Katiba Imevunjwa? Nini kifanyike?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
24,474
34,512
Ibara ya 68 Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inasema;
Nanukuu: "Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa." mwisho wa kunukuu​


Ibara ya 55 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ibara ndogo ya (4) inasema:
Nanukuu: "Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge". Mwisho wa kunukuu​


Uteuzi wa hivi karibuni wa Mheshimiwa rais kwa wabunge ambao kikatiba anapaswa kuteua kwa nafasi 10, ni takwa la kikatiba kuwa lazima waapishwe kwanza kabla hawajaanza majukumu yao ya kibunge. Kwa mujibu wa Ibara ya 68 inaelezea kwa ufasaha kuwa mbunge mteule anaweza kufanya kazi moja tu kabla hajaapishwa na si vinginevyo, nayo ni kumchagua Spika. Baada ya hapo anapaswa kuapa kabla hajatekeleza wajibu wowote.

Ukiangalia Ibara ya 55 ibara ndogo ya (4) inaelekeza Mawaziri na naibu Mawaziri wanateuliwa kwa kigezo kipi kikuu. Lazima wawe miongoni mwa Wabunge na si Wateule wabunge.

Jambo kama hili liliwahi kufanyika enzi za JK ambapo alifanya uteuzi na kabla hawajaapishwa aliwaapisha kuwa mawaziri.... Inaonekana washauri wa Rais wanajitahidi kuwa inadequate ili kuharibu sifa njema ya Ikulu kulinda Katiba yetu.

Wabunge mnaosoma humu, tunaomba hili likarekebishwe Bungeni ama kwa kurekebisha Katiba isomeke mteuliwa Ubunge anaweza pia kuapishwa katika nafasi ya Waziri ama Naibu Waziri kabla hajaapishwa kuwa mbunge rasmi.

Wanazuoni wa sheria mtusaidie kudadavua hapa, nini kifanyike?
 
Kuna watu wanasema Prof. Palamagamba aliapishwa bunge lililopita, sijui kama ni kweli.
 
Kweli kunawatu wakiamuka wanazani yanayo tokea nyumbani kwao ndo yanayo tokea Tanzania nzima. Muwe munawaza na kuuliza kabla ya kupost humu kama huyu mboyoyo.
 
Mkuu Msanii na wengineo, Prof. Palamagamba J.A.M. Kabudi aliapishwa kwenye kikao cha Bunge lililopita. Alishakuwa Mbunge kamili na halali. Uteuzi wake wa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria hauna utata wowote. Tafadhali, muwe mnatafiti kabla ya kuandika humu JF kwenye watu wenye data na uelewa mpana.

Jisomee humu: https://www.jamiiforums.com/threads...alamagamba-waapa.1192504/page-3#post-20304004
Kwa jibu hili naondoa rasmi daubts zangu katika hili.

Nimeelewa
 
Back
Top Bottom