Broadfuture

New Member
Mar 28, 2022
4
3
UTANGULIZI

Maisha ya mwanadamu yamejikita katika ngazi mbalimbali za kijamii kulingana na muundo au mfumo ambao jamii husika hujiwekea. Ukubwa wa jamii zetu huanzia chini kabisa na hatimae kupanda juu kutoka ngazi moja had Ngazi nyingine. Ngazi hizi ni kama vile, familia, ukoo, kabila, taifa Fulani, bara moja na jingine na hatimae umoja wa mataifa Kwa maana ya mkusanyiko wa nchi zote wanachama duniani.

Katika ngazi hizo zote, jamii husika hujiwekea utaratibu wa kimakubaliano kuhusu namna jamii Yao itajiendesha na namna ambavyo kila mwanajamii atajua haki na wajibu wake katika jamii husika, hivyo makubaliano haya husaidia utawala wa jamii husika kutekeleza majukumu Yao Kwa ufanisi mkubwa.

Katiba ni sauti au makubaliano ya wanajamii kuhusu malengo Yao na mategemeo walionayo Kwa viongozi ambao wanachaguliwa kutokana na katiba ambayo jamii husika hujiwekea. Ni wazi kwamba mabadiliko chanya ya kiuchumi siasa na kijamii yanategemea sana ubora wa katiba husika katika kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa.

Nchi yetu nzuri ya Tanzania inatumia katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo, Kwa muda wote kutoka kuandikwa kwake imetumika kusimamia na kutekeleza matarajio ya watanzania.

Kama ilivyo katika ibara ya 18(1) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inatupa wananchi wa Tanzania haki ya kutoa maoni, ninaomba nijikite katika kutumia haki yangu hiyo kushauri kuhusu mambo muhimu ambayo katiba kama dira na muongozo mkuu wa nchi inayakosa na hivyo kufanya jamii yetu isiweze kufikia katika hatua nzuri ya ustawi wa uwazi, uwajibikaji, haki za binadamu , demokrasia pamoja na utawala Bora.

UHURU WA MIHIMILI
images (14).jpeg

Picha na jamii forums tanzania

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kikatiba inaundwa na mihimili mitatu ambayo Kwa mujibu wa ibara ya 4(1) na 4(2) vyombo hivyo vimefafanuliwa kuwa ni mahakama, Bunge na Serikali na hapo vyombo hivyo vimehusisha vyombo vya pande zote mbili za Muungano.

Udhaifu ambao upo katika eneo hili ni kwamba, uhuru wa vyombo hivi sio halisi kama ambavyo katiba hii inajaribu kutuaminisha na hivyo kuathiri upatikanaji wa haki miongoni mwa wanajami. Tuzingatie mifano ifuatayo.

(1) ikiwa Raisi wa Tanzania ndiye ambae anateua Jaji mkuu pamoja na majaji wote wa mahakama kuu kama ilivyo katika ibara ya 109(2) na ikiwa pia shuguli zote za kimahakama zinategemea kuletewa Fungu kutoka Kwa serikali Ili shughuli zake ziende unadhani ni Kwa kiasi gani watendaji Hawa watakuwa na uhuru katika majukumu Yao ya kutafsiri sheria hasa kwenye kesi ambazo serikali Ina maslahi nazo ?? ni wazi kwamba katiba inapaswa kutoa misingi imara ambayo itawezesha mihimili hii kuwa huru.

(2) Muhimili wa serikali huunda baraza lake la mawaziri ambalo husimamia wizara mbalimbali Kwa niaba ya serikali. Baraza Hilo Hilo pia, Kwa maana ya mawaziri ni sehemu ya Bunge la Jamuhuri la Muungano Kwa kuwa wao huteuliwa miongoni mwa wabunge kama masharti ya ibara 55(4) ya katiba ya Tanzania. Uwepo wa mawaziri bungeni kunawapa nafasi ya kuwa katika ngazi za maamuzi katika mihimili miwili Kwa wakati mmoja. yaani wanazitunga sheria na hao hao ndio wanaokwenda kuzisimamia jambo ambalo linaleta mgongano wa kimaslahi.

(3) Katiba inapompa Rais nafasi kumi za wabunge wa kuteuliwa ndani ya Bunge la Jamuhuri ya muungano Kwa akili ya kawaida kabisa ni kwamba Raisi anapewa nguvu ndani ya Muhimili mwingine na hivyo Kwa namna tofauti tofauti anaweza kuathiri utendaji kazi huru wa Muhimili wa bunge

(4)Kwa mujibu wa ibara ya 90(2)(b) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Rais wa tanzania anaweza kulivunja Bunge endapo limekataa kupitisha mswada wa serikali. wasiwasi wangu ni kwamba kipengele hiki huenda kikawalazimisha wabunge kupitisha muswada hata kama hauna maslahi ya wananchi wengi Kwa sababu tu wanaogopa ajira zao kuvunjwa kikatiba.

(5) ibara ya 66(1)(d) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inamtambua mwanasheria mkuu wa serikali kama sehemu ya Bunge la taifa. Mwanasheria mkuu wa serikali pia ni kiongozi mwandamizi wa serikali na hivyo uwepo wake ndani ya Bunge unaweza kudhoofisha uhuru wa Muhimili huo kufanya majukumu yake

UTAWALA BORA
images (10).jpeg

Picha na Nigerian image

Utawala Bora ni mchakato ambao unahusisha utawala wa sheria, uwazi na uwajibikaji, namna ambavyo viongozi husikiliza na kurudisha mrejesho Kwa wananchi, usawa mbele ya sheria pamoja na maridhiano. Hizi ni nyenzo muhimu sana katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Pamoja na kazi nzuri na jitihada za kuboresha utawala Bora nchini bado yapo mambo mengi na makubwa yanayotakiwa kufanyika Ili kuleta mabadiliko ya kiutawala katika jamii yetu kama ifuatavyo;

RUSHWA
images (13).jpeg

Picha kutoka CSAAE

Rushwa ni adui mkubwa sana wa haki na maendeleo ya jamii yetu. katika nchi ya Tanzania ripoti za taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na utafiti ikiwemo pia taasisi ya serikali TAKUKURU zimeelezea rushwa kujitokeza katika sekta mbalimbali kama afya, elimu, mahakama, polisi na maeneo mengine mengi yanayohusika na utoaji wa huduma za kijamii. Hivi sasa hata baadhi ya watu wamekuwa wakipambania nafasi mbalimbali za uongozi si Kwa lengo la kutumikia wananchi bali tayari Kuna Imani iliyojengeka kuwa unapopata nafasi katika maeneo ya maamuzi Kuna "ulaji" ambao utafanya maisha yako yabadilike haraka.

USAWA MBELE YA SHERIA
images (12).jpeg

Picha na dreamstime.com

Kuna mazingira mengi sana hapa nchini ambayo yanafanya jamii yetu isijione kuwa na haki sawa mbele ya uso wa sheria. Kwa mfano asilimia kubwa ya kesi ambazo zinaendeshwa katika mahakama za wilaya na hasa zile ambazo zinahusisha adhabu kubwa kama kifungo Cha miaka thelathini na kifungo Cha maisha, watuhumiwa wengi ambao ni masikini na sio wajuzi wa sheria wamekuwa hawapati uwakilishi wa wataalamu wa sheria Ili kuhakikisha haki zao katika mashauri hayo zinasimamiwa ipasavyo. Kama tunakubaliana kwamba zipo kesi za kweli ni vyema pia tukubaliane kwamba zipo kesi za uongo ambazo wananchi wanabambikwa na kwamba ikiwa aliyebambikwa kesi akakosa uwakilishi au ufahamu mzuri wa kisheria anaweza kufungwa hata kama kosa husika si la kweli.

UWAZI NA UWAJIBIKAJI
images (15).jpeg

Picha na NTV kenya

Si vibaya tukitolea mfano taifa la jirani la Kenya na hata lile la Afrika ya kusini ambapo wamefanikiwa Kwa kiwango Cha kuridhisha kuhakikisha uwazi unakuwepo hasa kwenye jambo lenye maslahi Kwa nchi. Mfano, kunapokuwepo na kesi zenye maslahi Kwa umma kesi hizo huendeshwa Kwa uwazi na wananchi wote kutoka pande zote za nchi hizo wanaweza kujionea na kufatilia mwenendo mzima wa kesi hizo kupitia Runinga. Hii inasaidia kuwafanya wahusika wawajibike Kwa viwango vinavyotarajiwa. Mfano ni kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais Kenya. Nchi yetu ya Tanzania hairuhusu hata kupeleka mahakamani shauri la kupinga matokeo ya Urais kama ilivyo katika ibara ya 41(7) jambo ambalo ni hatari katika uwazi wa maamuzi ya wananchi. Pamoja na mambo mengine mengi yanavyohitaji uwazi kama vile mikataba muhimu ya nchi, uendeshaji na usimamiaji wa miradi, ni lazima viongozi wahakikishe mambo hayo muhimu yanafanywa Kwa uwazi Ili wananchi wajue muelekeo halisi wa nchi Yao.

HAKI ZA BINADAMU

images (7).jpeg
picha kutoka mtandaoni

Binadamu ana haki nyingi sana ambazo zinatajwa katika katiba yetu, Lakini kuitaja haki ya mtanzania katika katiba ni jambo moja na kuhakikisha haki hiyo inatekelezwa ipasavyo ni jambo jingine kabisa. miongoni mwa haki zinazokiukwa na kufanya jamii yetu ibaki nyuma katika eneo hili ni pamoja na haki ya kupata taarifa na uhuru wa kutoa maoni pamoja na haki ya faragha. Katika usimamizi wa sheria chini ya jeshi la polisi kumekuwepo na malalamiko mengi kuhusu ukiukwaji wa haki za watuhumiwa hasa ikishusisha watuhumiwa kupigwa Ili kukubali mashtaka ambayo wanashitakiwa nayo. Jambo hili linazorotesha sana upatikanaji wa haki za wananchi kwani watuhumiwa hupelekwa mahakamani na kielelezo Cha maelezo ya onyo ambayo yanatokana na kupigwa au kutishiwa.

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
images (16).jpeg

Picha NTV kenya

Uhuru wa vyombo vya habari bado ni tatizo kubwa kutokana na sheria mbalimbali kandamizi katika tasnia hiyo. mfano sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015 na sheria ya upatikanaji wa habari ya mwaka 2016. Hali hii inafanya haki ya msingi ya mtu kupata taarifa sahihi kukiukwa Kwa kiwango kikubwa sana na ni vyema mamlaka kuhakikisha upatikanaji Bora wa habari Ili kuijenga jamii mpya inayofurahia upashanaji habari.

DEMOKRASIA NA UZALENDO
images (8).jpeg

Nchi ya Tanzania inafanya siasa za vyama vingi tangu ilipoanzishwa mwaka 1992 na kutekelezwa Kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1995. Mfumo huu kama ulivyodadavuliwa na wataalamu wengi kwamba unaongeza uwazi na uwajibikaji na kuruhusu serikali kusimamiwa ipasavyo na vyama vya upinzani. Pamoja na faida hii kubwa sana katika maendeleo ya kiuchumi, Andiko langu linapenda kuwakumbusha watanzania kuwa utekelezwaji wa democrasia ni lazima uende sambamba na uzalendo wa wananchi wote.

Imekuwa desturi ya vyama tawala na vyama vya upinzani kuonesha kwamba hakuna jambo ambalo upande mmoja litafanya likasifiwa hata kama jambo Hilo ni zuri na Lina tija Kwa taifa. Hali kadhalika si jambo la ustawi pale ambapo chama chenye nguvu kinapojaribu kukwamisha haki za kisheria za chama kingine Ili kisiweze kutekeleza majukumu yake Kwa mujibu wa sheria. Ndio maana nimeandika demokrasia na uzalendo kwani kila mmoja katika makundi haya akijua kuwa lengo kubwa ni kunyanyua maendeleo ya Tanzania na sio tumbo lake, basi atakuwa na uwezo wa kukosoa kile kinachopaswa kukosolewa Ili kilete tija Kwa taifa na pia hatasita kupongeza na kuboresha kile ambacho kimefanywa na upande wa pili kwakuwa lengo kubwa ni kuifanya nchi kipaumbele Cha kwanza.

UKOLONI MAMBO LEO
images (9).jpeg

Picha kutoka Kwa elenga mbuyinga. (Mwandishi)

Watawala wetu ni lazima wawe makini na zimwi hili lenye malengo maovu kabisa na ustawi wa jamii yetu. suluhisho kubwa la kuondoa janga hili ni kutengeneza sera Bora za kujitegemea na kuwekeza katika sekta zitakazowezesha kundi kubwa la wananchi kujiajiri Ili kukuza Pato la nchi yetu. Mikataba ya mataifa makubwa imekuwa sio salama kabisa katika nchi nyingi za kiafrika na hivyo kutokuwa makini Kwa viongozi na kukosa fikra za kizalendo kunaweza kufanya nchi yetu kutonufaika na rasilimali yake

Kwa kuhitimisha, ningeomba kila mwana jamii wa Tanzania atambue kuwa ana jukumu kubwa la kuleta mabadiliko katika jamii yetu bila kujali yeye ni kiongozi au ni mwananchi wa kawaida. Na kwakuwa sote tunaamini uwepo wetu Duniani ni matakwa ya MUNGU hivyo tukifanya Yale yanayompendeza tutaibadilisha sana nchi yetu na kuwa sehemu ya baraka kubwa.

Chanzo cha marejeo

- Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

-mtandao.

0682011337
 
Attachments

  • images (7).jpeg
    images (7).jpeg
    24.6 KB · Views: 9
  • images (8).jpeg
    images (8).jpeg
    30.9 KB · Views: 9
UTANGULIZI

Maisha ya mwanadamu yamejikita katika ngazi mbalimbali za kijamii kulingana na muundo au mfumo ambao jamii husika hujiwekea. Ukubwa wa jamii zetu huanzia chini kabisa na hatimae kupanda juu kutoka ngazi moja had Ngazi nyingine. Ngazi hizi ni kama vile, familia, ukoo, kabila, taifa Fulani, bara moja na jingine na hatimae umoja wa mataifa Kwa maana ya mkusanyiko wa nchi zote wanachama duniani.

Katika ngazi hizo zote, jamii husika hujiwekea utaratibu wa kimakubaliano kuhusu namna jamii Yao itajiendesha na namna ambavyo kila mwanajamii atajua haki na wajibu wake katika jamii husika, hivyo makubaliano haya husaidia utawala wa jamii husika kutekeleza majukumu Yao Kwa ufanisi mkubwa.

Katiba ni sauti au makubaliano ya wanajamii kuhusu malengo Yao na mategemeo walionayo Kwa viongozi ambao wanachaguliwa kutokana na katiba ambayo jamii husika hujiwekea. Ni wazi kwamba mabadiliko chanya ya kiuchumi yanategemea sana ubora wa katiba husika katika kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa.

Nchi yetu nzuri ya Tanzania inatumia katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo, Kwa muda wote kutoka kuandikwa kwake imetumika kusimamia na kutekeleza matarajio ya watanzania.

Kama ilivyo katika ibara ya 18(1) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inatupa wananchi wa Tanzania haki ya kutoa maoni, ninaomba nijikite katika kutumia haki yangu hiyo kushauri kuhusu mambo muhimu ambayo katiba kama dira na muongozo mkuu wa nchi inayakosa na hivyo kufanya jamii yetu isiweze kufikia katika hatua nzuri ya ustawi wa uwazi, uwajibikaji, haki za binadamu , demokrasia pamoja na utawala Bora.

UHURU WA MIHIMILIView attachment 2378221
Picha na jamii forums tanzania

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kikatiba inaundwa na mihimili mitatu ambayo Kwa mujibu wa ibara ya 4(1) na 4(2) vyombo hivyo vimefafanuliwa kuwa ni mahakama, Bunge na Serikali na hapo vyombo hivyo vimehusisha vyombo vya pande zote mbili za Muungano.

Udhaifu ambao upo katika eneo hili ni kwamba, uhuru wa vyombo hivi sio halisi kama ambavyo katiba hii inajaribu kutuaminisha na hivyo kuathiri upatikanaji wa haki miongoni mwa wanajami. Tuzingatie mifano ifuatayo.

(1) ikiwa Raisi wa Tanzania ndiye ambae anateua Jaji mkuu pamoja na majaji wote wa mahakama kuu kama ilivyo katika ibara ya 109(2) na ikiwa pia shuguli zote za kimahakama zinategemea kuletewa Fungu kutoka Kwa serikali Ili shughuli zake ziende unadhani ni Kwa kiasi gani watendaji Hawa watakuwa na uhuru katika majukumu Yao ya kutafsiri sheria hasa kwenye kesi ambazo serikali Ina maslahi nazo ?? ni wazi kwamba katiba inapaswa kutoa misingi imara ambayo itawezesha mihimili hii kuwa huru.

(2) Muhimili wa serikali huunda baraza lake la mawaziri ambalo husimamia wizara mbalimbali Kwa niaba ya serikali. Baraza Hilo Hilo pia, Kwa maana ya mawaziri ni sehemu ya Bunge la Jamuhuri la Muungano Kwa kuwa wao huteuliwa miongoni mwa wabunge kama masharti ya ibara 55(4) ya katiba ya Tanzania. Uwepo wa mawaziri bungeni kunawapa nafasi ya kuwa katika ngazi za maamuzi katika mihimili miwili Kwa wakati mmoja. yaani wanazitunga sheria na hao hao ndio wanaokwenda kuzisimamia jambo ambalo linaleta mgongano wa kimaslahi.

(3) Katiba inapompa Rais nafasi kumi za wabunge wa kuteuliwa ndani ya Bunge la Jamuhuri ya muungano Kwa akili ya kawaida kabisa ni kwamba Raisi anapewa nguvu ndani ya Muhimili mwingine na hivyo Kwa namna tofauti tofauti anaweza kuathiri utendaji kazi huru wa Muhimili wa bunge

(4)Kwa mujibu wa ibara ya 90(2)(b) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Rais wa tanzania anaweza kulivunja Bunge endapo limekataa kupitisha mswada wa serikali. wasiwasi wangu ni kwamba kipengele hiki huenda kikawalazimisha wabunge kupitisha muswada hata kama hauna maslahi ya wananchi wengi Kwa sababu tu wanaogopa ajira zao kuvunjwa kikatiba.

(5) ibara ya 66(1)(d) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inamtambua mwanasheria mkuu wa serikali kama sehemu ya Bunge la taifa. Mwanasheria mkuu wa serikali pia ni kiongozi mwandamizi wa serikali na hivyo uwepo wake ndani ya Bunge unaweza kudhoofisha uhuru wa Muhimili huo kufanya majukumu yake

UTAWALA BORAView attachment 2378198
Picha na Nigerian image

Utawala Bora ni mchakato ambao unahusisha utawala wa sheria, uwazi na uwajibikaji, namna ambavyo viongozi husikiliza na kurudisha mrejesho Kwa wananchi, usawa mbele ya sheria pamoja na maridhiano. Hizi ni nyenzo muhimu sana katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Pamoja na kazi nzuri na jitihada za kuboresha utawala Bora nchini bado yapo mambo mengi na makubwa yanayotakiwa kufanyika Ili kuleta mabadiliko ya kiutawala katika jamii yetu kama ifuatavyo;

RUSHWAView attachment 2378205

Picha kutoka CSAAE

Rushwa ni adui mkubwa sana wa haki na maendeleo ya jamii yetu. katika nchi ya Tanzania ripoti za taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na utafiti ikiwemo pia taasisi ya serikali TAKUKURU zimeelezea rushwa kujitokeza katika sekta mbalimbali kama afya, elimu, mahakama, polisi na maeneo mengine mengi yanayohusika na utoaji wa huduma za kijamii. Hivi sasa hata baadhi ya watu wamekuwa wakipambania nafasi mbalimbali za uongozi si Kwa lengo la kutumikia wananchi bali tayari Kuna Imani iliyojengeka kuwa unapopata nafasi katika maeneo ya maamuzi Kuna "ulaji" ambao utafanya maisha yako yabadilike haraka.

USAWA MBELE YA SHERIAView attachment 2378196
Picha na dreamstime.com

Kuna mazingira mengi sana hapa nchini ambayo yanafanya jamii yetu isijione kuwa na haki sawa mbele ya uso wa sheria. Kwa mfano asilimia kubwa ya kesi ambazo zinaendeshwa katika mahakama za wilaya na hasa zile ambazo zinahusisha adhabu kubwa kama kifungo Cha miaka thelathini na kifungo Cha maisha, watuhumiwa wengi ambao ni masikini na sio wajuzi wa sheria wamekuwa hawapati uwakilishi wa wataalamu wa sheria Ili kuhakikisha haki zao katika mashauri hayo zinasimamiwa ipasavyo. Kama tunakubaliana kwamba zipo kesi za kweli ni vyema pia tukubaliane kwamba zipo kesi za uongo ambazo wananchi wanabambikwa na kwamba ikiwa aliyebambikwa kesi akakosa uwakilishi au ufahamu mzuri wa kisheria anaweza kufungwa hata kama kosa husika si la kweli.

UWAZI NA UWAJIBIKAJI
View attachment 2387889
Picha na NTV kenya

Si vibaya tukitolea mfano taifa la jirani la Kenya na hata lile la Afrika ya kusini ambapo wamefanikiwa Kwa kiwango Cha kuridhisha kuhakikisha uwazi unakuwepo hasa kwenye jambo lenye maslahi Kwa nchi. Mfano, kunapokuwepo na kesi zenye maslahi Kwa umma kesi hizo huendeshwa Kwa uwazi na wananchi wote kutoka pande zote za nchi hizo wanaweza kujionea na kufatilia mwenendo mzima wa kesi hizo kupitia Runinga. Hii inasaidia kuwafanya wahusika wawajibike Kwa viwango vinavyotarajiwa. Mfano ni kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais Kenya. Nchi yetu ya Tanzania hairuhusu hata kupeleka mahakamani shauri la kupinga matokeo ya Urais kama ilivyo katika ibara ya 41(7) jambo ambalo ni hatari katika uwazi wa maamuzi ya wananchi. Pamoja na mambo mengine mengi yanavyohitaji uwazi kama vile mikataba muhimu ya nchi, uendeshaji na usimamiaji wa miradi, ni lazima viongozi wahakikishe mambo hayo muhimu yanafanywa Kwa uwazi Ili wananchi wajue muelekeo halisi wa nchi Yao.

HAKI ZA BINADAMU

View attachment 2378187 picha kutoka mtandaoni

Binadamu ana haki nyingi sana ambazo zinatajwa katika katiba yetu, Lakini kuitaja haki ya mtanzania katika katiba ni jambo moja na kuhakikisha haki hiyo inatekelezwa ipasavyo ni jambo jingine kabisa. miongoni mwa haki zinazokiukwa na kufanya jamii yetu ibaki nyuma katika eneo hili ni pamoja na haki ya kupata taarifa na uhuru wa kutoa maoni pamoja na haki ya faragha. Katika usimamizi wa sheria chini ya jeshi la polisi kumekuwepo na malalamiko mengi kuhusu ukiukwaji wa haki za watuhumiwa hasa ikishusisha watuhumiwa kupigwa Ili kukubali mashtaka ambayo wanashitakiwa nayo. Jambo hili linazorotesha sana upatikanaji wa haki za wananchi kwani watuhumiwa hupelekwa mahakamani na kielelezo Cha maelezo ya onyo ambayo yanatokana na kupigwa au kutishiwa.

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
View attachment 2387905
Picha NTV kenya

Uhuru wa vyombo vya habari bado ni tatizo kubwa kutokana na sheria mbalimbali kandamizi katika tasnia hiyo. mfano sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015 na sheria ya upatikanaji wa habari ya mwaka 2016. Hali hii inafanya haki ya msingi ya mtu kupata taarifa sahihi kukiukwa Kwa kiwango kikubwa sana na ni vyema mamlaka kuhakikisha upatikanaji Bora wa habari Ili kuijenga jamii mpya inayofurahia upashanaji habari.

DEMOKRASIA NA UZALENDOView attachment 2378188

Nchi ya Tanzania inafanya siasa za vyama vingi tangu ilipoanzishwa mwaka 1992 na kutekelezwa Kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1995. Mfumo huu kama ulivyodadavuliwa na wataalamu wengi kwamba unaongeza uwazi na uwajibikaji na kuruhusu serikali kusimamiwa ipasavyo na vyama vya upinzani. Pamoja na faida hii kubwa sana katika maendeleo ya kiuchumi, Andiko langu linapenda kuwakumbusha watanzania kuwa utekelezwaji wa democrasia ni lazima uende sambamba na uzalendo wa wananchi wote.

Imekuwa desturi ya vyama tawala na vyama vya upinzani kuonesha kwamba hakuna jambo ambalo upande mmoja litafanya likasifiwa hata kama jambo Hilo ni zuri na Lina tija Kwa taifa. Hali kadhalika si jambo la ustawi pale ambapo chama chenye nguvu kinapojaribu kukwamisha haki za kisheria za chama kingine Ili kisiweze kutekeleza majukumu yake Kwa mujibu wa sheria. Ndio maana nimeandika demokrasia na uzalendo kwani kila mmoja katika makundi haya akijua kuwa lengo kubwa ni kunyanyua maendeleo ya Tanzania na sio tumbo lake, basi atakuwa na uwezo wa kukosoa kile kinachopaswa kukosolewa Ili kilete tija Kwa taifa na pia hatasita kupongeza na kuboresha kile ambacho kimefanywa na upande wa pili kwakuwa lengo kubwa ni kuifanya nchi kipaumbele Cha kwanza.

UKOLONI MAMBO LEOView attachment 2378189
Picha kutoka Kwa elenga mbuyinga. (Mwandishi)

Watawala wetu ni lazima wawe makini na zimwi hili lenye malengo maovu kabisa na ustawi wa jamii yetu. suluhisho kubwa la kuondoa janga hili ni kutengeneza sera Bora za kujitegemea na kuwekeza katika sekta zitakazowezesha kundi kubwa la wananchi kujiajiri Ili kukuza Pato la nchi yetu. Mikataba ya mataifa makubwa imekuwa sio salama kabisa katika nchi nyingi za kiafrika na hivyo kutokuwa makini Kwa viongozi na kukosa fikra za kizalendo kunaweza kufanya nchi yetu kutonufaika na rasilimali yake

Kwa kuhitimisha, ningeomba kila mwana jamii wa Tanzania atambue kuwa ana jukumu kubwa la kuleta mabadiliko katika jamii yetu bila kujali yeye ni kiongozi au ni mwananchi wa kawaida. Na kwakuwa sote tunaamini uwepo wetu Duniani ni matakwa ya MUNGU hivyo tukifanya Yale yanayompendeza tutaibadilisha sana nchi yetu na kuwa sehemu ya baraka kubwa.

Chanzo cha marejeo

- Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

-mtandao
Huu uzi umetulia sana madini yameshiba.
 
Back
Top Bottom