Katiba ibadilishwe, rasmi Tanzania iwe na chama kimoja tu

Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
921
1,658
Kwa hizi drama zinazoendelea hapa nchini ni vema kwa serikali yetu huru na yenye kujiamulia mambo yake yenyewe pasipo kuingiliwa na mtu wala nchi yoyote kufanya mabadiliko ya katiba na kupitisha rasmi mfumo wa chama kimoja~monopartism

Kwa sasa inaonekana tunapoteza muda tu wakujihisisha na shughuli zingine za kimaendeleo kwa kufocus zaidi kwenye chaguzi zisokuwa hata na chembe ya upinzani kwa kutawaliwa na mabavu ya chama kimoja cha kijani

Pia ni upotevu wa pesa za wananchi ambazo zingetumika kufanya maendeleo katika nyanja mbalimbali hapa nchini, pia pesa za wagombea hasa wa upinzani nawasikitia zinaenda bure kugharamia uchaguzi na kampeni huku wakijua kabisa hawawezi kutangazwa mbele ya chama dola

Ewe mkuu wa serikali ni wakati wako sasa kuondoa huu usumbufu na malalamiko na vitisho toka upinzani kama vile kuandamana na kwenda mahakamani ni vema ukabadili katiba ijulikane wazi tuko chini ya chama kimoja



Chifyono
 
Nakumbuka kipindi kile Wananchi wengi wakipiga kura hawakutaka vyama vingi, walisema vitaleta vurugu
 
Kubadilisha katiba na kuipeleka katika mfumo wa chama kimoja eti kwa kuwa CCM wanaminya haki ya vyama vya upinzani ni kuunga mkono maovu yanayofanywa na ccm, katiba iendelee kuwa ileile inayoruhusu mfumo wa vyama vingi ili maovu ya CCM yaendelee kuonekana peupe.

Kinachohitajika ni kudai katiba mpya yenye uwezo wa kumdhibiti shetani hata kama atakuja malaika naye awezekudhibitiwa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom