Katiba inasemaje: Rais akifukuzwa uanachama na chama chake?

Hata akivuliwa Uanachama, atachaguliwa tena kuwa Rais kama uchaguzi utaitishwa tena kwani wananchi walimchagua yeye na siyo chama!
Akivuliwa uanachama anapoteza sifa za kuwa rais. Kama uchaguzi ukiitishwa hata akigombea hata shinda. Wengi wanaipenda CCM. Mfano ninao. Aliyehusika kwenye sakata la ESCROW, alishinda uchaguzi. Chaajabu, yule aliyeibua sakata hilo la escow, alipigwa chini. Kwa kigezo hicho, ni dhahiri wananchi tunawachukia wanaotaka kututoa tulipo kutupeleka mbele. Kama una hoja nzito ya kupingana na mm, iandike hapa
 
Sijui watu wanapepo gani kwasasa lakini ngoja nijibu,
Kikatiba diwani,mbunge pamoja na raisi ni lazima wawe wanachama kutoka katika chama chochote,hivyo endapo atavuliwa uanachama automatic atapoteza nafasi yake ya uraisi
Kwani waliomchagua ni wanachama wa chama chake? By the way kwa sheria ya Tanzania Makamu wa Rais anachukua nafasi hiyo hadi uchaguzi ujao
 
Akivuliwa uanachama anapoteza sifa za kuwa rais. Kama uchaguzi ukiitishwa hata akigombea hata shinda. Wengi wanaipenda ccm. Mfano ninao. Aliyehusika kwenye sakata la escow, alishinda uchaguzi. Chaajabu, yule aliyeibua sakata hilo la escow, alipigwa chini. Kwa kigezo hicho, ni dhahiri wananchi tunawachukia wanaotaka kututoa tulipo kutupeleka mbele. Kama una hoja nzito ya kupingana na mm, iandike hapa
Kwani ni malumbano? Wewe kama umejiona umetoa hoja nzito ni za kwako!
 
Kwa Tanzania uanachama ndio mpango mzima. Malawi yule Mama Joyce Banda alifukuzwa uanachama na chama chake tawala akiwa makamu wa rais, akaendelea kuwa makamu wa rais na akajiunga na kachama kadogo. Baadaye rais wa nchi akafariki, mama akaukwaa urais kiulaini huku akiwa chama tofauti na kilichomuweka madarakani.
 
jibu zuri, asante. sasa tuchukulie hali ya sasa ambapo m/kiti ana nguvu na ushawishi mkubwa kwa chama chake na upande wa pili rais ana dola nyuma yake, ikitokea wawili hawa wakahitilafiana mmoja kwa maslahi binafsi na ya wanaomzunguka na wa pili kwa maslahi mapana ya taifa letu, je m/kiti au rais nani atamuwahi mwenzake? au ni gemu ya kumlia mwenzio timing?
Kimsingi kwa katiba yetu raisi si kitu mbele ya chama,hapa namaanisha chama kinaweza kabisa kumyumbisha raisi.
Mfano tuchukulie mazingira ya sasa ambapo raisi si mwenyekiti kwenye chama chake cha siasa,na huku kwenye chama ambacho raisi anatoka kinaongozwa na mwenyekiti mwingine,kama mwenyekiti anaushawishi ndani ya chama inawezekana kabisa raisi akayumbishwa kwani hakuna raisi bila uanachama na ikumbukwe kua chama ndicho kilichoshikilia uanachama wa raisi.
Kwa msingi huo kama raisi ushawishi wake upo kwenye dola na si chama,kama chama kikiamua kumtunishia misuli raisi,raisi hana ubavu mbele ya chama chake.
 
Diwani,mbunge Na raisi mwenyewe lazima wawe wanachama wa chama cha siasa,hivyo akivuliwa uanachama anapoteza sifa ya kuwepo madarakani.
Ila Kama ilivo ada katiba haisemi chochote kuusu mamlaka yake wakati wa kuendesha mchakato wa uchaguzi,hii inamana utaitishwa uchaguzi yy akiwa madarakani,mazingira ambayo anaweza kuamia chama kingine Na kugombea tena huku akijipa support ya dola kujihakikishia ushindi.
 
Diwani,mbunge Na raisi mwenyewe lazima wawe wanachama wa chama cha siasa,hivyo akivuliwa uanachama anapoteza sifa ya kuwepo madarakani.
Ila Kama ilivo ada katiba haisemi chochote kuusu mamlaka yake wakati wa kuendesha mchakato wa uchaguzi,hii inamana utaitishwa uchaguzi yy akiwa madarakani,mazingira ambayo anaweza kuamia chama kingine Na kugombea tena huku akijipa support ya dola kujihakikishia ushindi.
 
Akivuliwa uanachama anapoteza sifa za kuwa rais. Kama uchaguzi ukiitishwa hata akigombea hata shinda. Wengi wanaipenda CCM. Mfano ninao. Aliyehusika kwenye sakata la ESCROW, alishinda uchaguzi. Chaajabu, yule aliyeibua sakata hilo la escow, alipigwa chini. Kwa kigezo hicho, ni dhahiri wananchi tunawachukia wanaotaka kututoa tulipo kutupeleka mbele. Kama una hoja nzito ya kupingana na mm, iandike hapa

nimekuelewa kidogo, kwa mfumo wa siasa za nchi yetu chama tawala kina nguvu kuliko rais, hapo kweli m/kiti ni kama bosi wake hadi pale atakapomkabidhi kijiti.
 
Diwani,mbunge Na raisi mwenyewe lazima wawe wanachama wa chama cha siasa,hivyo akivuliwa uanachama anapoteza sifa ya kuwepo madarakani.
Ila Kama ilivo ada katiba haisemi chochote kuusu mamlaka yake wakati wa kuendesha mchakato wa uchaguzi,hii inamana utaitishwa uchaguzi yy akiwa madarakani,mazingira ambayo anaweza kuamia chama kingine Na kugombea tena huku akijipa support ya dola kujihakikishia ushindi.
 
Kisheria iko hivi: Sifa zinazohitajika ili mtu kustahili ( to qualify) kugombea urais zimeahinishwa kwenye Ibara ya 39 ya Katiba na baadhi ya hizo sifa ni kuwa awe na miaka zaidi ya 40, awe na adhaminiwe na chama, awe raia wa Tz, na asiwe amehukumiwa na kosa la ukwepaji kodi, na pia awe na sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge. Hizi sifa ni lazima mtu awe nazo na zinakaguliwa na Tume ya Uchaguzi siku ya uteuzi.

Katiba vile vile chini ya Ibara ya 42 (3) inaweka wazi muda ambao rais atadumu ofisini kuwa ni miaka mitano isipokuwa atakapokufa au atakapojiuzulu kabla ya hiyo miaka mitano. Asipokufa au kujiuzulu atakuwa rais mpaka pale rais mwingine atakapokula kiapo au atakapokoma kuwa rais kwa mujibu wa Katiba. Sasa pamoja na hizo sababu zilizowekwa moja kwa moja(expressly) kwenye Ibara hii ni wazi kuwa Ibara hii haijaweka sababu zote ambazo zitapelekea rais kukoma kuwa rais. Kwa mfano haijataja rais kuondolewa na Bunge kwa impeachment ambayo ipo chini ya Ibara ya 46A na hii itatafsiriwa kama mojawapo ya sababu ya rais kukoma kuwa rais kwa mujibu wa Katiba ambayo imewekwa kwenye Ibara ya 42 (3) (d).

Kwa mfano inagundulika baada ya rais kuchaguliwa kuwa yeye sio raia halali wa Tz sidhani kama itakuwa halali kusema kuwa atabaki tu kuwa rais kwa sababu hiyo sababu haijawekwa kwenye Ibara 42 ya Katiba ambayo ndo inaweka ukomo wa urais. Hii itakuwa ni sawa na pale anaponyang'anywa uanachama na hivyo kupoteza sifa za kuwa rais. Kwa hiyo Ibara ya 42 ni lazima isomwe pamoja na Ibara ya 39 ya Katiba.

Kwa hiyo CCM wakichukua kadi yao Magufuli atapoteza sifa za kuwa rais kama ilivyoelezwa hapo juu.

Am a forth year student pursuing law degree but I stand to be corrected.
 
Diwani,mbunge Na raisi mwenyewe lazima wawe wanachama wa chama cha siasa,hivyo akivuliwa uanachama anapoteza sifa ya kuwepo madarakani.
Ila Kama ilivo ada katiba haisemi chochote kuusu mamlaka yake wakati wa kuendesha mchakato wa uchaguzi,hii inamana utaitishwa uchaguzi yy akiwa madarakani,mazingira ambayo anaweza kuamia chama kingine Na kugombea tena huku akijipa support ya dola kujihakikishia ushindi.
namshauri m/kiti amkabidhi kijiti rais mapema iwezekanavyo, ili kuepusha msuguano wa kimaslahi baina yao.
 
Akivuliwa uanachama anapoteza sifa za kuwa rais. Kama uchaguzi ukiitishwa hata akigombea hata shinda. Wengi wanaipenda CCM. Mfano ninao. Aliyehusika kwenye sakata la ESCROW, alishinda uchaguzi. Chaajabu, yule aliyeibua sakata hilo la escow, alipigwa chini. Kwa kigezo hicho, ni dhahiri wananchi tunawachukia wanaotaka kututoa tulipo kutupeleka mbele. Kama una hoja nzito ya kupingana na mm, iandike hapa
Sina
 
Kikatiba nafasi ya urais inakomaje
Kikatiba kiti cha urais kitakuwa wazi, pamoja na sababu zingine zilizoorodheshwa, kwa matakwa ya mjadala huu katiba ina kipengele kinasema nafasi itakuwa wazi iwapo rais atapoteza sifa zilizomuwezesha kuchaguliwa kuwa Rais.

Sasa sifa kuu inayomfanya mtu aweze kugombea na kuchaguliwa kuwa Rais ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichomteuwa. Kuipoteza hii sifa na urais unafikia mwisho wake
 
Kwa nini wamfute uanachama?hao walokua wanasema hayo hawajitambui na yamkini walikua wamepombeka,ccm kundi la watu wengi sana,na wapo ambao wana uchungu na nchi na sisi wananchi tulivyo na ugumu wa maisha,sasa walioshindwa kuongoza kama anavyoongoza JPM hawawezi shangaa na hawawezi mfuta huyo mtu uanachama kwa sababu siyo ccm wote ni watovu wa nidhamu,wapo watakaomtetea kwa utendaji wake,wenye kutenda ktk haki,kwa hyo kuwaza kua kuna siku Rais watamfuta uanachama ni kujifikirisha tu kusiko na majibu ya wakifikiliacho!
Mjadala nadhani ulitaka kujua sheria inasemaje na wala sio kuwa hilo tukio litatokea
 
Kikatiba kiti cha urais kitakuwa wazi, pamoja na sababu zingine zilizoorodheshwa, kwa matakwa ya mjadala huu katiba ina kipengele kinasema nafasi itakuwa wazi iwapo rais atapoteza sifa zilizomuwezesha kuchaguliwa kuwa Rais.

Sasa sifa kuu inayomfanya mtu aweze kugombea na kuchaguliwa kuwa Rais ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichomteuwa. Kuipoteza hii sifa na urais unafikia mwisho wake
that's a very good and valid point, akivuliwa uanachama........urais kwishney.....jipu kuu haliwezi tumbuliwa......coz hata akiwa m/kiti bado anaweza undiwa zengwe akavuliwa uanachama.
 
1461360844221.jpg

Nauliza, leo naomba mnifae, mbunge akivuliwa uanachama wa chama kilicho mdhamini anapoteza ubunge, vipi kwa upande wa rais akivuliwa uanachama?

Mwenge ni jambo lilokuwa la kitaifa na lenye kuheshimiwa sana, lakini kwasasa limeonekana la kichama zaidi ingawa kiukweli bado ni suala la kiserikali na la nchi.

Rais wetu anapambana matumizi yaso na lazima na ni mfano bora kwa kupiga vita matumizi hayo na tumepata rais mwenye kupenda kujikita katika matumizi ya maendeleo. Hakika tuna kila sababu kuiga mfano wake hata katika maisha ya ndani ya familia zetu.

Hata hivyo, nikitazama hili suala hili la mwenge, na nikizingatia uthubutu wake wa kufuta sherehe za zilizo zoeleka za uhuru na muungano, na nikizingatia mwenge unazunguka nchi nzima kwa magari na posho kwa wakimbiza mwenge huku zikianza kwa sherehe na kuhitimishwa kwa sherehe, nina lazimika kuhisi kuwa rais wetu anajua kuwa mbio za mwenge JIPU lakini hana hila wala njia ya kulitumbua kwasasa.

Akijaribu hilo ataungwa mkono na wananchi, lakini atapata upinzani mkubwa ndani ya chama chake, chama ambacho bado kina amini kuwa mwenge ni jambo muhimu, kilelezo cha uhuru wetu na mbio zinazo hitaji kuendelea kudumishwa vizazi na vizazi bila kukoma.

Rais anaweza kuamua kulitumbua, lakini akifanya hivyo anaweza kuvuliwa uanachama wa CCM, na hapo ndipo inapokuja hoja yangu, nini kitatokea endapo rais aliye madarakani akivuliwa uanachama? Hivi kati ya mambo yanayo mfanya rais apoteze urais hili ni moja wapo? Kama urais utakuwa katika hatari ndio maana mwenyekiti wa sasa atachia ngazi mapema ili kumuhakikishia Magufuli urais wake?

Wabunge wetu hawako huru sababu katiba inawafanya kuwa watumwa wa chama badala ya watumwa wa wananchi, naogopa sana kama katiba yetu pia ina muweka rais wetu katika utumwa huo, utumwa kwa chama badala kwa wananchi. Tunahitaji katiba yetu ifungue pingu au minyororo hii ya utumwa kwa wabunge wetu na viongozi wengine wanao patikana kwa dhamana ya chama cha siasa.

Niko na imani wabunge wa CCM wanajua mbio za mwenge JIPU, hata rais huenda anajua pia kuwa mbio za mwenge JIPU, lakini hawana namna sababu CHAMA bado hakijaona kuwa kuna haja ya kuuweka mwenge katika jumba la makumbusho. Kama wangekuwa si watumwa wa chama, mwenge ungekuwa historia.

Mwisho poleni walimu, lakini mwisho kabisa, kauliza muulizaji, kama mwenge unazindua miradi ya maendeleo, kwanini mwenge hujazindua daraja la mwalimu Nyerere?

whatsapp/call 0622845394
 
Back
Top Bottom