tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,864
- 3,851
Tufikirie kwamba Baraka za Escrow na makinikia zilitokana na ushauri wa Baraza la Mawaziri kwa Rais na Rais alikubali. Basi Ibara ya 54 (5) ya Katiba ya Tanzania, inawakinga wote waliohusika. Soma mwenyewe mpaka mwisho
Baraza la Mawaziri na Serikali
Baraza la
Mawaziri
Sheria ya
1984 Na.15
ibara 9
Sheria Na.4
ya 1992 ib…
Sheria Na.34
ya 1994 ibara
12
54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe
wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa
Zanzibar na Mawaziri wote.
(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye
atkayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi
mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili
Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza
Mikutano hiyo.
(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya
Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha
kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji
wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na
litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote
litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo
maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.
(4) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria mikutano yote
ya Baraza la Mawaziri na atakuwa na haki zote za mjumbe wa
mikutano hiyo isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura katika
mikutano hiyo.
(5) Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa
na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika
mahakama yoyote.
Tanzania tuna safari ndefu sanaaa