katiba mpya izipe mahakama uhuru wake.

Frankness

Member
Aug 24, 2011
66
13
wadau katika hii katiba mpya naona ni vyema iwapo ibara za 108(2) na 109(1)(8)(9)(10)(11)zikasawazishwa, kana kwamba, raisi asiwe wa kuchagua principle judges wala commitee ya majaji.....either wizara ya sheria ndo iteuwe tena kwa kuangalia vigezo na uwezo wa huyo mtu kuwa judge.....si mtu anatoka kuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo na kupelekwa mahakama kuu na mahakama za rufaa.....
 
Asante kwa maoni yako, mhakama legelege kila siku husababisha mihimili miwili iliyobakia kuwa legelege. Mahakama pamoja na kutoa haku kwa wananchi in jukumu kubwa sana la kikatiba la kuwa kolokoloni,( watchdog) wa mihili hiyo miwili iliyobaki, inafanya hivyo kwa kufuta sheria zinazokinzana na katiba kwa upande wa bunge na kwa upande mwingine, serikalini, hutengua maamuzi ya watendaji ambayo yamefikiwa bila kuzingatia sheria.

Pamoja na hayo nakusihi utoe maoni yako haya kwenye tume ambayo inapatikana:

Katibu,
Tume ya kurekebisha katiba,
S L Posta 1681,
Dar es salaam.

Simu: +255 22 2133425
Fax: +255-22 2133442
baruapepe- katibu@katiba.go.org
tovuti: Tume ya Mabadiliko ya Katiba

unaweza kuwapata pia kwenye facebook na twitter uingiapo kwenye tovuti yao
 
Back
Top Bottom