Katiba: Kauli ya Mhe. Freeman Mbowe Kuhusu Mazungumzo na JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba: Kauli ya Mhe. Freeman Mbowe Kuhusu Mazungumzo na JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Nov 29, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Wanabodi, nimeona niwawekee kauli ya M/Kiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe akihojiwa na BBC jana jioni kuhusu mazungumzo ya Chadema na rais Jakaya Kikwete.

  Ili kuwasaidia wasioweza kuifungua haya mahojiano, nitawawekea transcription ya alichoongea neno kwa neno.

  Hear for yourself from Horses Mouth!.

  Pasco

  Update 1. Transcript:
  Transcript
  Charles Hillary : " ...Rais wa nchi hiyo Jakaya Kikwete kuendelea kuineemesha katiba hiyo ili kukidhi mahitaji ya kujenga kuaminiana na muafaka wa kitaifa. Makubaliano hayo yamefanyika baada ya chama cha Chadema ambacho wabunge wake walisusia hatua ya kusomwa na kupitishwa kwa muswada wa juu ya kuundwa katiba mpya nchini humo, kuomba kukutana na rais Kikwete.

  Eric David Nampesya, amezungumza na mwenyekiti wa chama cha Chadema, Freeman Mbowe, kwanza anaeleza kilichoafikiwa kwenye mazungumzo hayo"

  Mhe. Mbowe: "Cha msingi kuliko vyote, ni kwamba ni vyema kila mmoja wetu na kila Mtanzania akatambua kwamba, hoja ya kubadilisha ama kuandika upya katiba yetu ni ho
  ja ambayo ni ya mchakato, siyo jambo ambalo linamalizika kwa siku moja, kwa maana hiyo tumekubalianan kimsingi kwamba, iko haja ya kufanya mashauriano mara kwa mara na wadau mbalimbali, sio Chadema peke yake, wako wadau wengi katika taifa hili ambao wanapenda kuona mabadiliko haya ya katiba, yanatujenga kama taifa na hayatugawi kama taifa, kwa hiyo tumekubaliana kimsingi kwamba, ipo haja ya kuendelea kufanya vikao vya mashauriano tumemuomba rais pia aendelee kufa mashauriano na wadau wengine ndani ya vyama vya siasa, nje ya vyama vya siasa ili kuendelea zaidi kupata muafaka wa kitaifa

  Eric David Nampesya: " Lakini hoja yenu ya msingi ilikuwa ni kupinga jinsi mchakato ule mzima ulivyoendesha ambapo muswada ulisomwa kwa mara ya pili, nyinyi mkipinga kutaka usomwe kwa mara ya kwanza, inamaana sasa mmeridhia kilichotokea katika bunge mjini Dodoma?.

  Mhe. Freeman Mbowe: "Hapana, hapana, hatujaridhia kilichofanyika Dodoma, bado tumelalamika kuwa muswada ule ni mbovu, na bado tumeiachia serikali tuone itafanya nini katika kuurekebisha muswada huo, na tunajua wako wadau wengine wengi ambao nao wana mawazo yao, tunaimani kwamba serikali, kwa kauli aliyoitoa rais, pengine nae atawapa fursa ya kuwasikiliza malalamiko yao, kisha pengine serikali ilete sasa marekebisho ya ya ya sheria, ili kuwezesha kuingiza hoja mbalimbali ama kupunguza mambo mbalimbali yaliyokuwa yana lalamikiwa".

  Eric David Nampesya: Awali mlisema kwamba kama rais asingekutana na ninyi mngepeleka kilio chenu kwa wananchi hali inayotafsiriwa kwamba ni kuhamasisha maandamano nchi nzima, kwa maana hii, baada ya rais kukutana na ninyi, sasa mnafuta mpango wenu huo?.

  Mhe. Freeman Mbowe: "Ehe ee niseme tuu kwambaa..., tumezungumza tuu kwa kina kwa kweli, tumezungumza kwa kina, naa na serikali imeonyesha nia kutaka kufanya marekebisho ya msingi katika katiba hii, na kwa maana hiyo, tutaitegemea serikali kuchukua hatua za haraka, katika kikao kijacho cha bunge, tufanye baadhi ya mabadiliko ambayo yatapelekea kuleta mshikamano na maridhiano. Kwa maana hiyo, hatutakuwa na maandamano ya kupinga katiba katika hatua ya sasa, mpaka tungojee serikali ifanye mabadiliko ya msingi"

  Transcript inaendelea...
   

  Attached Files:

 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  waiting!
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Tupo pamoja mkuu,
   
 4. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nimeisikiliza, but kinachochanganya hapa ni kwamba haelezi kama walikubali Rais asaini muswada au la,
  lakini pia inaonekana kimsingi wameiachia Serikali kwa maana ya kuiamini kwamba itafanya marekebisho kulingana na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali, of which we have to forget. bado nasisitiza kwamba Tumeuzwa kwa bei rahisi sana kuliko ile walipwayo wale wa Ohio.
   
 5. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  unachokisema ndicho nami nimekisikia akihojiwa mh. Mbowe kwenye radio station moja hivi. Wanachotegemea wao ni kuona marekebisho au mapendekezo yao yakifanyiwa kazi kwenye bunge lijalo hapo january.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Sahara Voice, Mhe. Mbowe amesema kila kitu. Kama ilivyo kuongea kila mtu anauwezo wa kuongea ila sio kila mtu ana uwezo wa kuongea na kujieleza kiufasaha ili kueleweka vyema.

  Vivyo hivyo kwenye kusikiliza, kila mwenye masikio anaweza kusikia ila sio kila anaesikia anaweza kuelewa vyema kilichozungumzwa!.

  Nikipata muda nitawafanyia transcription ya neno kwa neno.
   
 7. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani naona mijadala inayoendelea huku kwenye JF inahusisha members tu ambapo kila mtu anakuja na lake. Zaidi ya haya maoni yetu ni barua za Ikulu na ile waliyosaini Mnyika na Nchimbi ambazo zote hazikuweka wazi nini hasa kimekubaliwa. Leo tumesikia Rais ametia sahihi hiyo sheria.

  Sasa hapa naona kuna mkanganyiko na mpaka sasa hakuna tamko lolote lililosainiwa na kiongozi wa CHADEMA kutuelezea wananchi nini hasa wamekubaliana na Kikwete na kama kweli walikubaliana Kikwete atie sahihi huo muswada ndipo mijadala ije baadaye. Tunaomba tamko kutoka kwa viongozi wa juu wa CHADEMA watuondolee sintofahamu hii. Wasituweke wananchi katika tension hapa kwa kujifikirisha nini hasa makubaliano yao.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Maeneo yangu Mhe. Ngeleja kafanya mambo, transcript kesho!.
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  muugano, composition ya wajumbe wa bunge la katiba, muundo wa ukusanyaji wa katiba ndio malalamiko ya chadema

  yanaboresha katiba ..kupita tume iliyopo ..mimi nafikiri no. hakuna cha maana rais unda tume tuendelee kutoa maoni yetu
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu Pasco...
  Tatizo watu wana mahaba na Chadema hawataki kuamini kama Mh Mbowe anaweza kusema hayo maneno
   
 11. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu Pasco,
  Watu wMbowe hakuwa na uwezo wa kumzuia JK kusaini huo mswaada, Mbowe na CDm wamefikisha kwa maandishi yale wanayoamini kuwa yangefaa zaidi kwenye mswaada kuliko hivi ulivyo sasa. Jukumu ya kuzuia usisainiwe walikuwa nalo wabunge wa ccm before and then JK himself. Wengine ni watanzania as individuals walikuwa na uwezo wa kujaa mitaani ka kuzuia hilo lisifanyike but what did they do??? kukaa kwenye computer na kulalamika, wengine vijiweni nk. Nadhani kama tunataka mabadiliko yeyote ni jukumu letu kuhakikisha yanatokea
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Umesema na umenisemea vyema mno.Nawashangaa kucha kutwa wanasema Chadema hivi au vile na wao wanajiweka pembeni utadhani si Watanzania .Too bad kupenda vya rahisi ukiwa mbali .Nashukuru mkuu umenena vyema labda itasaidia watu kubadilika hapa .
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lunyungu, mchelea mwana kulia, hulia yeye!. Watu wameweka too much great expectations on Chadema as if Chadema ndio one and only aliyetegemewa kuupinga muswada ule!.

  Natetea misimamo na maswali yangu kwao nikiamini yanasaidia kuamsha pale mlipolala na ikifika mkakumbuka shuka asubuhi, tutawaambia angalau tuliwaambia!.

  Tanzania ni yetu sote, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunapata katiba bora na sio bora katiba!.
   
 14. A

  Ame JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280

  Watu walikuwa tayari kuja kitaa lakini wapi viongozi wao walio amini wame beba matamanio yao? Mine or mine nyie watu acheni kuumiza wanyonge bana kuzichezea feelings zao kila siku mnataka waanze kujilipua ndo mjue watu wamechoka?
   
 15. A

  Ame JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Haya bwana nimeamua kufuta hasira yangu!
   
 16. O

  Omr JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tayari kawekwa mfukoni na kikwete huyo. Huu ndio mwanzo wa mgawanyiko wa CDM, yanayo tokea CCM sasa ndio yanaelekea CDM. Makundi mawili yatajitokeza na hili kundi la wageni wa KIkwete ndio watashinda.
   
 17. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Usitake kujijumuisha wakati huwa unataka kujipapanua kama by stander!
   
 18. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  huijui siasa............kati ya CUF na Hamad nani kawekwa mfukoni mwa CCM?

  it is easy kwa mwanachama mmoja kuwekwa mfukoni, lakini ukikiona chama kimewekwa mfukoni ujue habari imekwisha.
  chagua utakalo........kama sio tikiti maji utajua nalosema hapa.
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,136
  Likes Received: 6,631
  Trophy Points: 280
  sijui hata akina mbowe kilichowapeleka ikulu ni kitu gani,
  wangebaki kule mjengoni kama walitaka kuchangia kuhusu katiba,
  mimi naona wameanza kupenda kubembelezwa,
  wameniuzi,
  kama vipi nahamia kwa lowassa.
   
 20. m

  macinkus JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Chadema walikwenda kunywa chai tu Ikulu. Picha zinaonyesha wazi jinsi walivyo karimiwa na Rais mwenyewe binafsi. Sasa amekwisha tia saini mazungumzo ya nini tena. Kesho anteua tume, secretariati, hadidu za rejea zilizopitishwa na bunge etc. Mpaka January 2012 atakuwa ametekeleza matakwa yote ya sheria iliyopitishwa na bunge. Shame on Chadema kwa kuiuza nchi kwa kikombe cha chai. Sasa CCM kweli itaendelea kutawala milele. Inasikitisha sana.

  macinkus
   
Loading...