Katiba inaonesha Rais akiwa nje ya nchi majukumu yanabaki kwa Makamu. Kwanini Rais anatoa 'press' akiwa nje?

..Yes, I am serious.

..I am not afraid of "making fun of myself" from time to time, otherwise how would I learn?

..Vinginevyo hebu tufafanulie ni mambo gani Rais anaweza kufanya na kutofanya anapokuwa nje ya nchi.

..Je, taarifa za uteuzi kutoka wakati Raisi yuko nje ya nchi, ni lazima imaanishe kwamba amefanya uamuzi huo akiwa nje ya nchi.

..Hakuna uwezekano kwamba alishaamua, isipokuwa taarifa ndio zilichelewa kutoka?

..Je, unadhani VP Dr.Mpamgo ndio alipaswa kuteua na taarifa iseme " kaimu Raisi amewateua ..." ?

..Ngoja tuwashirikishe wanasheria wetu hapa JF Pascal Mayalla, Petro E. Mselewa .

Action hutambulishwa na vitu vitatu: who, where, and when. Ukisoma press release utaviona hivyo vitu. Who: Samia; Where: Washington, D.C.; When: April 14, 2022.

Yes, kuna urgency, acting president (VP Dr. Mpango) angeweza kufanya hivyo. Vinginevyo, hilo lingeweza kumsubiri yeye Samia arudi.

Yapo majukumu mengi muhimu ambayo yamewahi kufanywa na acting presidents at different times. Kwa mfano, kuna miswada ya sheria kadhaa (ambayo nimewahi kuiona) iliyosainiwa kuwa sheria kamili na Judge Warioba (alipokuwa anakaimu kiti cha Rais)!
 
Rais wa Tanzania anapata wapi uhalali wa kujifanya kwamba yeye ni indispensable (unsubstitutable)? Kwamba Tanzania bila yeye haiwezi kitu chochote?

Kwa mara nyingine tena, nimeona Chifu Hangaya (akiwa Washington, DC) amefanya uteuzi wa viongozi watatu, kama press release niliyoambatanisha inavyoonesha. Kama kawaida anaendelea na ukiukaji wa Katiba yetu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 47(1)(c) ya Katiba yetu, Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Na kwa mujibu wa Ibara ya 37(6)(b) ya Katiba hiyo hiyo, ili Rais ahesabike kuwa yuko nje ya nchi, lazima awe nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne.

Ingawa Ofisi ya Rais wa JMT yaweza kuwa mahali popote ndani ya mipaka ya JMT, katu haiwezi kuwa mahali popote tu duniani, kama Chifu Hangaya anavyotaka kuifanya. Ni lazima iwe ndani ya mipaka ya nchi yetu.

Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Period. Why is she so insecure?

Hivi, Katiba ya Tanzania ipo ili itusaidie, kama kila uchao inasiginwa na wale walioapa kuilinda?

View attachment 2188837
Wa kulaumiwa Nyerere na muungano wake
 
Maccm ya kule kwa Tulia ndio wafanye impeachment? Amino ww unaona mbali sn, wale mapimbi kule Dom hayana akili kbs, hebu yachape fimbo mpk yapate akili.

Hata impeachment trials za US presidents huvaliwa njuga na wale wasiokuwa washirika wao, huku washirika wao wakiendelea kuwakumbatia.

Impeachment, by design, ni kibarua kigumu sana. Washirika wa Rais huwa hawatilii maanani ushahidi unaowasilishwa. Ndiyo maana, katika historia ya Marekani, hakuna Rais hata mmoja ambaye amewahi kuwa impeached and convicted at trial. Conviction inawezekana tu iwapo wapinzani wanashikilia at least 2/3 ya viti vya chombo kinachohusika!
 
Tatizo ni kuwa hata ukikaimu nafasi ya urais, huwezi kutengua au kuteua.
Unakuwa na cheo tu kisicho na meno.
 
..Yes, I am serious.

..I am not afraid of "making fun of myself" from time to time, otherwise how would I learn?

..Vinginevyo hebu tufafanulie ni mambo gani Rais anaweza kufanya na kutofanya anapokuwa nje ya nchi.

..Je, taarifa za uteuzi kutoka wakati Raisi yuko nje ya nchi, ni lazima imaanishe kwamba amefanya uamuzi huo akiwa nje ya nchi.

..Hakuna uwezekano kwamba alishaamua, isipokuwa taarifa ndio zilichelewa kutoka?

..Je, unadhani VP Dr.Mpamgo ndio alipaswa kuteua na taarifa iseme " kaimu Raisi amewateua ..." ?

..Ngoja tuwashirikishe wanasheria wetu hapa JF Pascal Mayalla, Petro E. Mselewa .
Mkuu JokaKuu , nashukuru kwa kunialika kwenye mjadala huu. Kikatiba, teuzi zilizofanyika hufanywa na Rais tu. Katiba haijasema popote kuwa Kaimu Rais anaweza kufanya uteuzi huo. Kimsingi, Kaimu hukaimu mambo mengineyo lakini si kwa hayo. Ndiyo maana, Rais anafanya teuzi akiwa huko Marekani. Amesafiri na 'mamlaka yake'.
 
Mashitaka ya Rais (impeachment trial) inaendeshwa na Bunge. Bila kuwa na wabunge wa upinzani wa kutosha Bungeni, hata azimio tu la kumshitaki Rais haliwezi kupita.

Katibu wa bunge akiwa wapi boss? Jua katibu wa bunge ndio msimamizi wa bunge na yeye ni mteuliwa wa rais.
 
..Tunatakiwa tujiulize maswali haya:-

1. Je, Raisi hayuko kazini?

2. Je, Raisi yuko nje ya nchi?

..Kwa maoni yangu, Makamu wa Raisi anapokaimu atatekeleza mambo ambayo utekelezaji wake unahitaji uwepo wa Raisi "PHYSICALLY."

..Kwa mfano, tendo la kuapisha Wateuliwa linaweza kufanywa na Makamu wa Raisi as Acting President. Lakini sidhani kama Acting President anaweza kuteua.

..Makamu wa Raisi ambaye ni Acting President anaweza kusaini mswada kuwa sheria, lakini sidhani kama anaweza kusaini mswada ambao Raisi mwenyewe hajiuridhia.

..Tukirudi kwenye teuzi za Raisi, suala hilo huwa ni mchakato, na tangazo linapotoka mara nyingi ni kuwa Rais alishiriki ktk hatua mbalimbali na alishatoa uamuzi.

..Mwisho, Ssh yuko ktk ziara nchini Marekani. Yuko nje kwa zaidi ya MASAA 24, je ina maanisha Ssh huko aliko amekuwa sio Raisi wa Tanzania?

..Nadhani mtoa mada alitakiwa kusoma vifungu vya katiba zaidi ya hivi alivyovileta, na zaidi kudurusu waandishi wa katiba yetu walilenga nini walipoandika kifungu kinachohusiana na Kukaimisha nafasi ya Raisi.

Cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Petro E. Mselewa , Pulchra Animo

Dude, kutoa maoni ambayo hayana legal basis ni kupoteza muda wa watu. Tuletee ibara za Katiba ambazo unazitumia kama basis ya maoni yako.

Kama acting president anafanya tu vitu ambavyo president alikuwa amesharidhia, kwani hilo la teuzi linashindikana kuwa na sura hiyo hiyo? Mwenyewe umeshasema uteuzi ni mchakato.
 
Hiyo kazi ya tour wangewapa hata timu ya basketball hapo USA waizindue lakini Rais kufunga safari mpaka Marekani huko ni kupoteza fedha zetu bure tu.

Rwanda waliwapa kazi Arsenal na walipata coverage nzuri.

Rais alipaswa kwenda kunegotiate na producers wa Oil huko tupate bei nzuri ili hali ya maisha itengamae lakini ndio kwanza wanamweka busy na mambo mepesi mepesi tu.
Tumepigwa, hapa hatuna rais
 
Mkuu JokaKuu , nashukuru kwa kunialika kwenye mjadala huu. Kikatiba, teuzi zilizofanyika hufanywa na Rais tu. Katiba haijasema popote kuwa Kaimu Rais anaweza kufanya uteuzi huo. Kimsingi, Kaimu hukaimu mambo mengineyo lakini si kwa hayo. Ndiyo maana, Rais anafanya teuzi akiwa huko Marekani. Amesafiri na 'mamlaka yake'.

Mkuu Mselewa, hii delineation umeipata wapi kwenye Katiba?

Ibara ya Katiba ya JMT inayotoa mwongozo wa utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais ni Ibara ya 37. Yapo mambo ambayo ibara ndogo ya 10 ya ya Ibara hii imemkataza (expressly) Kaimu Rais kuyafanya. Ibara hiyo ndogo inasema hivi:

Bila ya kujali masharti yaliyoelezwa hapo awali katika ibara hii, mtu atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais, kwa mujibu wa ibara hii hatakuwa na madaraka ya kulivunja Bunge, kumwondoa yeyote kati ya Mawaziri katika madaraka yake au kufuta uteuzi wowote uliofanywa na Rais.
 
Aliyekua Mbunge wa Arusha Godbless Lema kachangia pia kuimaliza Arusha kwa kuchochea vurugu na maandamano ya kijinga.

Yuko wapi sasa?? Haya ndio matatizo ya kuendekeza siasa za kijinga kama za Lema na wenzake.

Rwanda huwezi kuta maandamano ya kijinga kama Lema aliyokuwa akiyahamasisha.

Tangu 2015, nitajie lini Lema alifanya maandamano Arusha. Maandamano ya 2011 mpaka leo unayahesabu. Acheni kunuficha kwenye hakuna.
 
Wale matendo yao kwa asilimia 100 yanategemea ushauri anaopewa. Akipata mshauri mbovu imekula kwenu. Eva alishauriwa na Ibilisi na matokeo yake kila mtu anayajua!
Hakika mkuu
b8b1c0d9d755c3cd45483f6fddf15193.jpg
headless.jpg
 
Thubutu, yule ndio hasa anasimamia nini kijadiliwe bungeni. Kama ulikuwa hujui ujue sasa.

Katibu wa Bunge angekuwa all that powerful angemnusuru hata Lowassa enzi zile za sakata la Richmond. Cabinet ya JK iliambulia kuvunjika.

Soma vizuri Kanuni za Kudumu za Bunge. Katibu wa Bunge sio mbunge; anafanya shughuli za kiutawala Bungeni (ikiwemo kutunza kumbukumbu zinazotakiwa za proceedings za Bunge) na kutoa ushauri wa kiufundi when and as needed.

Kuhusu impeachment ya Rais, soma Ibara ya 46A ya Katiba yetu!
 
Rais akiwa nje hawezibkutekeleza majukumu yake.

..Je, akiwa nje ya mipaka anakuwa sio Raisi tena, na hawezi kutekeleza majukumu yake?
 
Katibu wa Bunge angekuwa all that powerful angemnusuru hata Lowassa enzi zile za sakata la Richmond. Cabinet ya JK iliambulia kuvunjika.

Soma vizuri Kanuni za Kudumu za Bunge. Katibu wa Bunge sio mbunge; anafanya shughuli za kiutawala Bungeni (ikiwemo kutunza kumbukumbu zinazotakiwa za proceedings za Bunge) na kutoa ushauri wa kiufundi when and as needed.

Kuhusu impeachment ya Rais, soma Ibara ya 46A ya Katiba yetu!

Lowassa alitolewa kafara, ukiona mjadala umeruhusiwa huko bungeni basi ujue serekalini imeafiki.
 
Maraisi wengi wa Africa ni waoga sana na inafika wengine wakiwa hata hospitali nchi za nje ila bado wanaendelea kutoa maelekezo ya moja kwa moja

Nakumbuka wengi tu baadhi wanaaga Bunge kama Buhari na wengine huwa wanaondoka tu na kuanza kutuma vi memo
Cheza na madaraka ya kiafrika? Huwa hawaamini wamefika hapo

Ila kwa kuwapa watu shavu akiwa nje ni kosa kwani hana Makamu?
Hata kuteua jamani
Lakini sishangai hata mtangulizi wake alijibatiza vyeo kibao
 
Rais wa Tanzania anapata wapi uhalali wa kujifanya kwamba yeye ni indispensable (unsubstitutable)? Kwamba Tanzania bila yeye haiwezi kitu chochote?

Kwa mara nyingine tena, nimeona Chifu Hangaya (akiwa Washington, DC) amefanya uteuzi wa viongozi watatu, kama press release niliyoambatanisha inavyoonesha. Kama kawaida anaendelea na ukiukaji wa Katiba yetu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 47(1)(c) ya Katiba yetu, Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Na kwa mujibu wa Ibara ya 37(6)(b) ya Katiba hiyo hiyo, ili Rais ahesabike kuwa yuko nje ya nchi, lazima awe nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne.

Ingawa Ofisi ya Rais wa JMT yaweza kuwa mahali popote ndani ya mipaka ya JMT, katu haiwezi kuwa mahali popote tu duniani, kama Chifu Hangaya anavyotaka kuifanya. Ni lazima iwe ndani ya mipaka ya nchi yetu.

Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Period. Why is she so insecure?

Hivi, Katiba ya Tanzania ipo ili itusaidie, kama kila uchao inasiginwa na wale walioapa kuilinda?

View attachment 2188837
Acha hangaya,hata nyerere alikuwa anafanya hivyo,elewa mamlaka ya uteuzi ni ya rais tu huwa hayakaimiwi
 
Lowassa alitolewa kafara, ukiona mjadala umeruhusiwa huko bungeni basi ujue serekalini imeafiki.

Sidhani kama wewe ulikuwa unalijua Bunge la Speaker Sitta. Unajua kwanini Speaker Sitta hakupitishwa tena kugombea kiti cha Speaker baada ya uchaguzi mkuu uliofutia?
 
Back
Top Bottom