Katiba Mpya haitashuka kama mana jangwani. Mapito ya Mbowe na CHADEMA ndio njia yenyewe chungu yenye shubiri lakini yenye tija

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Siku zote watawala hawataki kugawana power na wengine wao wangependa kuhodhi power hiyo milele. Mungu fundi akaweka kifo na sisi wanadamu tukajiwekea katiba.

Rais aliyepita Magufuli alitufundisha vizuri sana umuhimu wa katiba Bora. Aliwaambia wazi wakurugenzi nikulipe mshahara nikupe gari walinzi nk halafu umtangaze mpinzani kashinda? Hili lilikuwa somo kubwa sana kwa Watanzania.

Wakati Magufuli akiwaambia hivyo wakurugenzi ni utaratibu wa CCM kuchagua wakurugenzi ambao ni makada wa CCM Sasa swali linakuja makada wa CCM watasimamiaje uchaguzi wa haki?

Hapa ndipo umuhimu wa katiba mpya unapoanza Jambo jingine matokeo ya urais hayatapingwa mahakamani. Haya ni maajabu mengine.

Yani makada wa CCM (wakurugenzi) wasimamie uchaguzi halafu utegemee uwe free and fair nooo haiwezekani halafu at last eti akitangazwa mshindi wa CCM usiende kudai haki mahakamani hapana hii sio sawa.

Muda ni huu

Wakati sahihi ni huu !
Katiba mpya ni Sasa.
Chadema wasitegemee kuingia kwenye kipute Cha uchaguzi mkuu 2025 kwa katiba hii itakuwa ni kupoteza muda hivyo kuanza kuidai Sasa ni perfect timing kwao .

Tukubaliane kwa uwazi CCM wasingependa kuondoka madarakani milele na kuruhusu katiba mpya ndio kuiondoa ccm madarakani.

Hivyo ni haki kusema KATIBA MPYA HAITASHUKA KAMA MANA JANGWANI NI LAZIMA IPIGANIWE KWA NGUVU ZOTE.
 
Hili jambo nimelisisitiza sana, cdm wasikubali hii hadithi eti tutoe muda, muda ni sasa. Anayetaka kusubiri ikishapatikana hii mpya atatafuta nyingine aliyoisuburi.
 
Tuwaelimishe wananchi Haki na wajibu wao, lipa Kodi.... Pia hoji na dai, huduma stahiki, sio hisani ya kiongozi .....Katiba mpya!
 
Back
Top Bottom