Katiba Mpya : Jee huku ni kutokufahamu ama ni Makusudi?


GHIBUU

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Messages
3,887
Points
2,000
GHIBUU

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2011
3,887 2,000
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Agostino Ramadhani akizungumzia mwelekeo wa utoaji maoni kuhusu Katiba Mpya unavyoendelea Zanzibar amekaririwa na gazeti la ZANZIBAR LEO akisema “anashangazwa na wengi wanaopewa nafasi ya kutoa maoni yao katika mchakato huo wamekuwa wakizungumzia zaidi mfumo wa Muungano wakati kukiwa na maeneo mengi ambayo wananchi wa Zanzibar wanaweza kuyatumia kama sehemu ya kuainisha mahitaji yao katika misingi ya katiba mpya. Akiyataja maeneo hayo alisema kuna masuala ya ardhi na kero za wawekezaji kwa kuielekeza serikali namna ya kuzifanyia kazi kwa misingi ya Katiba kutokana na hivi sasa bado wananchi wamekuwa wakilipigia kelele eneo hilo.”
Najiuliza hivi Jaji Ramadhani ambaye ni mwanasheria aliyefikia nafasi ya kuwa Jaji Mkuu hajui kuwa maeneo ya ardhi na kero za wawekezaji hayamo katika masuala ya Muungano na katika maeneo hayo Wazanzibari wanatawaliwa na Katiba ya Zanzibar na siyo Katiba ya Muungano? Vipi alitegemea Wazanzibari watoe maoni kuhusu mambo hayo kupitia mjadala wa Katiba ya Muungano?
Kioja kama hiki alikizua Mwenyekiti wa Tume hiyo ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (na huyu naye ni mwanasheria na Jaji) pale alipokwenda kufuatilia utoaji wa maoni kisiwani Pemba akasema anashangaa alikuwepo Tanga na wananchi wakawa wanatoa maoni kuhusu elimu na walimu, lakini Pemba hawazungumzii hayo na badala yake wanazungumzia Muungano tu. Alitushangaza maana kwa mtu wa hadhi na elimu yake alipaswa kujua kujua kuwa elimu na walimu si mambo ya Muungano.
Kinachoonekana ni kuwa maoni ya Wazanzibari kuhusu Muungano yanawatia kiwewe Joseph Warioba na Agostino Ramadhani. Wanachopaswa kukifahamu ni kwamba katika suala la Muungano, Wazanzibari hawatarudi nyuma katika kusimamia wanachokiamini. Ni vyema Warioba na Agostino wakapata nafasi ya kumsikiliza Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Amani Karume, hotuba yake ya Kizota ili wapate darasa la uvumilivu kwa wenye mawazo tofauti na yao na waache kuwapotosha Wazanzibari kwa kuwataka watoe maoni kwa mambo yasiyowahusu kwenye Katiba ya Muungano.
 
M

Mandi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Messages
385
Points
0
M

Mandi

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2011
385 0
kwa zanzibar muungano ndo adui maisha yalikuwa poa kabla 1964 lakini baada ya 64 hayakuwa poa ni balaa tu.say no union
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Points
2,000
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,000
Sioni kosa hapo, katba ya jamhuri inabadilishwa na watu wakipenda wanaweza pendekeza chochote ktk jamhuri ya muungano wa Tanzania.Wazanzibar wasilete kichaa kutengeneza katiba kwa kutumia katiba yao ya kichwani.

Katiba inayowekewa mipka hivi itakuwa na mipaka au mapungufu wakati wa utendaji pia.
 

Forum statistics

Threads 1,295,165
Members 498,180
Posts 31,202,051
Top