Katiba kupatikana kwa kupambana na Polisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba kupatikana kwa kupambana na Polisi?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by We can, Dec 29, 2010.

 1. W

  We can JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tokea vuvuvugu la Katiba mpya lipambe moto hasa baada ya Uchaguzi wa mwaka huu 2010, polisi nao wanaonekana kutoa mwongozo wa namna ya kudai Katiba. Kama siyo usanii walioufanya jana Jijini Dar Es Salaam, basi ni dhahiri kuwa hawajui wajibu wao. Huwezi kumzuia mtu kuandamana masaa machache kabla ya kuandamana huku akiwa ameshakupa taarifa zaidi ya masaa 72. Harafu, huwezi ukatoa mwongozo wa namna ya kuandamana wewe polisi! Kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao.

  Nionavyo mimi, si Polisi, wala mtu yeyote (anayedhani yuko karibu na mungu) na awaye yote, anayeweza kuzuia UANDIKWAJI wa Katiba Mpya 2011. Si jeshi, si polisi, si mahakama wala bunge, wanaweza kupinga suala hili. Tena, hayupo mtu hata mmoja anayeweza kuchelewesha mchakato huu AKAFANIKIWA!

  Tazama aibu zinavyowapata wale wanaojituma au kutumwa kuja kuropoka juu ya hoja za kupinga kuandikwa katiba mpya. Wanataka viraka kwa Katiba mpya ili maisha ya Wa Tanzania, yaendelee kuwa VIRAKA. Je, ni lini mara ya mwisho walivaa nguo za viraka?

  Hebu tuwe waungwana, Mh. Kombani na Werema, are you serious when you come in front with such wiseless ideas? SHAME ON YOU.

  Bila shaka Mh. Dk. Kikwete atatokea muda mfupi (kabla ya 2011) na kuwajuza wa Tanzania hatima ya uandikishwaji KATIBA MPYA. Tunahamu sana kusikia anasema nini juu ya hili......
   
Loading...