Katiba Mpya: CHADEMA msikubali mkutano wenu na JK kuhusisha vyama vingine, hasa CUF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya: CHADEMA msikubali mkutano wenu na JK kuhusisha vyama vingine, hasa CUF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Nov 24, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Chonde chonde viongozi wa Chadema – katika mkutano wenu na JK kuhusu Katiba mpya, kamwe msikubali ujumuishe vyama vingine kama ilivyopendekezwa na Kamati Kuu ya CCM (CC) kwa Rais Kikwete.

  Ni vyema kila chama kikakutana na JK peke yake.

  Hofu yangu ni kwamba pendekezo hili limetolewa ili kumsaidia JK kukabiliana na hoja za viongozi wa Chadema wtakaokwenda kukutana naye. Wajumbe wa CUF watakaokwenda, ambacho ni chama mshiriki wa CCM huko Zanzibar, wanaweza kuvuruga mkutano huo ukiwa wa pamoja na Chadema ikaonekana haina hoja.

  Nasema hivyo kwa sababu tayari CCM inaonekana kuufanya Muungano kuwa ni mtaji wake mkubwa wa kisiasa katika suala la Katiba mpya kwa kuwapa Zanzibar uwakilishi sawa jambo ambalo CDM inalipinga kwa sababu ya kutokuwap pia kwa serikali ya "Tanganyika" katika Muungano.

  Ingekuwapo serikali hiyo ya Tanganyika, uwakilishi wa namna hiyo ungekubalika na CDM.

  Msifanye makosa CDM kujijumlisha na vyama vingine katika mkutano na JK – na hasa CUF – maana hawa CUF wako zaidi kwa masilahi ya Zanzibar na CCM.

  Natoa tahadhari.
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye red (well said) - maelezo haya hapa chini nimeyaweka kwenye post nyingine

   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu -- Nakuunga mkono 100 asilimia. Kila chama kiende kwa JK kivyake!
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  So waliobaki waende january infakt
   
 5. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Huu mkutano umeombwa na CHADEMA, na CHADEMA wamesema wanaomba kukutana na Rais. Kama Rais ana mpango wa kuwa na mkutano na vyama vyote vya siasa, nina imani atawaalika kwa wakati mwingine, na hapo kila chama cha siasa kitaamua kama kitashiriki au la.

  Lakini Rais ataonekana mtu wa ajabu sana kwenye mkutano ambao CHADEMA wameomba kukutana na Rais, halafu Rais akavialika vyama vingine, ikiwa hivyo basi CHADEMA wana haki ya kugomea mkutano wa namna hiyo maana hawakuomba kukutana na vyama vingine vya siasa ikulu.
   
 6. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hivi hoja walizonazo CHADEMA kukutana na JK ndio hoja za hivyo vyama vingine CCM wanaoshinikiza wahusishwe?

  Hii michezo ya Kitoto CCM wanayofanya ishapitwa na wakati kama CCM wanataka na hivyo vyama vingine vishiriki pamoja waombe miadi na JK na sio kukurupuka eti kisa CDM... CCM wasipotumia busara huu mchakato katiba mpya itakuwa vurugu tupu..
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hata mimi naunga mkono hoja! Cdm ilishakataa ushirikiano na kafu. Kwanza wao waliukubali mswada na kushiriki kuupitisha. Sasa wataenda kwa jk kujadili nini?

  Cdm wasikubali!!!!!?
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Mkuu unategemea nini toka kwa msanii!? CHADEMA waneomba mkutano na yeye kama CHADEMA halafu anataka katika mkutano huo viwepo vyama vingine!!!!

  Juzi tu SAS na Kitine wamemwambia kuhusu umuhimu mkubwa wa chama chake kukaa chini na CHADEMA kuhusiana na upatikanaji wa katiba mpya... Kikwete haitakii mema nchi yetu.
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  CC ya CCM ndiyo imetoa pendekezo la vyama vingine pikutane na Rais
  • Hivi vyama vilipanga kukuta na Rais
  • Vina hoja ya kuiwasiklisha kwa Rais
  • Vimejipanga vizuri au vinashurutishwa tu
  Tuwaache hawa wenye hoja walio jiandaa wawasilishe hoja zao hii ni kwa masilahi ya umma wote
   
 10. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,959
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja.
   
 11. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tatitizo la CCM hawaamini kuwa CDM ni chama cha UPINZANI ndiyo maana wanawachukulia ki simple tu
   
 12. M

  Marytina JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  kweli hapo JK anatafuta wakumsaidia kuchakachua hoja
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Si kazi inatafutwa sababu tu ya kuuvuruga mkutano huo!

  Kama ccm wanadhani kuna haja ya vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni(ccm, cdm, cuf, nccr etc) kukutana ni vema wakaandaa mkutano mwengine badala ya kutaka kudandia huu ulioombwa na cdm.
   
 14. l

  luhwege Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Naunga mkono hoja kwa kuwa vyama vingine vipo kwa ajili ya kufuata upepo sitashangaa wakaingia kichwakichwa CDM semeni hapana kama watalazimisha mjiondoe tupo nyuma yenu kwani watetea haki nchi hii ni CDM tuuuuuu naunga mkono 100%
   
 15. K

  Kamura JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama suala ni kujadili katiba kwa nini vyama vyote visikutane pamoja kuliko kwenda kimojakimoja? acheni ubaguzi, THIS IS NOT A ONE MAN SHOW!
   
 16. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  CUF hawana ulazima wa kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa watawakilishwa na huyo huyo JK
   
 17. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  mleta mada uko sahihi sana........nami nahauri siku hiyo wakiiigia ikulu na kukuta kuna mlema , dovutwa,jusa na wengine chadema wamwambie kikwete sisi tulikuja kuongea na wewe na si kuongea na vyama vingine.......watoke nje wajipukute mavumbi nje ya mlango pale ikulu waondoke.............
   
 18. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  we mwehu nini....hivyo vyama vingine ni lini vimeomba kukutana na huyo jk??
   
 19. i

  ibange JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli maana ukiondoa chadema na wabunge wa NCCR (sio chama ila wabunge) hakuna chama kingine kinachopinga. Kama hawapingi unakutana nao wa nini? Kama unataka kukutana nao aombe m kutano mwingine.

  Issue chadema wanapinga mchakato ambao umeungwa mkono na CUF(CCM B) na TLP(CCM C). Sasa huwezi kusema cuf na tlp ni wapinzani. Wanataka kuwatumia ku neutralise hoja
   
 20. l

  limited JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  this is not right kinachotafutwa ni solution sio malumbano ya vyama na chama.
   
Loading...