KATIBA: Karimjee & Msekwa Halls kuwa mijadala Aprili 8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KATIBA: Karimjee & Msekwa Halls kuwa mijadala Aprili 8

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Invisible, Apr 6, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 2. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  angalau wafanye muswada mmoja uangukie weekend, hapa wengi watashindwa hudhuria
   
 3. z

  zamlock JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  msekwa ataweza mtiti wake na watu walivyo na hasira na mswaada wa kikwete kutoka kwa moi kenya yani hawa ccm iko siku yao watalia na kusaga meno
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusubiri maoni ya vichwa!
   
 5. Kichwa cha panz

  Kichwa cha panz Senior Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ambao tuko huku mikoani tunawezaje kushiriki mana ni vema na haki tukipata fursa hiyo pia. Tunawezaje kuchangia kwenye mjadala huo?:help:
   
 6. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mikoani sio Tanzania, ni Tanganyika, kwahiyo mtasikiliza Radioni tu maana Bunge nyie haliwajui, linawajua watu wa Dar es salaam na Dodoma tu, Basi!!!!!:love:
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  na hivi wazanzibari si wadau tena katika huu muungano ?
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Usiwe na hofu mta wakilishwa na watu wa Dar es salaam, by the way mpo wachache ni kama 1 ya 8 ya watu wa Dar es salaaam.
  Tulieni munyolewe.
   
 9. e

  emma 26 Senior Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 10. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wasituletee mambo ya Brigedia wa Dowans ya kuchuja watu wa kuingia ukumbini.

  Na tunataka hiyo mijadala iruke hewani na sisi huku kitaa tujiridhishe.
   
 11. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wazanzibari hawana faida yoyote kwa watanganyika.
   
 12. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Hivi hata Mwanza wamepotezea! Wanaogopa eeh! Hatutaki na hatukubali, tutapachimba. They are trying to run away from hard people.
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Tarehe 7 si ni siku ya Karume(sikukuu)?
   
 14. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #14
  Apr 6, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  But tar 7/4 ni Karume day, so kuna kaunafuu...
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  RED BOLD: Tatizo la kusoma heading na kuanza kuchangia bila kujua content, sijui mtu unakuwa na haraka gani kiasi hicho hadi unakosa umakini katika mambo madogo tu kama haya.

  Hata hivyo heading nayo hujaielewa vile vile, hapa unazungumziwa ukumbi wa msekwa-ukumbi wa zamani wa bunge uliopewa jina la msekwa kwa heshima ya spika mstaafu bw.Pius Msekwa.
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Duh,Iam Speechless!
   
 17. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #17
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Nilicheka sana...Jamani JF kuna vituko.Mkuu Mwita,msamehe bure kapitiwa
   
 18. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  wandugu wapendwa,

  habari hii ifuatayo ni mapendekezo ya kutoa kwa wale wataoshiriki kutoa maoni ya kukataa muswada wa uundwaji wa katiba mpya utaofanyika tarehe 7, 8 na 9 April 2011 kuanzia saa 3 asubuhi katika ukumbi wa pius msekwa hall - dodoma,karimjee - dar na zanzibar ukumbi bado kutajwa.

  leo mchana waziri kombani amekutana na kina mama wavaa kanga na vilemba pale white house akiwahimiza kujitokeza kesho pius msekwa hall - bungeni dodoma kusaidia kukubali muswaada ataokuwa ukikusanyiwa maoni

  wanaharakati nao wamekuja na huu, usome na ushiriki plz!!! hali si nzuri

  MAONI YA KUPINGA MUSWADA WA SEREKALI WA UUNWAJI TUME NA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA
  Maoni haya yanatarajiwa kutolewa mbele ya kamati itayokaa siku tatu, kuanzia tarehe 7, 8 na 9 mwezi wa 4, 2011. Maoni haya yatakusanywa na kamati ya bunge ya katiba na sheria katika vituo – Pius Msekwa hall – Dodoma, Karimjee hall Dar es salaam na Zanzibar katika kituo ambacho hakijawekwa bayana. Nia ya serekali ni kupitisha muswada huu hapo tarehe 14 April 2011. WeWE BABA, WEWE MAMA UNAOMBWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUUPINGA MUSWAADA HUU KWA NGUVU ZOTE! Kimsingi, mambo yafuatayo yanaufanya nuswada huu kuwa batili. Muswada huu inabidi ukataliwe kwa ajili ya manufaa ya umma kutokana na vigezo vifuatavyo.
  1. Muswada huu unapaswa usomeke kwa lugha ya kiswahili, lugha ambayo inaweza kueleweka na watoa maoni wote.
  2. Muswada huu unapaswa uwe na uwakilishi kamili wa makundi yote ya jamii. Wawakilishi ambao ni wabunge wanapaswa kupewa muda wa kurudi majimboni mwao na kupata maoni ya wananchi. Kitendo cha kutoa muda mfupi – short notice tangu uliposomwa (5 April 2011) hadi utapopitishwa 14 – 15/April 2011 hautoi fursa ya wabunge kufanya hivyo.
  3. Mamlaka ya raisi yamekuwa makubwa kupita kiasi katika zoezi zima. Raisi ametajwa kuunda tume, kuteua wajumbe, katibu nk.. jumla ya wajumbe imetajwa kuwa ni 30, wajumbe 15 kutoka bara na 15 visiwani. Inapendekezwa kuwa
  a. raisi asiteue tume na shughuli hiyo iachiwe kwa bunge, [FONT=&quot]Mkutano Mkuu wa Katiba (National Conference/congress) [/FONT]au chombo cha wataalamu.
  b. Wajumbe wa tume watoke katika makundi mbalimbali.
  c. Idadi ya watu wa Zanzibar na Tanzania Bara haitoi fursa ya kupata uwakilishi sawa katika tume.
  d. kutokana na kuwepo harufu za udini miaka ya karibuniu kuwe na uwakilishi sawa kwa makundi yote ya kidini
  e. hadidu za rejea zitakazotumiwa katika zoezi zima ziwe zimeainishwa ndani ya sheria / muswada tofauti na ilivyo sasa
  4. Taarifa / matokeo ya tume yasipelekwe kwa raisi kama inavyoainishwa katika muswada huu bali irudishwe kwa watu ndio waseme kama ni sawa au la.
  5. Mfumo wa kukusanya maoni usiwe kupitia ADHOC FORA (majukwaa holela). Kuwe na majukwaaa rasmi ya kutoa maoni na yawe yameainishwa kwenye muswada.
  6. Raisi amesemwa kuwa ataunda bunge la katiba - constitutional assembly kupitia na kupitisha mapendekezo yaliyotolewa na tume. Tunakataa raisi kuunda bunge hili la kupitia mapendekezo kwani bado ni kuendelea kurudisha mamlaka makubwa haya kwa mtu mmoja.
  7. Tume ya uchaguzi imetajwa kusimamia na kuratibu kura za maoni kukubali au kukataa mapendekezo mapya ya katiba baadae kumrejeshea mwanasheria mkuu. – hapa bado ni kurejesha mamlaka kwa raisi. Tume ya uchaguzi haijaweza kuwa huru na haki kuaminiwa kwa jukumu kubwa namna hii kwa taifa.
  8. Pia imekatazwa kwa mtu / kikundi / taasisi chochote kukampaign kwa ajili ya kupigia kura ya ndiyo au hapana kwa katiba itayopendekezwa. Adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili na hakuna faini. Hii haiwezekani kwani imeshaonekana maranyingi watu wakihamasishwa kupiga kura kwa ajili ya kukubali au kukataa katika iliyopendekezwa. Mfano wa hii ni kura ya NDIYO maoni iliyohamasishwa na serekali ya mapinduzi zanzibar kukubali kuundwa kwa serekali ya mseto visiwani mnamo mwaka 2010.
  9. Muswada haujasema muda utaotumika kwa zoezi zima hadi kukamilika. Jambo hili linatoa mwanya kwa mchakato huu wa katiba kuchukua hata miaka 50!! Hili linapaswa liainishwe waziwazi na kama muda usipotosha mara zote bunge litaombwa liongeze muda!
  10. Muswada umeainisha mambo takribani 10 ambayo ni matakatifu na hayapaswi kujadiliwa. Mambo hayo ni kama vile a. uwepo wa bunge b. uwepo wa muungano c. mamlaka ya raisi (executive president) etc etc. huku ni kuwanyima wananchi kuwa huru na utoaji wa maoni. Tunu zozote za taifa ambazo hazitakiwi kujadiliwa zinapaswa kuwa outlined na MKUTANO WA KWANZA WA KATIBA,……

  Mipango ya hila
  1. Kuna mpango wa hila kusema kuwa i. bajeti hii iko sasa tu na haipaswi kuchelewa……..Angalizo ni kuwa sio kila suala linahitaji bunge kukaa, mfano 400 bilioni zilizotolewa kwa ajili ya majenereta hazikupitishwa na bunge, na sio lazima bunge la bajeti tuu lifanye kazi hii……..

  KUNA hoja kuwa fungu la kuendesha zoezi hili litoke kwenye fungu la jumla la serekali (CONSOLIDATED FUND) na sio fungu la bajeti la wizara husika. Ili kuzuia kukwama kwa zoezi.

  2. Kuna mpango wa kuwashawishi wananchi kuwa mchakato wa sasa wa kupitishwa muswaada wa uundwaji wa tume sio kitu cha msingi hivyo waupitishe anyhow! WANANCHI WANAOMBWA KUWA WAANGALIFU NA KUSHIRIKI ZOEZI HILI KIKAMILIFU KATIKA VITUO VILOTAJWA HAPO AWALI

  3. kuna mpango wa kusema wapinzani wanachelewesha uandikwaji wa katiba mpya watapoanza kuhoji umakini unaopendekezwa kutumika na pengine kupendekeza muda uongezwe ili marekebisho yafanyike.. Wananchi wanapaswa kuwaelewa na kukataa ghilba hii!

  Pamoja tuukatae muswaada huu!
  MUNGU IBARIKI AFRIKA!
  MUNGU IBARIKI TANZANIA!
  MUUGUAJI KWA AJILI YA TAIFA
   
Loading...