Katiba Mpya itatupunguzia mizigo sisi wananchi

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Kwa Sasa Ni ndoto ya wachache Ila kwa sehemu kubwa Ni kero kwa wanufaika. Watatakaje katiba mpya wakati wananufaika?

Watatakaje katiba mpya wakati wanaona Raha na kufurahia tu madaraka waliyonayo? Watatakaje katiba mpya wakati inawabeba kwenye uchaguzi? Suala la katiba mpya huwezi kulizungumza mbele ya vyombo vya usalama ukatoka salama.

Madhara ya katiba tuliyonayo Ni kuwa imeleta ulemavu wa kifikra miongoni mwa wateule wachache. Mawaziri, nakatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa mikoa na kuteremka chini wote wamekuwa chombo Cha utukufu. Huwezi kusikia wanaanza hotuba bila kutaja utukufu. Kwao mwanzo mwisho hakuna dira ya kitaifa Bali utasikia TU mtukufu amesema.....mtukufu ametoa .....mtukufu ...mtukufu.

Katiba mpya Kama pendekezo la Warioba tutakuwa na serikali ndogo ambayo iko kikatiba kwa maana ya wizara. Huu utitiri wa viongozi wa kubebana hautakuwepo hivyo bajeti pia kupumua kwenye uendeshaji wa serikali. Yaani watu wanabuni tozo badala ya kupunguza ukubwa wa serikali hii Ni kichekesho.

Wananchi tutakuwa na viongozi wanaowajibika kwa wananchi na siyo hawa ambao kauli na vitendo Ni kusifia utukufu kila kukicha halafu mwisho wa siku Ni kula fedha nyingi kupitia ziara na mishahara. Mfano napenda kipengele Cha waziri kutokuwa mbunge na kuwa akihitaji kuwa waziri ataomba na kufanyiwa usahili ndipo anakuwa waziri.

Viongozi wanaotokana na furaha ya mtu mmoja kamwe hawawezi kuwatendea wananchi kazi iliyotukuka Bali watakuwa wanajipendekeza kwa aliyewateua na kuona Ni namna gani wamfurahishe na saa zingine kumshauri Mambo ya uongo ilimradi asikasirike. Wananchi tutafakari
 
Katiba mpya ni ufunguo wa Tanzania tuitakayo,na vizuri hata viongozi watapata unafuu katika uongozi wao na uwajibikaji,siasa itakuwa sio biashara kama ambavyo sasa imekuwa ni moja ya biashara ya kujipatia kipato kwa njia za udanganyifu,si unawaona wabunge karibia wote hawana uhalali wa kuwepo pale bungeni kwani namna walivyojinyakulia nafasi hizo ni yaleyale ya uteuzi.

Tukubalianeni tu kuwa bunge lililokuwepo ni bunge Teule au wabunge wake wote wameingia hapo kwa kuteuliwa na sivinginevyo,kivuli cha haki iliyokandamizwa kinawaandama na hata ukiwaangalia hawana furaha wawepo mbele ya wananchi,sijawahi kuwaona kuwa na furaha au kucheka,saa zote wapo na wasiwasi.
 
Kuna haja gani ya katiba mpya, ikiwa iliyopo tu watu wanaivunja na hakuna reaction yoyote.

Magufuli kavunja sana katiba na hakuchukuliwa hatua yoyote.

Sasa hata ikija hiyo mpya una uhakika gani hawataivunja.
 
Back
Top Bottom