Katiba Mpya: Je rais mstaafu ashitakiwe au asishtakiwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya: Je rais mstaafu ashitakiwe au asishtakiwe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bitabo, Dec 26, 2011.

 1. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Makwaia wa Kuhenga

  YAPO matukio mawali makubwa ya hivi karibuni. Tukio la kwanza ni lile swali la mwandishi mmoja pale Ikulu alilomuuliza Rais Jakaya Kikwete hivi: “Mheshimiwa Rais, habari zilizopo zinasema mwenzio aliyetangulia katika jengo hili alifanya biashara wakati akiwa rais. Na wewe je…?”

  Tukio la pili ni pale Dodoma majuzi wakati mbunge kutoka kambi ya upinzani, alipotoa data kuhusu ubadhirifu wa Benki Kuu (BoT) na kule kupewa mkopo kwa mmoja wa wabunge kwa dhamana ya benki hiyo ya serikali.

  Matukio haya mawili ni makubwa. Yanastahili kujengewa mada pekee. Lakini mimi nitayaunganisha kuyazungumzia kwa pamoja. Kwa sababu lile swali la mwandishi linazaa tukio la pili: Haja ya kujenga na kuimarisha taasisi za utawala bora. Na taasisi hizo ni kama vile Bunge, vyombo vya habari, vyama visivyokuwa vya kiserikali na kadhalika.

  Tuanze na kale kaswali ka yule mwandishi. Kwa kweli mie binafsi nilistuka nilipokuwa nafuatilia mkutano wa rais na waandishi pale Ikulu nikiwa kwangu kupitia luninga.

  Sipendi kurudia aliyojibu rais kwa sababu wengi walifuatilia kwenye televisheni na magazeti asubuhi yake. Vichwa vya habari na hata katuni zilizochorwa baada ya mkutano huo, zilionyesha kuwa rais anamkingia kifua mwenzie aliyemtangulia.

  Mimi nadhani hilo halikuwa suala la rais kumlinda aliyemtangulia. Kwangu mimi ni suala la kulinda utulivu wa nchi yetu kwa sababu tukishaanza kuwafuatafuata marais waliomaliza ngwe yao, tutakuwa HATUFIKI. Tukianza hivyo tutatumbukia kwenye ile ngoma ya wanga ya kula nyama za watu. Hakuna kuacha!

  Mpaka sasa tunastahili kujipongeza kwa sababu kulinganisha na nchi nyingi za dunia ya tatu hata nchi za jirani tumepiga hatua kubwa ya ustaarabu wa kidemokrasia. Tunafanya uchaguzi, lakini pamoja na mapungufu yake, tunasonga mbele. Rais aliyepo anampisha anayekuja kwa wema na amani. Sasa tunaye rais wa nne. Haya ni maendeleo makubwa.

  Lakini maendeleo makubwa zaidi ni kwamba rais mstaafu anaachwa apumzike kwa amani bila kushitakiwa ama kwa tuhuma za ubadhirifu au kuvurunda kulikojitokeza wakati wa utawala wake. Lakini hatuko peke yetu katika hili. Hata wale tunaowaiga katika medani za siasa za ushindani huko Ulaya na Marekani, nao hawana hayo ya kuwaandama viongozi wao wastaafu. Kwa nini hawafanyi hivyo?

  Ndipo lile tukio la mbunge wa kambi ya upinzani kuanika bungeni data alizonazo kuhusu ubadhirifu wa BoT na zile za mbunge mwenzie linapokuwa jibu la swali hili la kwa nini marais wa nchi zilizoendelea hawashitakiwi wakishamaliza ngwe zao?

  Tofauti kubwa kati yetu na wale ni kwamba wenzetu wale wa Ulaya na Marekani wanazo tayari taasisi za kuimarisha utawala bora wenyewe wanazita “oversight institutions”. Pale Marekani mamlaka na madaraka ya rais, ingawa ni makubwa, lakini wanazo njia za kufuatilia mamlaka hayo ili yasiipeleke nchi kubaya.

  Hata kama rais wa nchi hiyo atakuwa na kiburi cha kufanya atakavyo, lakini atafanya hivyo huku akijua haungwi mkono na watu walio wengi na hivyo kukwamishwa ama asiendelee kutawala au asichaguliwe tena.

  Waziri Mkuu, Tony Blair, majuzi ameng’atuka baada ya kuona atakuwa na matatizo makubwa huko mbele ya safari kama angeendelea kutawala.

  Sasa hapa nyumbani, rais wa nchi hii ana madaraka makubwa mno yasiyo na vizingiti. Anateua kuanzia wakuu wa wilaya wa mikoa, mawaziri, majaji, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na wajumbe wake, mabalozi, makatibu wakuu na kadhalika kwa mapenzi na hekima yake tu bila kuulizwa au kushituliwa na chombo chochote cha wazi cha umma.

  Mwalimu Nyerere aliwahi yeye mwenyewe kushitukia mamlaka aliyonayo kikatiba. “Kwa mamlaka haya niliyo nayo naweza kabisa nikawa dikteta…,” alisema.

  Sasa ukifika mahali rais wa nchi hii anakuwa na mamlaka ya namna hii bila vizingiti vya kikatiba, kitamzuia kitu gani kufanya anavyotaka? Kitamzuia kitu gani yeye mwenyewe akishirikiana na waziri wake mhusika, kwa mfano Waziri wa Madini kuruhusu kuchimbwa madini na kampuni za kimataifa na nchi kuambulia mrahaba badala ya kukamata hisa?

  Kitamzuia kitu gani akiamua kumsaidia shemeji yake ambaye ana uhusiano na kampuni ya nje ya kigeni, kuleta kampuni hiyo ya kigeni kuendesha kampuni nyeti ya umma?

  Wewe msomaji wa safu hii, unaweza kunisaidia kuendeleza maswali kama haya yakajaa gazeti hili lote!

  Kutokana na jinsi katiba ya nchi yetu ilivyokaa, ni rahisi kabisa rais anayechaguliwa kwa misingi kwamba ni mtu safi, akabadilika kabisa pindi anapoingia Ikulu. Waingereza wanasema: ‘Power corrupts but absolute power corrupts absolutely – mamlaka yanalevya lakini mamlaka yasiyo vizingiti yanalevya chepe chepe!’

  Sasa tufike mahali pamoja na kujenga utamaduni mzuri ambao tumeuanza, wa marais wetu kumaliza ngwe yao kwa mujibu wa katiba na kupisha wengine na kuwaacha kupumzika kwa amani, sasa tuanze kujenga kwa dhati na kuimarisha taasisi zisizo za kiserikali, vyombo vya habari na Bunge lenyewe kuendelea kukosoa bila hofu na kwa uwazi kama alivyojaribu kufanya Mbunge Dk. Slaa (CHADEMA) majuzi.

  Inashangaza kwa mfano kusikia baadhi ya wabunge wakilalamikia taasisi isiyo ya kiserikali kama vile HakiElimu na kuishutumu kwamba inajitumbukiza kwenye mambo ya siasa na kama inataka “ijiandikishe kama chama cha siasa”. Haya ni maneno ya kipuuzi sana ambayo hayastahili kuzungumwa na wabunge ambao wanatazamiwa na wananchi kuwa ni watu wasomi wanaofahamu kuwa siasa ipo kila mahali! Tatizo la HakiElimu ni lipi? Kutahadharisha kuibuka kwa matabaka ya masikini na matajiri nchini mwetu? Eh!

  Sasa kama tunataka kuacha kunyoosheana vidole hasa kuwanyooshea vidole marais wastaafu, lazima hatua ya kijasiri ichukuliwe. Nayo ni kutazama upya katiba ya nchi iliyopo kwa sababu ndiyo inayompa rais mamlaka makubwa yasiyo vizingiti. Lakini katika hili ni vigumu kuwatazamia wabunge waliopo kufanya lolote kwa kuwa wengi wao ni wa chama tawala na baadhi yao wanatazamia kuteuliwa na rais aliyepo kuwa mawaziri na kadhalika!

  Ndiyo hapo ni muhimu kwa jamii yote ya nchi hii kuwaunga mkono wenyeviti wa vyama vya upinzani kuhusu wito wao wa kuandikwa katiba mpya ya nchi hii, ambayo itaweka sawa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuweka taasisi mpya za kulingania utawala bora. Tuzungumze wiki ijayo.

  Makwaia wa Kuhenga ni mwandishi mwandamizi, anayepatikana kwa barua pepe: makwaia@bol.co.tz

  Hii thread iliwahi kuletwa jamvini na BAK tarehe 13 JULY 2007. Kwa kuwa tunajiandaa kutoa maoni kwenye katiba mpya japo mchakato wake umeshaharibiwa na magamba na bunge lao, nadhani hii mada bado ipo ''live'' sana. tuendelee kuijadili maana juzi tu huko France yule babu Jacques Chirac kapigwa mvua zake na pilato
   
 2. M

  Mwanamutapa JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 499
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Not only the former president grabbed our national wealth while in office but also the current president is not clean either he has used his friends Edward Lowassa and Rostam Aziz to plunder the wealth of our nation, now going back to your question the answer is clear in democracy every individual is equal before the law no matter what type of position an individual might had held before or is still holding if the individual breaks the law must face justice.
   
 3. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  binadamu wote ni sawa kila mtu ahukumiwe kwa makosa yake, kwa haki na kwa sheria, kusiwe na mtu juu ya sheria, RAISI ASHITAKIWE SIO TU AKITOKA MADARAKANI BALI PIA HATA KAMA BADO YUKO MADARAKANI NA KUFANYA KOSA,
  NCHI ZOTE ZILIZOENDELEA RAISI HANA KINGA YA KUMFANYA ATENDE MAOVU NA KUKWEPA MKONO WA SHERIA
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,956
  Trophy Points: 280

  Imetulia hii Mkuu. Tungekuwa na katiba ya namna hii yule Mkapa angekuwa Keko anachezea mvua nyingi.

   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,918
  Trophy Points: 280
  Mkuu nadhani tatizo ni the "will" to take them to the court of law, kwani hukumbuki JK alisema "mwacheni mzee apumzike"?

  So therefore sheria zinaweza ziwepo ila zikafumbiwa macho.

  Utamaduni wa kuwawajibisha viongozi ukiwepo, haitajalisha kwamba wako madarakani ama hawapo, na ni wazi CCM hawawezi kuchukuliana hatua za kisheria inavyotakiwa, ukiwa CCM ni kama una immune flani against the laws of the nation, unakuwa above the law espeacially ukiwa na madaraka na pesa na uko ccm.
   
 6. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  kwa mtaji huo, kweli tunaweza kujenga uchumi imara? kwa mtaji huo, tunaweza kuheshimika duniani? tanzania tuna mabalozi zaidi ya mia moja kutoka mataifa mbali mbali wanwakilisha nchi zao hapa nchini, sasa wanaposomaga habari za, Lowassa, Rostam Aziziz, David Jairo, karamagi, chenge, Liyumba, kuvushwa twiga 133 uarabuni,Luhando kutetea maovu, hivi hawa mabalozi hutupa heshima gani wakiendaga kwao? kwa kifupi, hatuna heshima ya kimataifa kabisaa.

  madhara yake ni kuwa, nchi za asia na Uturuki hutuletea mavitu rejects,vyakula vyenye sumu, makochi ya mbao mbovu, maziwa ya sumu kwa watoto, wacheza kamali, maduka ya silaha mbovu, kwa sababu moja tuu, wanajua raisi wa nchi yetu hashitakiwi hata kama akifanya wansa makosa! mara katiba yetu ikiweka kifungu cha adhabu ya kifo na kuwa raisi yeyote akitawala nchi yetu lazima ashitakiwe akivurunda madarakani, hutasikia kamwe mchele wa sumu wala maziwa mabovu ya watoto kutoka china! wala vifaa vibovu vya umeme kutoka malaysia! ndio maana tunataka katiba mpyaa ili tuweke adhabu ya kifo na raisi ashitakiwe akivurunda! Mtu kama Luhanjo asingemkingia kifua Jairo David, maana angeogopa kifo!!!!
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,918
  Trophy Points: 280
  Binafsi ninaamini tunahitaji katiba mpya ili itusaidie kupatikana kwa viongozi wapya through uchguzi huru, watakaoweza kuwa na guts za kuisimamia katiba waliyoapa kuilinda.
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  msumari wa motto huo !! well said brother,, you have made my day Amen.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Makwaia kaandika kama an ignorant apologist for the power that be disguising as a nationalist with the good of the country at heart.

  Kakosea kuanzia uandishi mpaka mantiki.
   
 10. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,669
  Likes Received: 2,199
  Trophy Points: 280
  ukitaka kujua kwanini ccm imehodhi mchakato wa katiba mpya, ni pamoja na hayo.
  msitegemee kamwe kuingizwa kwenye katiba mpya maswala yanayo wagusa kama hayo.
  wanajua tukipewa tutunge katiba wananchi tutaingiza na hayo maswala ya kuwaondolea kinga ,
  so watatupiga chenga mpaka pasipatikane katiba yetu bali ya ccm kama ya awali! tuwapinge mapema.
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Sio kushtakiwa tu na hukumu ya kunyongwa bila kusahau viboko iwepo.
   
Loading...