Katiba mpya ifute uwakilishi haramu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya ifute uwakilishi haramu

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 15, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,254
  Trophy Points: 280
  Uwakilishi bungeni kwa zaidi ya asilimia sabini ni haramu kwa sababu hautokani na wananchi wanaoishi maeneo husika ila wahamiaji kutoka mijini huwanyang'anya wakaazi wa maeneo yale uwakilishi husika na hivyo kufanya uwakilishi huo kuwa ni haramu au kwa lugha ya kimombo carpetbaggers.........................

  Katiba mpya iweke legal residence status requirements za kuhakikisha watu kutoka mijini au nje ya nchi ambao hawakukaa kwenye majimbo yao kwa wakati mwafaka hawaruhusiwi kugombea maeneo yale....................

  Mfano utakuta mkaazi wa Dar eti kwa vile alizaliwa jimbo fuilani na kusomea kule lakini haishi pale kwa miaka nenda rudi bado anajiandikisha kuwa mgombea wa hilo jimbo kwa minajili ya kuukwaa ubunge kwenye jimbo ambalo haishi humo na matatizo yake wala hayajui ila ni ya kujulishwa tu......................

  Hata kwenye kugombea uraisi upo uhaja wa kuweka legal residence requirements kwa minajili ya kuwazuia walowezi wetu waliokaa nje ya nchi kwa miaka mingi kutokuja na kuvuruga utawala wetu kwa kugombea nafasi hii nyeti wakati hawajaishi humu nchini ili kuyafahamu matatizo yetu.................
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Good thinking. Haya mawazo nayaafiki kwa asilimia mia moja kwani wengi 'hujirudisha' majimboni wakati wa uchaguzi ilhali hawajui matatizo ya jio husika. Ila haya mawazo yatapata upinzani mkali sana kwani wengi wa wanasiasa wanafaidika na mfumo wa sasa.
   
 3. K

  Kwiifoenda Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli wawakilishi wengi wanakuja kama mamluki wakati wa uchaguzi, mfano batilida kugombea Arusha, Mpendazoe kugombea segerea nk ulikuwa ni uhuni wa kisiasa! Hawa mara nyingi ni watu wenye malengo ya mda mfupi ya kujinufaisha kwa nafasi zao huku wakiwaacha watu bila uwakilishi! Koffi Anan aliwahi kukataliwa kugombea urais wa Ghana kwa kigezo cha kuishi nje ya nchi kwa miaka mingi!
   
Loading...