"Katiba, Katiba, Katiba...", msikilize Jaji Warioba kuhusu Katiba mpya

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
7,105
18,005
Wanajukwaa,

Sina maneno mengi. Wanasema kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza. Nchi hii inahitaji wazee wa aina hii ili kupona. Mimi sina cha kuongeza. Sikiliza mwenyewe hapa:

Mama ulibukia huko, kamilisha baraka zako duniani kwa kusimamia taifa kupata Katiba Bora.
 
Hivi wakati wa JPM huyu mzee alikuwa wapi? Mbona sikumsikia hata siku moja akinena ama kushauri kuhusu Katiba mpya? Alinyamaza kimya kabisa, sasa anaibuka na Katiba mpya! Ya Mungu mengi.
 
Mama ulibukia huko, kamilisha baraka zako duniani kwa kusimamia taifa kupata Katiba Bora.
Kisha sema, yeye na uchumi, hilo la Katiba mtajijua wenyewe!

Ashughulikie Katiba bila ya yeye kujuwa ni jinsi gani ataitumia hiyo katiba mpya itamsaidia kuendelea kuwepo madarakani? Katiba mpya kwake haina umuhimu wowote, hadi hapo atakapoona joto linapanda.
 
Hivi wakati wa JPM huyu mzee alikuwa wapi? Mbona sikumsikia hata siku moja akinena ama kushauri kuhusu Katiba mpya? Alinyamaza kimya kabisa, sasa anaibuka na Katiba mpya! Ya Mungu mengi.
Hata kama hukumsikia wewe, huwezi kumlaumu huyo mzee kujikomba kwa Magufuli kwa lolote.

Hajawa na unafiki walio kuwa nao hata hao waliofaidika na kifo cha Magufuli, wanaoimba kazi iendelee, huku wakichimba mikwara gizani.
 
Hivi wakati wa JPM huyu mzee alikuwa wapi? Mbona sikumsikia hata siku moja akinena ama kushauri kuhusu Katiba mpya? Alinyamaza kimya kabisa, sasa anaibuka na Katiba mpya! Ya Mungu mengi.
Kabla ya kuuliza swali ungetuelezea ulichokifanya wewe kama wewe. Yeye yawezekana alisoma alama za nyakati lakini mawazo yake yalikuwa pale pale! Wewe ulifanya nini?
 
Huyu Mzee hakubaliani na CCM, katika kichwa chake kinachomuumiza Roho ; moja ni kukwaama kwa mchakato wa Katiba ambao yeye mwenyewe na kundi lake waliusmamia kwa uelevu wa hali ya juu, lakn chama chake chenye wabunge wengi bungeni Kikaufyekelea mbali.

Pili baada ya kufyekelea mbali matukio makubwa yasiyoitakia mema nchi hasa Uwizi wa Uchuguzi ukiongozwa na Mabegi kichwani ya kura ameyashihudia kinyume na alivotegemea, akiwa Mzee mwenye kaliba ya Mwalimu na aliyefunzwa utu kwa nchi yake hawezi kukubali ubaradhuli huu unaofanywa na Chama chake.

Huyu Mzee ni baba bora anayeuchukia uchafu huu mana Ameishajua mbele msingi wa Taifa umoja, upendo na mshikamano vitapotea na Hatimaye nchi itawaka moto.

Huyu ndye Jaji Joseph Warioba Mzee asiyetetea tumbo lake Bali ustawi wa Nchi yake!!Long live Mzee!!
 
Wewe mwenywe kipindi hicho ulikuwa unajisaidia kwenye kopo usiku ukiogopa kutoka nje. Kwani haujui kuwa tulikuwa na dikteta kipindi hicho? Ulitaka Jaji Warioba afanye nini sasa? Vijana mlijifungia ndani sasa ulitaka mzee wa miaka zaidi ya 80 akufanyie nini? Huyo mzee alifanya mengi sana wakati wa ujana wake.
Hivi wakati wa JPM huyu mzee alikuwa wapi? Mbona sikumsikia hata siku moja akinena ama kushauri kuhusu Katiba mpya? Alinyamaza kimya kabisa, sasa anaibuka na Katiba mpya! Ya Mungu mengi.
 
Wewe mwenywe kipindi hicho ulikuwa unajisaidia kwenye kopo usiku ukiogopa kutoka nje. Kwani haujui kuwa tulikuwa na dikteta kipindi hicho? Ulitaka Jaji Warioba afanye nini sasa? Vijana mlijifungia ndani sasa ulitaka mzee wa miaka zaidi ya 80 akufanyie nini? Huyo mzee alifanya mengi sana wakati wa ujana wake.
Naye mnafiki tu, mbona wakati wa JPM hakujitokeza kusema chochote siku JPM aliposema Katiba haiko kwenye Ilani ya CCM na hivyo hawezi kushughulika na suala la Katiba? Kwani Ilani ya CCM sasa imesema kuwa kuna suala la Katiba mpya? Mzee kama alinyamaza basi na anyamaze tu!
 
Back
Top Bottom