Wakati na muda
wa kushika
madaraka ya
Rais
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9
42.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema
iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa
kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla
ya kupita siku saba.
(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtu
aliyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katika
ibara ndogo ya (3), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miaka
mitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais.
(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-
(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti
hicho atakula kiapo cha Rais; au
(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka;
au
(c) siku atakapojiuzulu; au
(d) atakapoacha kushika kiti cha Rais kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii.
Au wanatumia kifungu hichi, kuwa rais aliyechaguliwa ataendelea kuwa rais hadi rais mpya atakapo apishwa