eliesikia
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 787
- 755
Hebu angalieni ibara ya 41 katika katiba ya nchi kipengele cha 6 na 7 vinakinzana mwaka huu
41. (6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote.:sad:
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake.
Katiba imelazimishwa kumtambua Jk.. Maana hata na yenyewe inamtambua raisi aliyetokana na wananchi na si vinginevyo... JK hayuko pale kwa mujibu wa sheria bali de facto(kwa kutumia nguvu na kubaka demokrasia)...
CHADEMA wana haki ya kutambua baadhi ya matokeo ya ubunge ndio maana mengine yako mahakamani tayari... Mimi nadhani kipengele cha kutotambua matokeo ya uraisi ndio kero hapa kifutwe halafu mengine tutaongea baadae...
Kule jamaa wanachakachua lakini muhimili mmoja yaani serikali wamebaka mamlaka ya mahakama kwa kusema matokeo ya uraisi hayawezi kupelekwa mahakamani<ibara ya 41(7)>...
Mimi nashauri siku raisi anasoma hotuba pale bungeni ni lazma CHADEMA watoke kuonyesha nia yao ya dhati... Lakini kama watakuwepo basi lazma watakuwa na njia yao mbadala ya kukataa haya matokeo kama walivyodai watatupa msimamo mzima wa ligi ulivyokuwa na kilichotokea...
Watu wengi hawaelewi maana ya mtu anaposema hamtambui raisi maana wengine wanafikiri anakiuka sheria ya treason... Lakini La hasha CHADEMA wamekuwa wastaarabu saana maana maeneo mengine watu walishaanza kutembea barabarani kudai haki tumeona Shinyanga, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma ujiji kusema kwelli CHADEMA wametumia utaratib mzuri sana na kufuta ile dhana ya kuwa wanapenda fujo... Huu ni ustaarabu mwenye akili atafikiri ila aliyenyimwa akaombewe tuu!!!
Nawasilisha hoja