Katiba inasema nini kuhusu kuhusu kura zilizo haribika

amanij

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
353
198
Watanzania na wataalamu wano fahamu mahesabu na sharia.

Kati uchaguzi matokeo hujumlishwa na kutolewa; ninacho uliza ni kuhusu kura zilo haribika zimo katika kuhesabiwa au hutolewa kabisa.

Katika uchaguzi wa Zanzibar 1995.

Salmin alipata 50.2% ya kurahalali (165271) na

Maalim Seif alipata 49.8% (163706) kura halali lakini kura zilizo haribika hazikutiwa hesabuni.


Voting statistics ya 1995

Walojiandikisha 348934
Walopiga kura 333899
% Turnout 95.69

Kura zilizoharibika zina kuwa sihalali lakini zimo katika jumla ya kura zote zilo pigwa

Kwanini kwa sababu ; asilimia ya kura zilo haribika zinge zingatiwa basi hakuna mgombea aliyevuka asilimia 50%

Mfumo huu umeendelea mpaka sasa. Hii na sawa !!!

Salmin 165271 49.5%
Maalim seif 163706 49.03%
Kura zilzo haribika 4922 1.47 %

Jumla 333899 100%

Mfumo huu umeendelea mpaka sasa. Hii na sawa !!! Au ndio katiba ina sema hivyo?
 
Kwa mujibu wa Katiba zote ya Zanzibar na Tanzania, Katiba zimeipa mamlaka Tume ya Uchaguzi kwa eneo husika (Zanzibar na Tanzania) kama chombo / taasisi huru, kuanda na kusimamia mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi mdogo.

Sasa katika kutekeleza majukumu yake, Tume ya Uchaguzi imeweka utaratubu wa namna ya kuhesabu kura, ambapo kura zote (ambazo hazijaaribika na zilizo haribika) zilizotumika katika upigaji kura katika kila nafasi ya Ugomboa (Ubunge, Urais na Udiwani).

Baada ya kujua idadi ya kura zote zilizotumika katika kila nafasi, ndipo utambuaji / uchambuaji wa kura kwa kila mgombea kufanyika sambamba na kutenga kando kura zote zilizo haribika katika nafasi husika ya Ugombea (Ubunge, Udiwani na Urais).

Kisha kura za wagombea wa nafasi moja (Ubunge au Udiwani au Urais) huesabiwa na kumpata mshindi na pia kura zilizo haribika katika nafasi hiyo husika ya Ugombea hutangazwa.

Hivyo, kura zilizoharibika huwa haziesabiwi kwa mgombea, kama hilo limefanyika na ushahidi unao nenda Mhakamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom