Katiba bora ni ile wananchi wameshirikishwa katiba iliyopo wananchi hawakushirikishwa tunataka katiba shirikishi

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,879
Wadau nawasabahi.Katiba iliyopo ni katiba iliyoandaliwa na makada wa CCM kutoka tanzania bara Tanganyika na Zanzibar kila upande ukiwa na wajumbe wasiozidi 10.

Wajumbe hao walijifungia na kuiandaa katiba hiyo kwa mawazo yao na ya viongozi wa ccm na serikali bila ya kuwashirikisha wananchi ambao ndio wenye nchi na katiba ni yao.

Je, uhalali na ubora wa Katiba hii unatoka wapi wakati wananchi hawakushirikishwa?

Katiba ni ya wananchi na sio viongozi ndio maana katiba iliyopo inawa nufaaisha sana viongozi na kuwagandamiza wananchi.

Kutokana na hilo kuita hii katiba ni bora sio sahihi na ndio maana hayati baba wa taifa aliwahi kusema katiba hii inamfanya raisi awe dikteta.

Rais yeyote atakayeanzisha upatikanaji wa katiba mpya atakuwa anaupinga udikteta.

Tunataka katiba itakayo washirikisha wananchi wote sio kundi la wanachama wa chama kimoja cha siasa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom