Katiba Mpya, Cha kutisha, Kusikitisha na Kushangaza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya, Cha kutisha, Kusikitisha na Kushangaza!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Tumbomoto, Aug 18, 2012.

 1. T

  Tumbomoto New Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninaamini kwamba kila mtanzania anashauku na anangoja kwa hamu kukamilika na kutangazwa kwa katiba mpya. Kinachonishikitisha, kunitisha, kuniogopesha na kunishangaza ni kuona kwamba kati wa wataalamu na wasomi wote walioko hapa Tanzania, aliyeonekana kufaa kusimamia na kuendesha zoezi zima la urekebishaji wa hiyo katiba si mwingine ile Mzee Kikongwe, Mheshimiwa Joseph Sinde Warioba! Hili limeturudisha kwenye ule ule mchezo wa kurushiana mpira kwa chenga kali. Vizee ambavyo vimekuwa vikiyumbishayumbisha hii nchi tangu wakati wa uhuru ni hao hao tu - Kaa pale nikupasie, na ukishapiga danadana chache unirudishie, na mimi nitakurudishia. Eboo! Sisi vijana tutaingia lini kwenye hiyo kabumbu? Tangu nikitambaa, nimekuwa nikisikia hilo jina Wariobawariobawarioba...! Mzee, ulikuwa na ulipewa nafasi nyingi sana za kuleta mapinduzi ya kubadili hali duni na unyonge wa Mwafrika ukianzia na Mtanzania. Kama miaka yote hiyo hukufanya chochote kinachoonekana na ambacho waweza kujivunia, sasa hivi ni jioni kwako, jua linazama na usiku unaingia! La busara kwako kufanya ni kuinua mikono juu uwaachie wengine wajaribu. Acha kuwahadaa watanzania kwani umezunguka karibu ofisi zote hapo Dar es salaamu kwa miaka mingi ajabu. Zaidi ya kwamba uliitwa Mheshimiwa, Mheshimiwa, Mheshimiwa, sioni ni kigezo au umaarufu gani uliotumika kukupatia hiyo kazi ya katiba. Badala yake, wape vijana wasomi mliowafunikia kwenye mazulia nafasi ili nao wajaribu kwa awamu yao. Wewe Warioba unatakiwa atafutiwe kijana akukokee moto uote na uvute kiko, kama ni ushauri tutakufuata kwa heshima na taadhima, lakin kwamba wewe ndiye mtengeneza katiba - Uongo mtu na ni kupoteza muda wa watanzania!
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Subiri wafanye madudu, safari hii kizazi cha dot com hakikubali kuburuzwa! kama hawatafanya cha maana tutafanya baada ya uchaguzi 2015, na tutawachukulia kwa kushindwa kulitendea haki hili taifa!! Kifupi tuko macho na tunafuatilia kwa makini tena hatua kwa hatua.
   
Loading...