kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,293
- 12,593
Katiba hii ya sasa ni nzuri sana kwa kiongozi muadilifu na anayekusudia kufanya mambo mema kwa haraka. Rais Nyerere aliweza kuitumia kwa kujenga ummoja miongoni mwa watazania, kukuza kiswahili, kujenga vijiji vya ujamaa, kuunganisha na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kusaidiana na nchi nyingine kuikomboa Africa.
Rais Magufuli anaitumia sasa hivi kukomesha vichuguu vyote vya ubabaishaji kazini, wizi, na rushwa kwa urahisi kabisa. Hata wazungu waliendelea haraka enzi zile kwakuwa katiba zao hazikuruhusu demokrasia na ziliruhusu mtumwa, viboko, kufanyakazi kwa masaa mengi kwa siku kwa ujira kidogo bila kuhoji, kutawala na kupora mali za nchi nyingine, n.k.
Hata China inaendelea kutokana na kuruhusu demokrasia kidogo sana na kuwanyonga wezi na wababaishaji wengine. Katiba hii ni bora kwa Rais safi mwenye dhamira safi kwa taifa, lakini ni mbaya kwa Rais mwizi wa makinikia yetu na twiga wetu kwakuwa katiba hii inauwezo wa kusababisha vyombo vyooote vya ulinzi na usalama visione twiga hai akipakiwa kwenye ndege mchana na kuondoka zake na madawa ya kulevya yapite airport salama usalimini.
Sasa kwakuwa hatujui ni Rais gani anayefuta 2020 ni Bora kabisa tujilinde kwa kutunga katiba itakayokidhi rais yeyote wa aina yoyote