Katiba hii safi kwa marais Magufuli na Nyerere

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,291
12,584
Katiba hii ya sasa ni nzuri sana kwa kiongozi muadilifu na anayekusudia kufanya mambo mema kwa haraka. Rais Nyerere aliweza kuitumia kwa kujenga ummoja miongoni mwa watazania, kukuza kiswahili, kujenga vijiji vya ujamaa, kuunganisha na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kusaidiana na nchi nyingine kuikomboa Africa.

Rais Magufuli anaitumia sasa hivi kukomesha vichuguu vyote vya ubabaishaji kazini, wizi, na rushwa kwa urahisi kabisa. Hata wazungu waliendelea haraka enzi zile kwakuwa katiba zao hazikuruhusu demokrasia na ziliruhusu mtumwa, viboko, kufanyakazi kwa masaa mengi kwa siku kwa ujira kidogo bila kuhoji, kutawala na kupora mali za nchi nyingine, n.k.

Hata China inaendelea kutokana na kuruhusu demokrasia kidogo sana na kuwanyonga wezi na wababaishaji wengine. Katiba hii ni bora kwa Rais safi mwenye dhamira safi kwa taifa, lakini ni mbaya kwa Rais mwizi wa makinikia yetu na twiga wetu kwakuwa katiba hii inauwezo wa kusababisha vyombo vyooote vya ulinzi na usalama visione twiga hai akipakiwa kwenye ndege mchana na kuondoka zake na madawa ya kulevya yapite airport salama usalimini.

Sasa kwakuwa hatujui ni Rais gani anayefuta 2020 ni Bora kabisa tujilinde kwa kutunga katiba itakayokidhi rais yeyote wa aina yoyote
 
tatizo ni moja kuhusu Magu
Anadhani suala (sio swala) la katiba mpya inayoombwa na watanzani basi ni agenda ya akina Tundu Lissu na upinzani
hapa ndo kipimo chake cha busara kinapokoseka kupenda kuweka ushindani usio na maana yoyote kwa watu ambao hawana madhara na serikali yake
ubishi unamshushia hadhi
 
Hatuwezi kuipata katiba mpya ya wananchi kwa sababu sisi (WaTz) hatuna pressure ya kudai, tunadhani ni kazi ya vyama vya upinzani !!!
 
2020 unataka kumtoa huyu uliyemsifia kwa kuwanyoosha wazungu ili ukamweke nani tena? Ama ndo unaota kuwaleta hao wa kupakia twiga wakiwa hai? Kwasababu naamini bado tunaye huyu uliyemsifia hatuna haja ya uharaka wa hivyo. Mda uongea na wakati uja pale hatma ikiwadi.. Vuta pumzi.
 
Ukitizama nchi nyingi ( isipokuwa chache tu)zimeendelea kiuchumi baada ya kubadilisha utawala wa vyama vya kisiasa.Hivyo sahau maendeleo chini ya fikra zilezile.
 
2020 unataka kumtoa huyu uliyemsifia kwa kuwanyoosha wazungu ili ukamweke nani tena? Ama ndo unaota kuwaleta hao wa kupakia twiga wakiwa hai? Kwasababu naamini bado tunaye huyu uliyemsifia hatuna haja ya uharaka wa hivyo. Mda uongea na wakati uja pale hatma ikiwadi.. Vuta pumzi.

Kwa Mungu hakuna dogo wala kubwa, yeye ndiye Muweza, sisi wanadamu tunapanga lakini yeye anapanga zaidi yetu na alitakalo ndilo huwa. Niheri tukeshe tukipanga kama nchi maana hatuijui siku wala saa Mungu atatujalilia kitu gani kesho.
Tusiache kupanga maana Rais ajae ni Mungu pekee anamjua. Amen
 
Kwa Mungu hakuna dogo wala kubwa, yeye ndiye Muweza, sisi wanadamu tunapanga lakini yeye anapanga zaidi yetu na alitakalo ndilo huwa. Niheri tukeshe tukipanga kama nchi maana hatuijui siku wala saa Mungu atatujalilia kitu gani kesho.
Tusiache kupanga maana Rais ajae ni Mungu pekee anamjua. Amen
Hitimisho lako kama liko hivi basi meseji yako haina muunganiko mzuri wa kimantiki. Kaifanyie review ili tukuelewe unavyotaka kueleweka
 
Hitimisho lako kama liko hivi basi meseji yako haina muunganiko mzuri wa kimantiki. Kaifanyie review ili tukuelewe unavyotaka kueleweka
Inaeleweka tu mkuu, Rais Nyerere alidhani kuwa marais wote wajao wangekuwa kama yeye lakini haikuwa vile hata chembe, alishuhudia kwa macho yake kuundwa Azimio la Zanzibar na kuzikwa kwa Azimio la Arusha. Aliona kwa kwa macho yake mashirika yake akiuzwa kama pipi, alitamani kulia lakini ilishindikana. Ingawa Rais Magufuli ni mwadilifu lakini faida za kuwa na katiba mpya ni nyingi kuliko hasara, maana hata yeye alisema sio Rais wa kudumu pale. Tunaweza kumpata Rais kama Trump ambae anafuta kila kitu alichosema na kufanya Obama. Tunaweza kumpata Rais ambaye atarudisha makinikia yote kwa Acacia na kumlaani Rais aliyeyazuia siku ya kwanza tu baada ya kuingia Ikulu.
 
Inaeleweka tu mkuu, Rais Nyerere alidhani Rais marais wote wajao wangekuwa kama yeye lakini haikuwa vile hata chembe, alishuhudia kwa macho yake kuundwa Azimio la Zanzibar na kuzikwa kwa Azimio la Arusha. Aliona kwa kwa macho yake mashirika yake akiuzwa kama pipi, alitamani kulia lakini ilishindikana. Ingawa Rais Magufuli ni mwadilifu lakini faida za kuwa na katiba mpya ni nyingi kuliko hasara, maana hata yeye alisema sio Rais wa kudumu pale. Tunaweza kumpata Rais kama Trump ambae anafuta kila kitu alichosema na kufanya Obama. Tunaweza Rais ambaye atarudisha makinikia yote kwa Acacia na kumlaani Rais aliyeyazuia.
Tunafikiria tubadilishe katiba ili JPM aendelee kuwepo na aitumie hii hii iliyopo ila ikifika mda anaondoka basi ndo atusaidie kutupatia mpya
 
Back
Top Bottom