Katiba mpya itaweza kutoa suluisho kwa yaliyojitokeza?

urassa

Member
Feb 13, 2009
68
1
Wanajf Katiba mpya inatakiwa kwa kuwa iliyopo sasa hivi haifai, kwa hiyo itakayokuja pengine itakidhi mahitaji ya kisheria ambayo ya sasa hivi haikidhi.
Nauliza kwamba hiyo katiba mpya itakayokuja itaweza kutatutua matatizo yaliyoshindikana kwenye katiba ya zamani au itategemea na muundo wa katiba mpya kama itaruhusu kutengua yaliyofanywa na ya zamani?:behindsofa:
 
Kaka Urassa
Huu sio Muda wa kuulizana Maswali ya Katiba itafanya nini, tunatakiwa kuisukuma serikali na pia kushiriki moja kwa kwa moja katika kuhakikisha kwamba Katiba Mpya inakididhi Mahitaji ya sasa na ya mbeleni kwa kadri tutakavyoweza kuangalia siku za usoni zitakuwa vipi.

Kwa Mfano Moja ya tatizo kubwa ambalo kama limesababishwa na katiba ama mafungufu ya sheria husika
basi moja kati ya hizo irekebishwe ili kuondokana na mafungufu hayo ni swala la uendeshaji wa vyama vya siasa na shughuli za vyama vya siasa.

Alichokifanya Kikwete, kukaribisha Familia yake nzima katika mchakato wa uchaguzi ni swala ambalo
kama ni stahiki, basi Liwe addressed kwenye Katiba Mpya.

Kikwete ametufumbua Mambo kwamba vyama vya siasa ambavyo ndio tunaamini kwamba ni vyombo
salama vinavyotumika katika kuandaa michakato na uongozi wa serikali yetu havina misingi imara, mtu
mmoja mwenye ushawishi anaweza akabadilisha taratibu zilizowekwa akaja na style zake za hajabu hajabu kabisa.

Ikiwezekana iweke vigezo vikali zaidi kwa wagombea uraisi, swala la umri sio issue sana tulitoe,badala yake tuweke vigezo makini zaidi, Wagombea wetu wa urais wawe ni watu wenye ufahamu wa juu katika maswala ya kijami, kuanzia maswala ya Dini, watambue kwamba Wananchi wataendelea kuwa na Imani tofauti na waheshimu Imani za wananchi wao, na watambue influence ya Imani za kidini katika maisha ya wananchi ikiwamo influence ya Imani za kidini katika michakato ya kisiasa, na wawe na uwezo wa kuhakikisha kwamba wananchi wakati wote hawayumbishwi na mambo kama haya.

Kuwa na Rais ambaye yeye mwenyewe analalamika na kuomba msaada bila kutoa japo elekezo moja
la nini cha kufanya, au elekezo la kurudisha wananchi kwenye mstari wakati wa taflani ni hatari, Kikwete kaishatuonyesha hili, Tuifanye katika yetu ituepushe na Viongozi wenye element za kikwete
 
Back
Top Bottom