inaelekea mwaka utaisha hatujasikia kitu.

  Zanzibar washaanza kujipanga namna ya kuchangia kwenye katiba kupitia Zanzibar legal society, chama cha waandishi wa habari n.k.

  Kwa jinsi upepo ulivyo inaelekea Wazanzibar hawako tayari kuwa na muungano wa design ya 1964. Kama watafanikiwa kwa hilo kuna kila dalili za Tanganyika kurudi......!!

  Je JK ansoma upepo wa siasa za Tanzania ...............ili yai la Muungano lisimpasukie mikonono au?

  Kuna wakati watu waliandika humu kuwa JK kasema hatakubali CCM au Muungano vifie mikononi mwake.

  Anyway, swali ni kwamba je mchakato wa katiba utaanza lini?? Au ndiyo SUBIRA YAVUTA HERI???
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  tatizo watu na waandishi masikio loliondo, wamesahau mambo mengine ya msingi hasa katiba
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mimi naogopa hizi habari za Loliondo zisije zikawa zimepikwa ili kuwafanya wananchi wa concentrate kwa mambo ya kikombe waachane na Dowans pamoja na Katiba. Tuwe macho
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Akirudisha Tanganyika , atapooza moto kidogo, la sivyo yai litapasuka tu.:drum:
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Kwa maoni yangu huwezi kuzungumzia Katiba mpya ya Muungano bila ya kuzungumzia Muungano wenyewe.

  Kama Watanzania tuko makini basi tungeanza na mjadala wa Muungano na Muundo wake na uendeshaji wake kwanza kwa sababu Katiba ya Muungano inatakiwa isisuguane na Katiba za nchi wanachama wa Muungano.

  Kwa usiri mkubwa uliougubika muungano leo nchi moja mwanachama wa Muungano haonekani na katiba yake pia imepotezwa. Jambo la lazima limejitokeza, kuiandika upya Katiba ya Muungano. Wako wapi wawakilishi halali wa nchi mbili za Muungano wa Tanzania(Tanganyika na Zanzibar). mambo ni mkorogo tu, hata mkorogo ule wa "mchina" una afadhali.

  Inawezekana kabisa Muungano ni jinamizi linaloisumbua serikali ya Muungano kwa sababu hapo nyuma wamejinyakulia mamlaka kienyeji bila ya majadiliano kama yale yaliyofanyika wakati wa kuunda Muungano wenyewe.

  Kwa hiyo, Nionavyo mimi ni kuwa Zaznibar wanafanya jambo zuri sana kujitayarisha kama wananchi wa upande mmoja wa Muungano ili waweze kuchangia kile wanachokitaka kiwemo katika katiba ya Muungano.

  Ingekuwa jambo la busara pia wananchi wa Tanganyika(Tanzania bara) pia kujitayarisha kama wananchi wa upande mwengine wa Muungano ili tuweze kuchangia kile ambacho tunakitaka kiwemo ndani ya Katiba mpya ya Muungano.

  Lakini la muhimu zaidi pia tujitayarishe kuifufua katiba ya Tanganyika ili iwepo sambamba na Katiba ya Muungano na katiba ya Zanzibar. Kuna mambo ya Tanganyika(Tanzania bara) yaongozwe na katiba yake. Kuna Mambo ya Muungano yaongozwe kwa Katiba yake na Zanzibar wanayo katiba yao inayoongoza mambo ya Zanzibar.Hizi ni mamlaka tatu tofauti.

  Kwa kutaka kwetu na kupenda kwetu njia za mkato ndio zinatuletea ugumu usio wa lazima. na kufanya uwepo Muungano usieleweka. na iwepo nchi ya kiini macho na mazingaombwe.
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  my great worry/doubt ni ikiwa kweli mh presidaa alivosema anaanzisha mchakato wa katiba mpya ili tunaposherekea miaka 50 ya uhuru december tuwe na kitu kipya (katiba) alikuwa anamaanisha real au ilikuwa tu ni kutuliza upepo uliokuwa mkali sana kipindi kile. sioni any developments and days are rushing. pengine tatizo la mtu asiekuwa serious with what he/she always speaks.
   
 7. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tatizo la JK ni kuogopa kufanya maamuzi magumu, na hili litamgharimu sana. Pia kumbukeni katibu wa bunge alisema hoja binafsi ya Mnyika imetupiliwa mbali kwa sababu hakuna kifungu katika katiba ya sasa kinachoruhusu katiba ya sasa kujadiliwa kwa kubadilishwa! kwa hivyo si Bunge si serikali wala mahakama vyenye uwezo wa kubadilika au kujadili kubadilishwa kwa katiba! Huu ni upuuzi mkubwa. Lazima kuwa na Bunge la Katiba siyo hili la akina Makinda na mabosi wake mafisadi ambalo litakuwa na nguvu kisheria kujadili au kubadili katiba
   
 8. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe, ila hiyo katiba ya kwetu Tanganyika ipoo ama walishaichakachulia mbali kama siyo kufilisi kabisa?
   
 9. F

  Falconer JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Asanteni wachangiyaji wa mada hii. Kwa ufupi, muungano ilikuwa ni kiini macho. Kulingana na sisi wazanzibari tumegundua kuwa hakuna muungano kisheria. Jambo lilioko ni utawala wakimabavu dhidi ya wazanzibari. Nahisi, Bw. J.K. haogopi muungano kuvunjika. Kitu kinacho mtia wasiwasi ni namna ya kuwaeleza watanganyika jinsi Raisi Nyerere alivo boronga mambo. Kwetu sisi, Nyerere hajawa "biggie" sababu tunamchukulia kama kiongozi alietuhujumu. VP Jk amlaumu Nyerere?. Hilo ndio suala la kujibiwa. Kama muungano utaendelea, basi, utaendela ki mabavu. Public Opinion z'bar ni kuwa 90% hawautaki muungano. Huu ndio uhakika wa wazanzibari. Kama uhalali wa muungano haupo, tunajadili katiba ya muungano ya nini?.
   
Loading...