Katiba Mpya: Diaspora tuhusishwe pia kwenye mawazo kama Watanzania wengine


K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,314
Likes
735
Points
280
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,314 735 280
Katiba mpya ya Tanzania inaandaliwa lakini Diaspora wa Tanzania hatujahusishwa wakati ukweli ni kwamba ni wengi sana dunia nzima kuanzia Europe yote, Asia, Americas, Africa and Australia. Tume ya Walioba inatakiwa kuweka mikakati kuhakisha Watanzania wa Diaspora nao mawazo yao yanasikika. Mimi ningeshauri wajumbe wasafiri baadhi ya sehemu ambazo kuna Watanzania wengi wa Diaspora na Kuongea nao ili tuhakikishe kila Mtanzania amewakilishwa kwenye mchakato wa Katiba ambayo ni ya Watanzania wote. Tatizo moja la kuweka wazee wengi kwenye tume ya katiba bado hawana mwanga kwamba Watanzania siku hizi wapo dunia nzima na wana mchango muhimu kwa nchi na wanahitajika kuhusishwa. Nimeshangazwa sana na CCM na Chadema wamekuja huku nchi za mbali kufungua matawi ya Chama lakini wanashidwa kusimama na kutoa ushauri kama huu ambao una manufaa kwa taifa. Tunaomba msaada wa kuhimiza tume wa Warioba iweze kuongea na Watanzania wa Diaspora
 

Forum statistics

Threads 1,235,907
Members 474,863
Posts 29,240,086