Katiba Ijayo Ipige Marufuku Ya CCM, CHADEMA, CUF Na Wengine Kuwa Na ' Wanamgambo' Wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Ijayo Ipige Marufuku Ya CCM, CHADEMA, CUF Na Wengine Kuwa Na ' Wanamgambo' Wao

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by maggid, May 6, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Kama mtego ule wa panya, tutafanya makosa makubwa kama kuna watakaodhani, kuwa haya ya watu kuchinjwa na kujeruhiwa na mapanga yatawakuta watu wa kundi fulani tu. Tukiacha yaendelee, basi, yeyote yule, bila kujali dini, rangi, itikadi au hata wadhifa wake, anaweza kuwa mhanga wa maovu haya. Kama taifa, kwa pamoja tuwalaani wauaji hawa na wanaowatuma.

  Na kwa vyama vya siasa vilivyo makini na vinavyoitakia mema nchi yetu, vianze sasa kuachana na utamaduni wa kuwa na ‘wanamgambo’ ama vikundi vya vijana vinavyopewa mafunzo ya kijeshi kwa masuala ya ulinzi.

  Historia inatufundisha,kuwa Afrika ‘ Parties militias’ ama vikundi vya wanamgambo vya vyama vya siasa huwa chanzo cha kuharakisha vurugu za kisiasa za wenyewe kwa wenyewe katika nchi na hata kupelekea mauaji. Tumeona Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kongo na kwengineko Afrika.

  Ni vikundi hivi vya wanamgambo wa vyama ambavyo hutumika na vyama, wanasiasa, au hujituma vyenyewe kufanya kazi ya kulipiza visasi vya kisiasa kwa kutumia silaha.

  Hapa kwetu tayari, vyama vikubwa vya siasa vina vikundi vya aina hiyo; CCM wana ‘ Green Guards’, Chadema wana ‘ Red Brigade’ na CUF wana ‘ Blue Guards’.

  Katika nchi ya kisasa si busara kuwa na utaratibu unaoruhusu vyama vya siasa kuwa na vikundi kama hivyo vya vijana vyenye kupata mafunzo ya kijeshi.

  Na hakika, Katiba yetu ijayo itusaidie kuondoa utaratibu kama huo wa ‘ kijima’ kwa kuweka marufuku ya vyama vya siasa kuunda vikosi vya vijana vyenye kukaa kambini na kupata mafunzo ya kijeshi, vikosi ambayo, vinaweza kuja kutumika vibaya na kutusababishia madhara makubwa kama taifa.

  Kama vyama vitahitaji ulinzi kwenye shughuli zake, basi, viombe ulinzi kwenye makampuni ya ulinzi yanayotambulika kisheria na yasiyofungamana na siasa za vyama.

  Vinginevyo, tuhakikishe jeshi letu la polisi linaimarishwa na linakuwa chombo cha usalama kinachoaminika na umma na kisichoegemea kwenye itikadi za vyama katika kufanya kazi yake. Vivyo hivyo, kwa vyombo vingine vya usalama katika nchi ikiwamo Idara ya Usalama wa Taifa. Vifanye kazi zao kwa kutanguliza maslahi ya taifa na si ya wanasiasa au vyama vyao. Inawezekana.

  ( Hii ni sehemu ya makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi leo Jumapili)

  Maggid Mjengwa
  Iringa
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kitu cha msingi TISS na polisi waache upendeleo kwa CCM. Inakera
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  CCM wana mgambo wengi, policcm, Jeshiccm, Green guard nk. CHADEMA wana Red brigade
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia mia moja. Hata katiba ya sasa inapiga marufuku lakini vinafimbiwa macho tu. Hivi vijeshi vidogodogo ni janga la taifa ambalo wakati wowote litasababisha vilio na kusaga meno.
   
 5. o

  obadiabula Member

  #5
  May 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uwe na akiri ya kuona mbali usiendeshwe na hisia, ukikosa hoja usichangie, CCM itatolewa 2015 itakusaidia nini vikiibuka vikundi kama BOKO HARAMS, JANJA WEED nk
   
 6. m

  maggid Verified User

  #6
  May 6, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hakika, na historia siku zote ni mwalimu mzuri. Tumeona ya Interahamwe juzi tu. Hatujachelewa.
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ukiona chama tawala nacho kimeanzisha "kikundi cha wana mgambo wake" hiyo ni dalili mbaya ya chama tawala kupoteza dola. Mwanzo CCM walipinga pinga, lakini baadaye serikali imekaa kimya kama haipo. Tukae mkao wa ki-Kenya Kenya, soon tutakuwa na Mungiki hapa. Maana Mungiki walialikwa mpaka Ikulu ya Mzee Mwai, japo Ikulu inakanusha.
   
 8. U

  Ukana Shilungo JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 911
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 60
  nimekusoma ndugu majggid,maoni yako nayaheshimu,ila naomba usome katiba ya nchi vizuri utagundua kuwa ushauri wako umepotoka kiasi kikubwa,kwani huko unakoshauri vyama vya siasa kuomba ulinzi kampuni binafsi,aina hiyo ya ulinzi ipo kinyume kabisa na katiba ya nchi,katiba imevunjwa.ni kama tu ingekuwa imeandikwa wazi kwamba ni marufuku vyama hivyo haviruhusiwi kuwa na askari wao kikatiba lakini ikawa nao kwa kukiuka katiba.Naam! ndivyo makapuni hayo ya ulinzi unayoyapigia upatu yanavunja katiba ya nchi na aliyeyapa vibali kavunja katiba ya nchi,kwa kukusaidia ndugu yangu soma katiba ya TZ SURA YA TISA 147 kifungu namba 1 kwenye mabano MAJESHI YA ULINZI.Na hapo utakapoona namna ulivyopotoka.MIMI NI NDUGU YAKO nasoma sana makala zako magazeti mbalimbali hasa Raia Mwema,hapa natumia jina tofauti na unalofahamu,natoka mkoa mmoja lakini kuvuka daraja la Mkapa kuja kusini.
   
 9. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Chama Tawala, pamoja na kupendelewa kote huko na vyombo vya Dola, Kama vile Polisi, TISS, TAKUKURU nk kukandamiza wapinzani iliona haitoshi na ikaunda Green Guards ambayo maovu yake yanalindwa na Dola, sasa nini kitegemewe kutoka kwa wapinzani ili kujitetea dhidi ya dhuluma hizo na usalama wake?
   
 10. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Ukianza kututia hofu kwa kuleta hoja za Interahamwe unafanya makosa makubwa...kwanza inabidi utambue utamaduni wa kisiasa wa nchi moja hadi nyingine hutofautiana.Kongo hawana amani wakati sisi tuna amani na sababu ya tofauti hizo haiko moja nazo zinatofautiana mno.
  Tambua kuwa RED brigade wanatoa ulinzi kwa viongozi wa chama na hata kwa mikutano ya chama.
  Kinyume na wazo lako ,napendekeza RED BRIGADE iimarishwe zaidi ipate mafunzo ya kiintelijensia iweze kuwalinda viongozi wetu.
  Polisi ,ambao kazi yao kuu ni kulinda mali na usalama wa raia walikuwa wapo wakati wabunge Highness Kiwia na mwenzake wanakatwa mapanga.Walikuwa wapo wakati mwenyekiti wa CDM USA RIVER anachinjwa.
  Tatizo kuu la Tanzania si RED BRIGADE wala GREEN GUARD.
  Kila mwenye akili ya kutafakari mambo anaelewa hili.
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,172
  Trophy Points: 280
  Hata katiba ya sasa hairuhusu
   
Loading...