kitalembwa
JF-Expert Member
- Jul 12, 2014
- 2,859
- 7,123
Wana bodi salaam,
Katiba yetu sio Msahafu/Biblia, nikiwa na maana muda wowote inaweza fanyiwa marekebisho pale inapohitajika kwa maslahi ya taifa yenye tija. Hili tumekuwa tukiliona likitokea kwani kufikia sasa katiba yetu imeshafanyiwa marekebisho mara kadhaa, pia nadhani hili linaweza kuendelea.
Naam, ninaona kuna haja ya kurekebisha katiba yetu, ili maraisi wastaafu waruhusiwe kugombea tena nafasi hiyo, pale watakapohisi wanaweza kufanya hivo, baada ya wao kujitosa kwenye kinyang'anyiro sisi wananchi ndio tutawapima kama tunaweza kuwaamini na kuwapa tena mamlaka ya kuliongoza taifa letu ama la.
Kwa hapa kwetu tunao maraisi wastaafu watatu ambao ni Mzee Mwinyi A.H, Mzee Mkapa B.W, na Mzee Kikwete J.K. kwa uhalisia Mzee Mwinyi amezeeka kwa umri wake (miaka 90 na kuendelea), lakini kwa hawa wawili bado nguvu zipo, zaidi kwa JK bado anaonekana anaweza kabisa kuongoza zipo.
Hakika ingependeza tena tungemuona JK kwenye harakati za kuwania tena hii nafasi, sio kwamba ni mkamilifu sana au kwenye uongozi wake hakuwa na dosari, ila dosari za awamu ya tano zimezidi kuvuka mipaka.
Enzi za JK;
-Wafanyakazi waliboreshewa maslahi, walipanda madaraja kwa wakati na kupata stahiki zao
-Demokrasia ilikuwepo ya kweli, hivi kwa ungozi huu wa JPM , kina slaa wangepata mwanya wa kuandaa mkutano wa kisiasa nchi nzima, sijui mambo ya kushukuru wanachi kwa kuwapigia kura ? mambo ya list of shame mnazi mmoja ? wangekaripiwa kwa makatazo, na wangeishia kuswekwa jela kwa kesi za uchochezi, lakini JK hakuwa anahaingaika nao, anawaacha wanatoa ya moyoni maisha yanaendelea.
-Mishahara ilikuwa inatoka kwa wakati, longolongo hazikuwepo
-Ajira zilikuwepo, japo hapa naomba nikiri kwamba aliweza kuajiri kwa kiasi chache kulingana na uhitaji na bajeti. Nikiri tatizo la ajira limekuwa sugu hata huko nchi za watu japo tatizo sio kubwa kama nchi za ulimwengu wa tatu mfano Tanzania. Hata USA, England, Germany na kwingineko hili tatizo lipo lakini huwezi kulinganisha na bongo.
-Uhuru wa habari ulikuwepo.
-Alijitahidi kujenga mahusiano mazuri na wapinzani, kuwaita kukaa nao pamoja na kujadili baadhi ya mambo yenye maslahi kwa nchi. Mara ngapi kina ZZK, Mbowe, Slaa, Lipumba wameenda ikulu na kunywa chai na mheshimiwa JK huku wakijadili mambo ya taifa letu ? vipi kwa huyu wa sasa ?
-Walau uchumi ulikuwa wastani, mambo yalikuwa yanaenda sio kama sasa, pesa ilikuwepo kwenye mzunguko. kwa kipindi hiki mambo yamebadilika sana.
-Miradi ya maendeleo ilikuwepo na ilifanyika vizuri kabisa, mifano mnayo.
Kwa kifupi hayo niliyoorodhesha hapo na mengine mengi ni baadhi ya mazuri ya JK, nchi ilikuwa na usawa, kila mtu alikula kwa namna yake, haki za binadamu zilizingatiwa n.k
Kwa nini katiba isirekebishwe hiki kipengele cha wastaafu waruhusiwe kugombea tena kikawekwa? hakika JK akijitosa tena atashinda kwa kishindo kikubwa sana.
Huyu mzee wetu ni mwanasiasa haswa, master mind, anajua afanye nini kwa wakati gani, hakurupuki na anapokea ushauri, kwa kifupi yupo smart sana na maamuzi anayoyafanya.