Katiba inasemaje: Rais akifukuzwa uanachama na chama chake?

Hatua yeyote ya ccm kumuwekea kauzibe magufuri ili apunguze makali kwa manufaa yao hatukubari.tuko tiyari kuwapigsa mawe wale wanaccm wanaotuibia hasa wale wenye mavipara na vitambi vikubwa
 
Kwa nini wamfute uanachama?hao walokua wanasema hayo hawajitambui na yamkini walikua wamepombeka,ccm kundi la watu wengi sana,na wapo ambao wana uchungu na nchi na sisi wananchi tulivyo na ugumu wa maisha,sasa walioshindwa kuongoza kama anavyoongoza JPM hawawezi shangaa na hawawezi mfuta huyo mtu uanachama kwa sababu siyo ccm wote ni watovu wa nidhamu,wapo watakaomtetea kwa utendaji wake,wenye kutenda ktk haki,kwa hyo kuwaza kua kuna siku Rais watamfuta uanachama ni kujifikirisha tu kusiko na majibu ya wakifikiliacho!
Msaada unaotakiwa kutupatia ni you just imagine imekua hivo japokuwa unaamini haiwezi kua hivo je, Katiba na sheria vinasemaje?
 
Hatua yeyote ya ccm kumuwekea kauzibe magufuri ili apunguze makali kwa manufaa yao hatukubari.tuko tiyari kuwapigsa mawe wale wanaccm wanaotuibia hasa wale wenye mavipara na vitambi vikubwa

Hayo majamaa uliyoyataja achana na fikra ya kuyapiga mawe, tusifike huko japo ikibidi tutafika swali ni kwamba ikitokea yakamfuta uanachama je, katiba na sheria za nchi vinasemaje? Tusaidie.
 
Vikao vya CCM wiki ijayo vina agenda gani.? Kwanza tujuze.?
Magufuli ni mmoja wa wahudhuriaji.?
Sijui agenda, pia sijui ikiwa Tingatinga atakuepo au hatakuepo ila nisaidie kujua katiba inasemaje akifutwa uanaccm watz tutakuwa tumempoteza na kulazimishwa kutafuta Tingatinga mwingine au wanakua wamechemka bado kunakuwa na mzunguuko wa kuweza kumlinda?
 
Mafisadi wote ndani ya ccm watamfuata fisadi mwenzao aliyekatwa.

salamu za kwa mzee wa pumzi hafifu aka Kingungue

Just imagine mafisadi uliyoyataja yamefanikiwa kumfuta uanaccm, je kuna jinsi ya kufanya aendelee kuongoza au kumfuta uanaccm ndo mwisho wa uraisi wake hakuna hatua nyingine?
 
Katiba imetaja wazi sababu za mtu aliye rais kukoma kuendelea kuwa rais. Na hiyo uliyoitaja haipo. Hivo basi kumfuta uanachama hakumvui urais. Hakuna zaidi.
 
Mtaani kwenu bado mnajadili siasa? Hamna shughuli za kufanya?
 
Me nadhani Swala na hoja ya msingi haijibiwa!!!,mfano zito alipofukuzwa chadema na ubunge wake ukakoma japo alikuwa Mbunge wa Kigoma na sio chadema peke yake!,

je ikotokea raisi uana Chama wake ukasitishwa kwa Chama alichoteuliwa nacho,
nini kinatokea kulingana na katiba n Sheria za nchi???!
 
Mafisadi wote ndani ya ccm watamfuata fisadi mwenzao aliyekatwa.

salamu za kwa mzee wa pumzi hafifu aka Kingungue
mbona huyu fisadi assadsyria3 anampinga magu huku akiwa ndani ya chama???
Nini kimetokea huko chamani???mana wanachama wengi wanamchukia magu sasa hivi,
Nasikia ukisikika unaimba wimbo wa sisiem mbele kwa mbele unashughulikiwa na chama
 
Last edited by a moderator:
Tegemea lolote kwa hao jamaa, usitimie kichwa na logic kufikiri ndio utaelewa CCM Ni watu wa aina gani.
Mfano katiba ya Warioba.
Mfano mwingine ni safari za Raisi nje ya nchi kuwa zinatija kwa taifa, baada ya masaa tu hazina tija. Baada ya Magu, sasa ni tishio wanataka azirudishe!!!!
 
Hayo majamaa uliyoyataja achana na fikra ya kuyapiga mawe, tusifike huko japo ikibidi tutafika swali ni kwamba ikitokea yakamfuta uanachama je, katiba na sheria za nchi vinasemaje? Tusaidie.

Ukishakuwa Rais umekuwa Mkuu wa nchi. Na kwa katiba yetu hakuna tena mtu yeyote aliejuu yako. Unakuwa amiri jeshi Mkuu wa majeshi yote ya JMT. Katiba haizungumzii tena suala la uanachama. Kuhusu kukoma Urais katiba imetaja sbb zinazoweza kumuondoa raisi madarakani na zote lazima ziridhiwe na bunge. Unajua kuwa secondary representative ya Wananchi ni bunge. Mambo yenyewe ni kifo ugonjwa nk. Kumuondoa raisi maana yake umejiondoa ww pia. Atakae itisha uchaguzi ni huyo huyo raisi mliemuondoa madarakani. Wakati ww sio mbunge mwenzako anakuwa rais mpaka raisi mpya atakapoapishwa. Kiuharisia kumuondoa madarakani raisi wa JMT wakati bado ana uwezo wa kuongoza ni kujimaliza ww mwenyewe kuliko kummaliza raisi
Pili chama kikimfuta uanachama haina uhusiano na Urais wake. Anaendelea kuwa rais na anaweza kujiunga na chama kingine akiwa bado rais. Ukimfuta rais uanachama maana yake halisi umekipokonya au umekiondoa chama chako madarakani. Yaan umekiua chama. Kitakosa mawaziri na hatimae kitakufa.
Mkuu lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Kwa sababu hiyo hata kama hawapendezwi na aina ya uongozi wa Magufuli hawana namna lazima wakubali.
Kwanza mimi naamin kuwa kwa chama kama cha Ccm kilichoshehen wasomi waliobobea walimchagua Magufuli wakiwa wanaelewa nn kitatokea. Haikuwa bahati mbaya. Hii ilijulikana tangu mwanzo na pengine Magufuli hayuko speed sana kama wanavotaka. Hii ni renovation ya lazima kama kweli wanataka ccm iendelee kutawala vinginevyo ccm itaelekea kule kanu unip na upn cha malawi viliko.
 
Bado mnaweweseka na ushindi wa Mr President? Poleni sana. Imetoka hiyo. Gear ya angani imeangusha ndege abiria wote wamekufa
 
Kuwa Mwanachama wa Chama cha Siasa ni matakwa ya kikatiba hivyo kwa viongozi wa kisiasa pamoja na mambo mengineyo endapo watakoma au kufutwa uanachama wa Chama alichokuwapo wakati anachaguliwa katika nafasi hiyo basi ndiyo ukomo wake wa kuitumikia nafasi hiyo unakuwa umefika, 1984 Alhaji Aboud Jumbe baada ya kufutwa uanachama wa ccm na nafasi yake ya urais wa Zanzibar akaipoteza.
 
Ukishakuwa Rais umekuwa Mkuu wa nchi. Na kwa katiba yetu hakuna tena mtu yeyote aliejuu yako. Unakuwa amiri jeshi Mkuu wa majeshi yote ya JMT. Katiba haizungumzii tena suala la uanachama. Kuhusu kukoma Urais katiba imetaja sbb zinazoweza kumuondoa raisi madarakani na zote lazima ziridhiwe na bunge. Unajua kuwa secondary representative ya Wananchi ni bunge. Mambo yenyewe ni kifo ugonjwa nk. Kumuondoa raisi maana yake umejiondoa ww pia. Atakae itisha uchaguzi ni huyo huyo raisi mliemuondoa madarakani. Wakati ww sio mbunge mwenzako anakuwa rais mpaka raisi mpya atakapoapishwa. Kiuharisia kumuondoa madarakani raisi wa JMT wakati bado ana uwezo wa kuongoza ni kujimaliza ww mwenyewe kuliko kummaliza raisi
Pili chama kikimfuta uanachama haina uhusiano na Urais wake. Anaendelea kuwa rais na anaweza kujiunga na chama kingine akiwa bado rais. Ukimfuta rais uanachama maana yake halisi umekipokonya au umekiondoa chama chako madarakani. Yaan umekiua chama. Kitakosa mawaziri na hatimae kitakufa.
Mkuu lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Kwa sababu hiyo hata kama hawapendezwi na aina ya uongozi wa Magufuli hawana namna lazima wakubali.
Kwanza mimi naamin kuwa kwa chama kama cha Ccm kilichoshehen wasomi waliobobea walimchagua Magufuli wakiwa wanaelewa nn kitatokea. Haikuwa bahati mbaya. Hii ilijulikana tangu mwanzo na pengine Magufuli hayuko speed sana kama wanavotaka. Hii ni renovation ya lazima kama kweli wanataka ccm iendelee kutawala vinginevyo ccm itaelekea kule kanu unip na upn cha malawi viliko.

Nmekuelewa sana wee jamaa
 
Back
Top Bottom