Katiba mpya ifikapo 2013 inawezekana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya ifikapo 2013 inawezekana

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Fareed, Nov 21, 2010.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Kikwete eteue Constitutional Review Commission


  DAR ES SALAAM, November 21, 2010

  Ili kuiokoa Tanzania na political crisis au impasse/stalemate kama iliyotokea
  Zanzibar, Rais Kikwete anapaswa kukubali matakwa ya wananchi ya kuwepo katiba
  mpya.

  Hii inatokana na ukweli kuwa Katiba iliyopo ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya
  mwaka 1977 ni batili.

  Katiba iliyopo ni batili kwa sababu 3 kuu:

  1. Ilitungwa kwa kukiukwa kwa mchakato unaokubalika kimataifa wa kutengeneza
  katiba ambao unataka uwepo mkutano wa kitaifa wa katiba ambapo makundi yote ya
  jamii yatakuwa yamewakilishwa, eg wanawake, vijana, wazee, viongozi wa dini,
  viongozi wa siasa, wasomi, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, n.k.

  2. Katiba iliandikwa mwaka 1977 wakati Tanzania iko katika mfumo wa chama kimoja
  cha siasa na kikundi cha watu wachache wasiozidi watano ambao walikuwa ni makada
  wa CCM.

  3. Miaka 33 tangu katiba ilipoandikwa, imewekwa viraka visivyopungua 14
  (marekebisho ya katiba). Katiba iliyo kamili huwa haibadilishwi mara kwa mara. Hii
  ni ishara kuwa katiba iliyopo ni batili na haijazingatia mabadiliko makubwa
  yaliyotokea Tanzania, ikiwemo kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi 1992.

  Kama Kikwete anataka kuacha legacy ili akumbukwe kwa mema, basi iwe ni hii ya kuleta
  katiba mpya.

  Kuanzia, Kikwete anashauriwa aunde Tume ya Kupitia Upya Katiba (Constitutional
  Review Commission) ambayo ipewe miezi 6 kukamilisha kazi yake na kukabidhi ripoti
  kwa serikali ifikapo Mei 31, 2011. Kuna majaji wengi waadilifu kama Robert Kissanga wanaweza kuongoza tume hii.

  Kwenye Bunge la Bajeti ya July-September 2011, upelekwe Bungeni muswada wa the
  National Constitutional Conference (NCC) Bill of 2011.

  Bunge likishapitisha muswada huu kuwa sheria, serikali inaunda rasmi the National
  Constitutional Conference (mkutano mkuu wa kitaifa wa katiba).

  Hii National Constitutional Conference ipewe kazi ya kukamilisha katiba mpya na
  kupitishwa kwake na Bunge kabla ya kuisha kwa mwaka 2013.

  Hii ina maana kuwa itabaki miaka 2 ambayo serikali, vyama vya siasa, NGOs na
  taasisi nyingine zitakuwa na muda wa kutoa elimu kwa jamii ili Watanzania waielewe
  katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2015.

  Katiba ya watu (a people's constitution) ndiyo suluhisho pekee la haki, maendeleo,
  amani na utulivu ya kudumu Tanzania.

  * Kenya wamepata katiba mpya baada ya damu nyingi za raia kumwagika. Tusifike
  huko. Tuige mfano wa majirani zetu Zambia ambao wameanzisha mchakato wa katiba
  mpya kwa amani na utulivu.

  Tembelea: About the NCC - National Constitutional Conference, Zambia
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuuu safi kabisa kwa mchango wenye busara ..... national constitutional conference will succeed constitution referendum ? please advice... na watanzania sasa tukae mkao wa kuanza mchakato wa kuangalia mambo muhimu tunayohitaji kuyaweka katika katiba mpya e.g death penelty is purely unecessary kwa mawazo yangu.. kwanini naita katiba mpya .... hii iliyopo ni OBSOLETE-please check all interpretations of this word careful ... na ukweli ni kwamba katiba hii ya mwaka 1977 ndio mwaka CCM a.k.a jembe na nyundo ilipozaliwa
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  2013 mbona mbali!
  Michakato ikianza February I'm sure 2011 hadi June 2011 tayari tutakuwa na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
   
 4. m

  matawi JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Perfect. Hiki ndo cha muhimu ukiweka sawa katiba mbona kuipeleka nchi kwenye asali na maziwa rahisi sana. Tanzania itakuwa nchi nzuri sana
   
 5. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa katiba mpya inahitajika kwa manufaa ya watanzania wote.
  Tatizo linakuja pale ambapo ni wanasiasa wa upinzani pekee ndo wanaolilia hili.
  Mtanzania wa kawaida haijui hata hiyo katiba ya sasa inasemaje.wengine wamebaki wanajiuliza katiba ni kitu gani?
  Kuna umuhimu wa katiba kuanza kufundishwa mashuleni kuanzia elimu ya msingi.
   
 6. e

  emma 26 Senior Member

  #6
  Nov 21, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ujumbe wenye busara
   
 7. F

  Fareed JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni sawa kabisa, nyingine nchi huitisha national referendum kwanza kuona kama wananchi wanataka katiba mpya au kufanya mabadiliko. Kwa hali ilivyo Tanzania, kwa kuwa katiba iliyopo ni batili na haikushirikisha wananchi ilipoandikwa 1977, hamna haja ya national referendum. It's a costly exercise and it's time consuming. Pia kuna uwezekano mkubwa serikali iliyopo madarakani ikachakachua matokeo ya referendum kama walivyofanya kwenye uchaguzi mkuu.

  Itakapoandikwa katiba mpya kwa kushirikisha wananchi kupitia National Constitutional Conference, kitawekwa kipengele kwenye katiba hiyo mpya kuwa mabadiliko yoyote ya katiba hii ya wananchi kwa siku za usoni hayawezi kufanywa mpaka yapate baraka za wananchi kupitia referendum.
   
 8. F

  Fareed JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu uzoefu wa nchi nyingine umeonesha kuwa kuandika katiba mpya kwa kufuata mchakato unaokubalika kimataifa ni suala gumu na linachukua muda sana kwani kunakuwa na mavutano mengi na pia kuna makundi mengi yenye mawazo tofauti lazima yashirikishwe. Kwa maoni yangu katiba mpya by 2013 is conceivable ingawa ni kweli mchakato unaweza kuwa fast-tracked kama kuna political commitment ya watawala.

  Hofu ninayoiona mimi ni kuwa hata Kikwete akikubali wazo la katiba mpya, bado serikali yake inaweza kuchelewesha mchakato kwa makusudi ili uchaguzi wa 2015 ufanyike chini ya katiba hii hii iliyoandikwa na makada wa CCM kwa faida ya CCM.

  This is a very urgent matter. Ninashauri CHADEMA wakae chini na CUF na vyama vingine vya upinzani na kuweka tofauti zao pembeni washuhulikie madai ya katiba mpya mara moja bila kuchelewa. Pamoja na tofauti zao zote, naelewa kuwa vyama vya upinzani wako pamoja sana kwenye kudai katiba mpya.

  Jambo la kutia moyo ni kuwa Watanzania wanataka katiba mpya, NGOs, donors, nao wanaunga mkono pia wazo hili na wako tayari kutoa pesa.
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  Nov 21, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nashukuru mmeliona hilo niliongelea hapa ktk jf ila bwana think twise akaja na maneno ya kashfa na kunibaguwa kuwa mi si mtz eti kwanini nahoji katiba,haya think twise,umeona ma great thikers tunavyo ona mbali,we subiri hapo home sisi tutapigania kukuletea katiba mpya na utafaidi matunda.
  ikiwezekana mchakato uanze sasa hakuna mda wa kusubili hizo pesa ccm inazotaka kufungulia kesi za uchaguzi kwa madiwani na wabunge kama alivyosema makamba serikali izitumie ktk mchakato wa katiba mpya

  mapinduziiiii daimaaaaa
   
 10. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  haya na tupaze sauti zetu wote kudai mabadiliko.
   
 11. b

  bojuka Senior Member

  #11
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HATUWEZI KUSUBIRI HADI 2013 TUNATAKA MCHAKATO UANZE FEBRUARI 2011
  No gap to loose
   
 12. T

  The Informer Senior Member

  #12
  Nov 21, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli, 2013 mbali sana. Hapo watakuwa wamepata fursa ya kuchelewesha mchakato makusudi ili 2015 ije tukiwa hatuna katiba mpya. Sisi tunasema tunataka katiba mpya NOW!
   
 13. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mawazo bomba
   
Loading...