Katiba mpya ilipingwa na wengi -Rasimu ya Warioba ilisiginwa- Yanayotokea sasa ni matokeo ya uzwazwa

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Wengi walifikiri watakaopata faida na katiba mpya ni kundi la kina fulani wapinzani. Wakati mijadala ilikuwa ikisisitiza katiba ni ya watanzania wote wanasiasa wa upande ule waliaminisha watu kuwa katiba na Rasimu ilikuwa suala la kichama.

Wananchi wenye nguvu kisiasa kifedha walivutia upande wa watawala wakizani maisha ya kulindana yapo ndani ya katiba.

Nilimuomba Mungu siku moja waliopinga Rasimu ya Warioba waje kukutana na masahibu ya hii katiba ya 1977.

Leo watu wanalia na ubaya wa katiba - inayoruhusu nguvu nyingi kwa watawala na uharamia wa aina yote.

Hakuna atakayetukomboa bila kuwa na katiba ya karne ya leo. Hakuna dawa zaidi ya wote kuungana na kudai katiba bora na huru. Katiba itakayotoa vifungu vya kishenzi kama kuweka mtu ndani bila kesi, kutoheshimu maamuzi ya mahakama, Mahakama kuendeshwa kisiasa , vyombo vya dola kunyanyasa raia, kuteka watu bila kuzingatia sheria, viongozi walioghushi vyeti kulindwa, wanasiasa kuamua nani afilisiwe bila kufuata sheria, visasi chuki kama ndio jinsi ya kuendesha nchi.

Katiba mpya itakayomfanya kila mtanzania kuwajibika kwa sheria. Badala ya kuishi kwa maelekezo ya mtu.

Tunaweza kuipata tukiamua - Ila kabla hatujafika huko lazima sindano kali ziwaingie wengi na wapate madhara yake ndio tutaelewana.

Yanayotokea hayanabudi kutokea ili watanzania waanze kutumia akili na elimu zao badala ya matumbo.
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
14,172
2,000
Lowassa, Sumaye, Kingunge na the like, ndio waliopinga katiba mpya!

......
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom