Katiba Mpya ikileta vurugu, CCM itakuwa ndiyo chanzo kwa kukataza mjadala

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Kuna kitu ambacho CCM hawataki kutuambia - sababu za kuiogopa sana Katiba mpya.

Tunachoona na visingizio tu kwamba Katiba mpya italeta vurugu, mara ooh tunashughulikia uchumi kwanza. Kwa nini na kwa vipi watu kujadili Katiba mpya kulete vurugu? Na Katiba mpya na uchumi vinaingilianaje? Kwani Katiba iliyopo iliandikwa tukiwa na uchumi mzuri kiasi gani? Haingii akilini, Rais Samia na serikali yako acheni visingizio vya kitoto.

Vurugu ambayo CCM na serikali yake inataka kuleta na kusingizia ni Katiba mpya inaleta vurugu ni hii dhamira ya kwazuia Chadema kuendesha makongamano ya Katiba mpya. Hivi Chadema wakiamua kukaa na kujadili katiba mpya, inamuathirije mtu mwingine ambaye sio sehemu ya hayo makongamano?

Ukweli ni kwamba CCM walikuwa tayari hata kuwafanyia fujo na kuwapiga kina Warioba kwa ajili tu ya kuzuia mchakato wa Katiba mpya usiendelee. Hilo tunajua wazi, kwamba upinzani wa CCM kwa Katiba mpya haujaanzia na Chadema, ulianza na kina Warioba. Leo hii Samia na CCM wanaendeleza tu kitu ambacho walikianza toka huko nyuma wakati wa Kikwete.

Na tunajua kwamba CCM na serikali wamedhamiria kuzuia kwa kila hali muendelezo wa mchakato wa Katiba mpya. Ikiwa walikuwa tayari kuwapiga kina Warioba, ambao kimsingi ni watu wao wa CCM, jiulize watawafanya nini Chadema ikiwa watashikilia msimamo kwamba mchakato wa katiba mpya lazima uendelee!

Basi ieleweke wazi, ikiwa Katiba mpya italeta vurugu, basi hiyo vurugu itasababishwa na CCM na serikali yake katika kujaribu kulazimisha watu wasijadili Katiba mpya, sio wale ambao wanataka kujadili mchakato wa Katiba mpya ambao ulianzishwa na CCM wenyewe

Reference:
- Rais Samia Katiba ya Tanzania sio ya Rais, wala CCM, wala Upinzani, ni ya Watanzania wote na huna mamlaka nayo. Kuapa kuilinda sivyo unavyofikiria
 
Mawazo hayapigwi rungu, tulidai Uhuru tukapata, tutadai katiba mpya na tutaipata.
 
Back
Top Bottom