Katiba Mpya Ielekeze Jinsi ya Kuiondoa Madarakani Serikali Iliyoshindwa Kazi Wakati Wowote

Kaldinali

JF-Expert Member
May 25, 2012
263
144
Katika maoni ya Katiba tuhakikisheKatiba itakayopatikana itaelekeza kwa uwazi njia halali ambazo wananchi watazitumia kuitoa madarakani kabla ya muda wa uchaguzi, serikali itakayothibitika kuwa imeshindwa kuongoza.


Moja ya sababu kubwa ambayo itoshe kuiondoa serikali iliyoko madarakani ni pale itakapofikia uamuzi wa kuligeuza Jeshi la Ulinzi wa wananchi JWTZ kuwa jeshi la kupambana na wananchi. Matumizi ya Jeshi bila idhini ya Bunge ndivyo walivyokuwa wanafanya akina Iddi Amin, Bokassa, Hittler na wenzake! Katika utawala uliostaarabika kidemokrasia hii ni dhambi kubwa haikubaliki.


Nyingine iwe ni serikali kutuhumiwa kwa unyama na mauaji ya raia wasio na hatia na hivyo kuwafanya wananchi waishi maisha ya hofu! Nchi kujaa migomo na vurugu zinazowafanya wananchi kukosa amani nchini mwao. Hapa ambapo serikali ya awamu ya 4 imewafikisha wananchi ni pabaya. Nchi inatengeneza visasi vingi! Bila kuwa makini kitakachofuata baada ya serikali hii kuondoka itakuwa ni kulipizana visasi tu! Tutawaficha wapi watoto wetu na wana wa nchi hii? Robert Manumba mkurugenzi wa upelelezi nchini, akimlilia kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza aliyeuawa na majambazi amewaamrisha Polisi walipe kisasi dhidi ya raia. Ni tamko la bahati mbaya kwa wadhifa alionao! Watu wa Mungu wanauliza je, na raia nao watumie amri hiyohiyo ya Manumba kulipiza kisasi kwa Polisi waliomuua mwandishi wa habari huko Iringa?

PASCHALLY MAYEGA: KIPANDE CHA MAKALA GAZETI LA TANZANIA DAIMA 10-24-2012
TEL 0713334239
 
Back
Top Bottom